Mapand
Senior Member
- Nov 9, 2022
- 134
- 202
Habari wakuu!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mimi ni kijana wa miaka 25, naishi Mafinga-Iringa (na ndiyo nyumbani) nilipozaliwa.
Sasa baada ya kuhitimu chuo miaka miwili iliyopita na katika kuendelea kufikiria namna ya kupata mtaji wa kufungua biashara yoyote yenye kunifanya nikaendesha maisha na yasinisumbue sana hata baada ya kuoa, bahati nzuri ndugu yangu mmoja aliniamini akanihitaji nisimamie biashara zake na ninashukuru Mungu niliweza kusimamia biashara.
Mpaka naondoka kwenye usimamizi wa hizo biashara mwezi uliyoisha juzi, palikuwa na maendeleo makubwa ya kukua kwa biashara pamoja na kuongezeka kwa wateja kwa wastani wa asilimia hata sabani ukilinganisha na mtangulizi wangu aliyekuwepo kabla yangu, japo naye hakufanya vibaya sana.
Sasa katika kutafuta fursa za kibiashara hapa mkoani kwetu (Iringa) nikaona biashara ambayo naweza kuifanya na ninaipenda ni ya timber production (uzalishaji wa mbao).
Kusema ukweli kwa hapa Mafinga kuna masoko mengi sana ya mbao na wanunuaji wanalipa cash bila usumbufu wowote.
Lakini tatizo la hawa wanunuzi wa mbao (Wachaga) nakiri kabisa ndiyo waliyoharibu bei za mbao kwenye masoko ya hapa kwetu kwasababu pesa wanazonunulia ni ndogo sana ukilinganisha na ugumu wa kazi yenyewe.
kwasababu ninayezalisha mbao kumbuka nanunua mti kama ulivyosimama na kumbuka katika shamba utakuta karibu kila mti unauzwa bei yake, sasa hasara huja pale kama hukufix vizuri bei ya kila mti kulingana na size ya mbao itakayozalishwa kwenye mti husika.
Sasa kutokana na changamoto ya bei ya kuuzia mbao kwa hapa nyumbani (Mafinga) nikafikiria kupeleka mwenyewe kwenye masoko makubwa yaliyopo Dar es Salaam, kutokana na bei zao kuwa nzuri kidogo kwasababu kwa masoko ya mbao hasa pale Buguruni bei niliona ziko juu sana ukilinganisha na bei ya huku kwetu, hata kama kuna transport costs na gharama zingine za ushuru serikalini.
Tatizo kubwa lililopo Dar ni madalali, tena bora wawe waaminifu, lakini hawa watu ni wahuni kiujumla na ninaweza kuwaita suyo madalali tena kwasababu udalali ni kazi halali na inatambulika na serikali.
Nasema madalali wa Buguruni ni wahuni na matapeli kwasababu kuna ndugu yangu alishawahi kupeleka mzigo wa mbao pale na akatapeliwa mpaka leo huwa anaziba maskio kabisa kupeleka mzigo Dar es Salaam hata kama siyo Buguruni tu.
Baada ya kujieleza kwa urefu zaidi, naomba kama kuna mtu yeyote anayeweza kuniunganisha na mfanyabiashara wa mbao (anayenunua kwa jumla) ili tufanye biashara kwasababu kikubwa ni uaminifu tu.
Natanguliza shukrani zangu kwenu.