Msaada: Bata wanatoa kinyesi cheupe, ni ugonjwa gani huu na tiba yake ipoje?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,407
74,033
Bata wanakunya kinyesi cheupe (kawaida huwa wanatoaga kinyesi cheusi), hawana kabisa hamu ya kula, kunywa maji na wanaishiwa nguvu na kutembea goigoi.

Please, nisaidieni ni ugonjwa gani na tiba yake.
 
Lumala hiyo,aka lendela. Watakufa wote. Wape maji yenye chumvi.
Lendela /lumala ni nini kwa kiingereza nime google halipo kuhusiana na magonjwa.

Tatizo ni unywaji na bata si rahisi kumnywesha kwa nguvu.
 
Wako mbali sana umeshindwa kuweka kapicha
Wana afya, wako vizuri kimwili, hawajakonda wanene lakini hawako active kama ninavyowajua. Ulikuwa ukileta chakula wanakutafuna miguu ukichelewa kuwapa na wanamaliza hapo hapo,, unaongeza wanamaliza,then wanatulia! mpaka wanye sana, then unawapa tena. maji walikuwa wanakunywa kwa wingi sasa wanakunywa kidogo.

Note: Lishe najitahidi kuwapa starter/majani/ mchanganyiko wa vyakula mbali mbali kutoka watengenezaji wa vyakula vya mifugo
 
lendela /lumala ni nini kwa kiingereza nime google halipo kuhusiana na magonjwa.
tatizo ni unywaji na bata si rahisi kumnywesha kwa nguvu.
Inshort ugonjwa wa kuhara, so lazima wakose nguvu.
 
Ungewaona Wataalam Kwenye Maduka Ya Dawa Za Mifugo Kupata Angalau Dawa Itakayofaa Kabla Hujapata Hasaraa
 
Pole Mkuu, najua hali uliyo nayo kwa sasa. Viumbe wako ukiwazoea wakiugua nawewe pia ni kama umeugua kama nakuona vile hujapata usingizi leo.
Sure , ila wana improvement, wameanza kula na kunywa maji. Nilitumia utaratibu wa kuomba msaada kwa wauzaji wa dawa za mifugo. It seems to work. na sasa niliamka kuwapa dawa tena. Imagine una ngombe anatoa lita 20 za maziwa a day, anaugua, huwezi kulala! I have one! Thanks for carering!
 
Back
Top Bottom