Msaada: Dada yangu anaangamia kwa ugonjwa Saratani ya Ini, damu na titi

Louis II

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,030
4,645
Ndugu zangu,

Nipo/ tupo katika kipindi kigumu sana kama familia, dada yetu aligundulika kuwa saratani ya Ini, damu na titi. Vyote hivyo vipo katika stage ya mwisho na mbaya sana na Madaktari wametupasha kuwa hakuna kitu wataweza kufanya kunusuru uhai wa ndugu yetu.

Mioyo imejawa na simanzi kwani tangu juzi tarehe 17 february hali imezidi kuwa mbaya zaidi na yupo ICU anapumulia Oxygen.

Ombi langu ndugu zanguni, kama kuna anayeweza kutusaidia au kutuelekeza katika tiba au dawa mbadala ambazo pengine zinaweza kumponyesha au kumpa nafuu kidogo basi atusaidie ili tuweze kuokoa uhai wa dada yetu.

Ahsanteni!

Update
Hatimaye Dada yangu ameaga dunia mapema leo ijumaa tarehe 21/02/2020 . Binafsi sina la ziada zaidi ya kumshukuru mungu na nyote ambao mliguswa pale nilipowapatia taarifa za ugonjwa wake na hata kunitia moyo na kunishauri kwa namna ambavyo mliweza. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe!!
R.I.P dadaangu kipenzi.🙏🙏🙏🙏🙏

PIA SOMA
 
Rafiki yangu alikua na kensa ya kongosho, alipewa wiki kama sita za kuishi kwani ilishaenea sana.

Yeye ni Myahudi kwa imani yake. Aliwenda kumuona Rabbi kwenye sinagogi lao na kumueleza. Walifanya maombi na Rabbi alimwambia aachane na chai na kahawa, alimpa list ya vyakula.

Chai ni herbs tu hata mchaichai unafaa bila sukari. Broccoli, mananasi, mchele pori ule wa hudhurungi. Maji anywe mengi na ikiwezekana badala ya maji anakunywa herbs.

Mpaka sasa anadunda na anaendelea na kazi.
 
Kama yupo ICU hali yake ni mbaya sana halafu ni kansa 3 kwa pamoja ila lingalipo tumaini maana lisilowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu linawezekana tena ndani ya muda mfupi tiba ya kwanza ni maombi kwa Baba wa mbinguni ikiwa ni mapenzi yake na apone.

Jambo la pili yeye mwenyewe mhusika pamoja na nyie mnaomuuguza msikate tamaa msione ndiyo mwisho, tatu chakula kama anaweza kula atumie matunda hasa citrus fruits, mboga za majani kwa wingi na akate matumizi ya sukari kabisa.
 
Sasa mnaambiwa mgonjwa anapumulia mashine na yupo katika terminal stage, hayo matunda sijui brocoli, atavipitishia wapi, ni kumwombea tu israel aitwae roho yake maana mateso anayopata ni makubwa kuliko maumivu na machungu mnayopata ndugu akiwa katika hali hiyo.
 
Back
Top Bottom