Utingo
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 10,270
- 8,033
Muda wote nikifuatilia huu mjadala wa Richmond/Dowans na sasa hawa jamaa wa IPC ndani ya mix, namuelewa vizuri sana John Perkins aliyeandika kitabu cha "Confessions of an Economic Hitman".
Ukiunga dots vizuri unaona hiyo kampuni ya IPC inavery powerful political connections ndani ya UK. Kwa hiyo in hindsight hao waingereza MI-5/MI-6 pamoja na CIA wanatumia mwanya wa ujinga na ulafi wa viongozi wetu kuhakikisha hatutoki kwenye lindi la umaskini. Hivyo basi tutaendelea kuwategemea wao kwa vizazi na vizazi vijavyo.
Mwanzo ni huu ulipaji wa Tsh billioni 185. Pesa hii kama itabaki Tanzania itasaidia kupunguza mortality rate ya watoto wanaozaliwa kwa kiasi gani? surely tutashuka tokea tulipo hivi sasa watoto 69 wanakufa kati ya 1000 wanaozaliwa. Hao kina Makamba, RA,JK, EL pamoja na ndugu zao hawajawahi kupoteza mtoto kutokana na complications ndogo tu ambazo zingeweza kutatuliwa kama kutakuwa na madawa,waganga walio motivated.
Leo hii wabunge kumaliza term ya miaka 5 tu, wengine wanachukua pesa kufikia TSh 100m. Muhimbili National Hospital sidhani kama kuna Daktari bingwa yeyote ambaye ameshawahi kulipwa kiasi kinachozidi milioni 20 katika kipindi hicho. Hii inaonyesha vipaumbele vyetu vipo wapi. Yaani leo hii madaktari hawalipwi hata Risk Allowance ya kufanyia kazi kwenye mazingira magumu (wagonjwa wenye damu zenye virusi nje nje) yaani unaenda kazini inakuwa ni risk ya uhai wako. Unaweza ukarudi nyumbani kwako tayari umepata maambuki ya VVU. Hapo sasa kati ya Wabunge na Madaktari nani ni wa muhimu? Tulivyo na akili mbovu/fupi tunafikiria kukimbilia India, lakini ukipata Heart Attack kwanza utaanzia MNH "Mtakuja National Hospital" pale triage, mpaka utakapo pata nafuu kama utasurvive. Mungu tusaidie!
Nawasilisha.
wananchi wa kawaida wako katika msiba mkuu