MRISHO MPOTO na siku ya UKIMWI duniani.

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Kesho terehe 1/12 ni siku ya UKIMWI duniani, je wadau mmejiandaa kuadhimisha namna gani?. Mimi naadhimisha kwa kusikiliza wimbo wa Mrisho Mpoto uitwao mtu huru, sijawahi sikia wimbo wenye kugusa hisia na kufariji kuhusu UKIMWI kuliko huu.

Je wajua Jacob anaishi na virusi mwaka wa ishirini sasa!?
Alitaka kujiua mwaka wake wa kwanza lakini shangazi yake akamwambia asikate tamaa
Je dawa ikigundulika leo si itakuwa ni heri yeye aliye subiri!?
Vunja mwiko wa uoga uwe mtu huru kwa kujua hali yako. fikiri kuhusu mashaka uliyo nayo?
Ukipata mafua unaugua mara mbili, ukipata uchovu kwa kufululiza night unachanganyikiwa''

Jamaa kaandika mashairi mengi sana yanayohamasisha kupima na kufariji walioambukizwa. Nategemea nyimbo kama hizi zitapigwa sana kesho.

nawatakia maadhimisho mema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom