Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Disemba 1, ya kila mwaka ni Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.

Siku hii hutumika kuikumbusha Jamii juu ya mapambano ya kumaliza unyanyapaa kwa Waathirika wa VVU na kukuza hatua za kuzuia, kupima, kutibu na pia ni fursa ya kuwaenzi waliopoteza Maisha pamoja na wito wa kufanya kazi ili kuelekea siku ambayo UKIMWI hautakuwa tishio tena kwa Afya ya Umma.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka 2023 ni “ACHA JAMII IONGOZE”.

Maadhimisho ya kwanza ya Siku hii yalifanyika Mwaka 1988, yakitoa jukwaa la kuongeza uelewa kuhusu VVU na UKIMWI pamoja na kuwakumbuka wale waathirika ikiwemo kuonesha alama ya Utepe Mwekundu inayotumika kama ishara ya umoja na msaada kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Japokuwa athari za janga hili zimekuwa kubwa, zikigusa watu binafsi, familia na Jamii zote, kumekuwa na maendeleo makubwa katika kukabiliana na UKIMWI kutokana na jitihada za utafiti wa Matibabu, kuongezeka kwa upatikanaji wa kinga na uelewa mpana wa VVU.

Dunia inaweza kumaliza maambukizi ya UKIMWI ifikapo mwaka 2030 iwapo tu jamii zilizo mstari wa mbele katika kutokomeza Maambukizi mapya zitapata msaada ambao zinahitaji kutoka Serikalini na kwa wahisani.

Baadhi ya mambo yanayotajwa kukwamisha juhudi za kutokomeza UKIMWI ni pamoja na Sera na Udhibiti wa Serikali, Upungufu wa Fedha, Uwezo Mdogo na Ukandamizaji wa Mashirika ya Kiraia na Haki za Binadamu kwa Jamii zilizotengwa.

Endapo vizuizi hivyo vitatatuliwa, mashirika yanayoongozwa na jamii yanaweza kuongeza msukumo zaidi kwa kukabiliana na VVU kote duniani.
 
Siku hizi watu hawaogopi kupata maambukizi, wanaamini hata wakipata VVU kuna dawa za kufubaza ugonjwa zinatolewa bure.

UKIMWI upo, na Unaua.
 
Ukimwi hauna dili tuendelee kuzagamuana tu maisha mafup haya
 
Back
Top Bottom