Mrembo aliyepotea

84.
Nguvu ya mwili ikaendelea kumuisha Alice. Akajihisi mwili wote kumtetemeka haswa sehemu ya magotini kukosa ushirikiano. Macho yake yote yakawa bado yanawaangalia wale mapolisi kwa upande wa chini yake. Wale mapolisi wakawa hawamwangalii tena zaidi ya kuwashuhudia wakiendelea kumuhoji yule mhudumu wa mapokezi.

“Mungu baba weza kunisaidia kutoka katika hii sehemu”
.
Alice akajikuta akiomba sala taratibu. Mwili wake ukawa bado hauna uwezo wa kutembea. Akainama chini kabisa kwa kukosa nguvu nakuanza kujiburuza huku akitafuta chumba kile alichofikia. Aliendelea kujikokota kwa utaratibu mithili ya mnyama aliyekosa ama kuumizwa miguu. Hakukuwa na msaada wowote kutokana na kila mmoja aliyepangisha hapo hotelini kujifungia ili kupisha uchunguzi uliokuwa ukifanywa hapo chini na mapolisi. Hatua chache alizotumia kujiburuta Alice zikamfanya akaribie maeneo ya mlango wa hoteli lakini hakikuwa chumba alichokuwa amepanga Aloyce hapo awali.

“What are you doing here ?” (Unafanya nini hapa?)

“Please help me?” (Nisaidie tafadhari?)

Alikuwa ni mmoja wa wapangaji pale hotelini. Alikuwa amefungua mlango kwa uwoga baada ya kuhisi kama kuna mtu anaugusa mlango wa chumbani mwake.

“Means you did’nt hear the command of the police?” (Inamaana amri ya polisi hujaisikia?)

Yule dada akaendelea kumhoji Alice na safari hii akaongeza sauti zaidi na kuongea kwa sauti ya juu kidogo hali iliomfanya Alice kuendelea kutetemeka kwa uwoga.

“I heard “ (Nilisikia)

Alice akajitahidi kujitetea kwa yule dada huku akifungua pochi yake nakutoa ufunguo wa chumba chake hali iliomfanya yule dada aamini kama Alice naye ni mpangaj kama yeye katika hotel ya Darlington. Kwa huruma ambayo ilikuwa imemuingia yule dada kwa muda mfupi akajikuta akichukuwa mikono yake nakuigusanisha na ya Alice kisha akamvuta nakumuingiza ndani ya chumba chake moja kwa moja nakumkalisha katika kochi la chumbani kwake.

“Tell me where are you from?” (haya niambie watokea wapi wewe?)

“M’ from Uganda” (Natokea Uganda)

Alice akadanganya kwa makusudi ili tu asiweze kujulikana.

“I’m from Kenya and we are neighbors because we all live in one East Africa zone. So you know Swahili?” ( Mimi natokea Kenya na ni jirani yako kwa sababu wote tunaishi ukanda mmoja wa afrika mashariki. Kwahiyo unajua Kiswahili?”

“Ndio najua!!”

Alice akamjibu kwa kutumia lugha ya Kiswahili nakumfanya yule dada aamini kama Alice anatokea afrika mashariki tena nchi ya Uganda.

“Nafurahi kukusikia hivyo. Naitwa Achieng, Sijui mwenzangu waitwaga nani vile?”

“Naitwa Jacky”

Alice ikambidi kuongopa jina lake. Hakutaka kabisa Achieng ajue anaitwa nani na hata anapoishi. Alice akajikuta yale maumivu aliokuwa nayo muda mfupi uliopita katika miguu yake kama yakimuisha taratibu. Furaha ya moyo ikaanza kumtawala hata lile tumbo ambalo lilikuwa kama linamkata likaanza kutulia kwa maumivu.

“Mie nalikuja hapa kwa harusi ya my brother aitwa Alongise Mangaliwa na ilikuwa yafanyika Darlington 1, sijui kwa wewe mwenzangu au tulikuwa kwa wote Darlington 1?”
 
85.

“Hapana!. Hapa unaponiona sikuja kwa harusi bali nilikuwa na bwana wangu tumekodi chumba kwa ajili ya ku enjoy naye kwa sababu bwana wangu huyo ni wa huku huku Nigeria na mara nyingi huwa nakuja huku kwa ajili yake.”

Katika maisha ya Alice hata siku moja hakuwahi kuwa muongo na wala kitendo cha kudanganya kwake alikuwa hajui lakini kutokana tu na uwoga wa tukio ambalo lilitokea usiku wake Alice ikambidi atumie uongo kumdanganya Achieng na hiyo yote nikujiweka katika mikono salama asijulikane kama alikuwa bibi harusi usiku wake katika ukumbi wa Darlington 2. Maongezi kwao yakawa marefu sana japokuwa Alice alikuwa mwingi wa maneno. Wakiwa bado katika hali ya maongezi mara gafla mlango wa chumba chao ukapigwa hodi kwa nguvu. Alice akamzuia Achieng Kwenda kufungua akaenda yeye na aliposogelea mlangoni akatoa ile kadi ya kufungulia mlango kisha akainama kwa kutumia jicho moja mpaka katika kitobo cha mlango nakuchungulia.

“My God, polisi tenaa?”

Alice akawa ameshagundua mavazi ya polisi wa ki nigeria ambao walikuwa wakibisha hodi. Akajihisi mwili kumuishia nguvu sambamba na kuanza kuhema kwa haraka zaidi.

******

“Alice yangu iko wapi, were is my Alice??”

Aloyce alijikuta amerudiwa na fahamu na kitu kilichokuja kumshtua ni kitendo cha yeye kujikuta akiwa kwenye kitanda cha hospitali huku mkono mmoja akiwa ametundikiwa dripu. Pembeni yake mapolisi zaidi ya sita walikuwa wamemzunguka kuhakikisha anapatiwa matibabu ipasavyo kutokana na kuwa mtu mkubwa tena mtoto wa rais kutoka Rwanda.

“Calm down, Calm down Aloyce. By the way Who is Alice?” (Tuliza kwanza jazba Aloyce. Hata hivyo Alice ndio nani)

“My wife” (Mke wangu)

Aloyce alizidi kuwa mkali. Akili yake haikuwa sawa kutokana nakupoteza kabisa kumbukumbu. Kumbukumbu ya tukio ambalo lilifanyika usiku wake. Hakujua hata imekuwaje yupo pale hospitali zaidi yakuendelea kutoa macho hapa na pale akimwangalia mchumba wake Alice kama na yeye yupo mazingira yale ya hospitali. Mavazi ya kipolisi tena ya mapolisi wale wa ki Nigeria ndio yaliomchanganya zaidi Aloyce. Akajitahidi sana japo kurudisha kumbukumbu za yeye kuwa pale mazingira ya hospitali lakini bado akili yake ikawa haifanyi kazi ipasavyo.

“I ask again, where is she?” (nauliza tena mke wangu yuko wapi?)

Hasira kali zikawa zimeshatanda ndani ya halmashauri ya kichwa cha Aloyce. Akajikuta akiinuka kwa kutumia nguvu kitandani kisha akachomoa mirija ya dripu nakuanza kunyanyuka kabisa kwa kuondoka.

“Now I find myself” ( Nitamtafuta mwenyewe sasa)

Aloyce akataka kutoka katika lile eneo lakini akashindwa kutokana na kuzidiwa nguvu na wale polisi wa ki Nigeria. Kwa amri ambayo walikuwa wamepewa kutoka makao yao makuu kumsimamia na kuhakikisha anapatiwa huduma muhimu zote hapo hospitali kuokoa maisha yake kisha kurudishwa kwao Rwanda. Aloyce akazidi kusumbuana na mapolisi mpaka wakaafikiana kumpeleka wodi ambayo baba yake alikuwa amehifadhiwa kwa matibabu. Kitendo cha kuingia tu macho yake moja kwa moja yakatahamaki kuonana na baba yake akiwa hoi kitandani akiwa kifua wazi.

*******

Mwili wa mke wa rais wa Rwanda, Kagwa ulikuwa tayari umeshafikishwa mochwari katika hospitali kubwa ya Faith City, Lagos, Nigeria. Maiti zilikuwa nyingi lakini zilikuwa katika hali ya kutokutambulika. Ni mke wa rais Kagwa na Janet pekee ndio walioweza kutambulika kutokana na eneo la vichwani mwao kuonekanika huku wakiwa hawana viungo vyote vya chini. Taarifa zikawasilishwa moja kwa moja kwa rais Kagwa Kwisereka ambaye naye alikuwa akitibiwa hospitali kwa tukio hilo hilo hilo la bomu. Akiwa bado njiani huku akionekana kupooza upande mmoja mzima kutokana na tukio la bomu. Kabla hawajafika hospitali ya FaithCity rais Kagwa akawa ameshapoteza fahamu. Gari la huduma ya kwanza la polisi wa ki Nigeria likafanikiwa kufika hopsitali ya Faith City huku rais Kagwa akiwa katika kupoteza fahamu. Wakajitahdi sana kuhakikisha fahamu zinamrudia kwa kumuwekea dripu sambamba na kumchoma sindano za ufahamu. Ikawachukuwa zaidi ya nusu saa madaktari wa hospitali ya Faith City kuhakikisha rais Kagwa anarejewa na ufahamu. Katika hali ya kuhangaika kwa madaktari hatimaye rais Kagwa akarudiwa na ufahamu japokuwa alikuwa bado hajitambui kitu gani kimemfanya yuko pale.
 
86.

“Mr. president, you should settle this treatment first. It is only a small accident which occurred.” ( Mhesimiwa rais, unatakiwa kutulia kwanza kwa matibabu hii ni ajali ndogo tu imekutokea)

“Accident? Which accident and Why have I been here?” (Ajali? Ajali ipi? na kwanini nimekuwa hapa?

Rais Kagwa akawa kama mtu aliyepigwa na butwaa. Akawa hajitambui tambui kwa sababu gani yupo maeneo yale.
.
“where is my wife?” (Mke wangu yupo wapi?)

Bado kumbukumbu zikawa hazijamrejea vizuri. Akiwa katika hali ya kustaajabu mara akashangaa mtoto wake, Aloyce akiingia hospitali na pembeni yake akizungukwa na mapolisi kama hao hao.

“Aloyce, Aloyce manangu?”

Rais Kagwa akajikuta akitoa mshangao baada ya kuonana uso kwa uso na mtoto wake, Aloyce. Mwili wa rais ukawa katika hali ya kuishiwa nguvu sambamba na macho yake kukosa nguvu na ushirikiano kutokana na kutokuvaa miwani.

“Daady, Dady, mumy is..”

“Where is she?” (yupo wapi?)

“Dady my mumy is dead?” (Baba mama yangu amekufa)

“Whaaaat? Unasemaje aloyce? Nani kamuua?”

Mshtuko wa taarifa ya kufariki kwa mke wake rais Kagwa toka kwa Aloyce kukaibua majonzi upya. Rais Kagwa akajihisi kizungu zungu katika kichwa chake. Ile presha ya kushuka aliokuwa nayo kipindi cha nyuma ikamrejea upya. Msisimko wa mwili kwa upande ule ambao ulikuwa haujapooza ukaanza upya. Aloyce akamsogelea baba yake na kumkumbatia kwa nguvu na kwa hisia zote huku akitoa machozi. Machozi yale ya uchungu. Akamkumbatia zaidi ya dakika mbili lakini kitendo cha kumuachia tu baba yake akawa kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Mwili wake wote ukawa umemkakamaa, Rais Kagwa akawa ameshakauka kwa kuaga dunia. Aloyce hakulitambua mapema.

“Dady? Dadyyyyyyyyyyyyy??”

Aloyce alitoa sauti kali kumuita baba yake japo ashtuke bila majibu yoyote. Hakuweza kuisikia tena sauti ya baba yake akimjibu zaidi ya kushuhudia akikauka kwa kuganda mithili ya barafu. Madaktari wakaamuru Aloyce asogezwe pembeni kisha wakamfunga macho rais Kagwa nakuamuru iletwe machela ya kubebea maiti haraka. Wakampakiza rais Kagwa katika machela ya kubebea maiti tayari kwa kuelekea mochwari kuuhifadhi mwili wake.

“Daddyyy kwanini naacha mimi. Dady please come back, rudi dady yangu, damn?”

Hasira kali zikamtawala Aloyce. Hasira Zilizochanganyikana na uchungu wa kuwapoteza wazazi wake wote wawili mama na baba yake. Akili yake yote ikarejea kwa Janet nakuamini moja kwa moja analijua tukio zima la kujilipua kwa bomu. Akaomba mapolisi wampatie mkanda wowote ambao umerekodiwa tukio zima lilivyokuwa. Mapolisi hawakuwa mbali na ushuhuda ule. Tayari walikuwa wameshajipanga kwa kila kitu. Wakamuamruru kwanza Aloyce atulize jazba wakampeleka mpaka makao makuu ya polisi nakuanza kumuwekea mkanda uliokuwa umerekodiwa matukio ya harusi zote mbili zilizofanyika usiku ule. Aloyce akawa akitetemeka huku akiuangalia mkanda kwa hasira zote. Kitendo cha baba yake kuingia akiwa na mama yake sambamba na bodigadi wake aliyekuwa akimfahamu. Akaangalia kwa umakini msichana wa kwanza kabisa alivyomfuata baba yake ukumbi wa Darlington 1. Akarudisha mara mbili mbili japo kumgundua kwa sura lakini hakuweza kumfahamu. Mkanda ukapekekwa mbele zaidi. Ukaonesha tukio la harusi yake katika ukumbi wa pili wa Darlington 2. Ukaanza kumuonsha Janet kuanzia anatoka ukumbini na kwenda chooni huku akimuacha Aloyce akifungua shampeni ukumbini. Ukaendelea kumuonesha Janet akiwa chooni akiyarekebisha mabomu kiunoni mwake.

“My god, kumbe Janet ni muuaji?”

Aloyce akastaajabu kwa kumuona Janet akiyafunga vizuri mabomu yale kiunoni. Moja kwa moja mkanda ukaendelea kuonesha Janet akirudi kutoka chooni na punde alipotoka tu akaunganisha moja kwa moja kuwafuata rais Kagwa na mke wake ambao walikua tayari wakiingia ukumbini hapo nakuwakumbatia.

“Stoop?”

Aloyce akaamrisha mkanda usimamishwe. Akili yake ikawa imeshatambua kila kitu. Kitu alichokitambua ni usiri kutoka kwa mke wake Alice. Akaona uchungu, ule upendo wa kumpenda Alice mpaka kuhakikisha anafunga ndoa naye ukampotea kwa ghafla. Akaona uchungu wa ndoa ndani ya masaa 24 tu. Kitendo cha kuwapoteza wazazi wake wote wawili ambapo kumesababishwa na Janet kuwaua kukamuingia Aloyce kichwani mwake vilivyo.

“Where is Alice?” (Alice yuko wapi?)
 
87.

Aloyce akawageukia wale mapolisi nakuwahoji kwa ukali. Akaamuru Alice atafutwe popote alipo ikiwezekana auliwe kabisa ama afungwe kutokana na kuhusishwa kwa vifo vya baba yake na mama yake. Mapolisi wakatii amri yake kwa kuondoka pale hospitali ya Faith City nakwenda mpaka hotelini kumfuatilia Alice. Mapolisi walipofika tu hotelini wakaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine na walipofika chumba cha mwisho wakabisha hodi bila kufunguliwa. Wakarudia mara mbili tatu bila majibu yeyote. Wakamtuma mmoja wao aende mapokezi kuangalia kamera kujua kama kuna watu katika hicho chumba. Ndani ya muda mchache wakawa wameshagundua kuna wasichana wawili na tena wako maeneo ya mlangoni wakichungulia kwenye tundu la mlango.

Mapigo ya moyo ya Alice bado yakawa yanaenda mbio. Mbio zaidi ya farasi wale wa jangwani. Akahisi mkojo mwepesi kupenyeza katika nguo yake ya ndani.

“Tuwafunguliage vile nataka kuingia?”

Achieng alimuamuru Alice afungue ule mlango. Kwa kutumia ishara ya kichwa, Alice akaonekana kutokuafiki kabisa kitendo cha kufungua mlango, akakataa.

“Nikwambie kitu Achieng?”

“Yeah waweza ni tell”

“Mi naelekea kujificha then after two or three minutes waweza kufungua mlango wako”

“Hapana Alice, bado sijakunyaka fresh, kwani kuna mikosa yeyote humu kwa ndani nafanya mimi au wewe na kwanini tuongope?”

Achieng akazidi kuwa mbishi hali iliomfanya Alice akimbie mule chumbani huku akiwa hajitanbui kama kamera za ulinzi zinamuangalia kwa kila atakachokifanya. Akaingia mpaka chooni nakujifungia mlango.
********

Mapolisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiaskari ya mapolisi wale wa naijeria bado walikuwa mlangoni katika hoteli ya Darlington 1. Walishajua kila kitu kuhusiana na wasichana wawili waliokuwa katika chumba ambacho walikuwa wakitazamana nacho. Kwa msaada wa kamea za ulinzi ambazo zilifungwa kila kona ya hotel ya Darlington zikawa zimewasaidia vya kutosha. Zaidi ya dakika kumi walikuwa wakigonga mlango bila majibu yeyote. Wakaamua kuuvunja.

“Where is colleague?” (Mwenzako yupo wapi?)

“I was alone in this room?” (Nalikuwa pekee yangu kwa hii chumba)

Achieng akajitetea mbele ya mapolisi baada ya Alice kumtoroka nakujificha.

“Do you know Alice, who you were with him in this room?"(Unamfahamu Alice ambaye mlikuwa naye humu chumbani?)

“No. (Hapana)

Hasira kali zikawajaa mapolisi kwa uongo ambao Achieng alikuwa akiwadanganya. Uongo wa kukataa kuwa alikuwa na mwenzake. Kamera zilikuwa na jibu tosha kwamba walikuwapo wawili tena nyuma ya mlango wakichungulia kupitia kitundu cha kitassa lakini Achieng alikuwa akijitahidi kumficha Alice asijulikane yupo wapi. Akaambulia makofi na mateke toka kwa baadhi ya mapolisi waliokuwa na hasira za karibu.

“We offer only one minute, tell us where is colleague?” (Tunakupa dakika moja pekee utuambie mwenzako yupo wapi?)

Kutokana na kuumizwa sana kwa Achieng na mapolisi. Uzalendo ukamshinda akajikuta akioneshea kwa mkono wake mmoja eneo ambalo Alice alikimbia kujificha. Mapolisi wakamwacha Achieng nakufuatailia mlango wa kuingilia chooni ambapo Achieng aliwaoneshea kwamba Alice kakimbilia humo. Wakaugonga mlango ule wa chooni zaidi ya mara mbili napo hakukuwa na majibu yeyote zaidi ya kuwa kimya kwa muda. Wakauvunja kama walivyouvunja wa awali wakuingilia ndani.
 
88.

“She is not here, ooopeeeii?” (Hayupo, ooppeeiii?)
.
Polisi mmoja wapo akahoji kwa mshangao. Hakukuwa na dalili yeyote ya mtu mle ndani japokuwa mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani. Wakaanza kukagua eneo zima la chooni mpaka bafuni. Choo pekee ndicho hakikufungwa kamera za ulinzi hivyo ikawaweka katika wakati mgumu wa kutambua Alice atakuwa kajifichia wapi. Baada ya kukagua kwa muda wa dakika mbili wakagundua kitu. Kipande cha Dari ambacho kilikuwa kimeshadondoka

“There! There!!” (Pale!, Palee!!)

Polisi mmoja akaoneshea kwa upande wajuu ya dari. Japo palikuwa na chemba ya kuingilia juu kabisa. Wakaamua kupanda hadi juu ya dari huku wakiwa na tochi. Wakamulika sana kukagua huku na kule endapo watamuona kajificha uko bila mafanikio yeyote. Wakiwa bado katika hali ya kuchanganyikiwa kwa kutoroka Alice kupitia juu ya dari punde Aloyce akatokea.

“Where is Alice?” (Yupo wapi alice?)

“Papaa!! Alice is not here, She passed over there?” (bosi Alice hayupo hapa, katorokea paleee?)

Akaongea mmoja wa polisi kumwambia Aloyce. Jasho lililokuwa likimtirirrika Aloyce likamzidia mara mbili yake. Kipupwe ambacho kilifungwa katika kile chumba akahisi kinatoa joto. Kamwe hakutaka macho na masikio yake yaweze kuamini kama Alice kawazidi ujanja.

“Ni muuuaji anatakiwa tumuweke hatiani. Kwanini mmemuacha akawatororka damn?” Aloyce akapandisha hasira. Akachukua tochi kubwa kutoka kwa polisi mmojawapo kisha akavua shati lake nakuwaamuru baadhi ya mapolisi ambao walikuwa wameshaanza kupanda kwenye dari washuke. Akapanda mwenyewe juu ya dari pasipo kuhitaji msaaa wowote. Akaingia bila kuwa na usismamizi wowote. Yale maumivu ambayo alikuwa nayo nakusababisha kupelekwa hospitali akawa ameshayasahau. Hasira kali zikabaki kwa Alice.

“Ole wake iko Napata, naua belive naua?” Aloyce akajikuta akiongea peke yake huku akipanda mule ndani ya dari. Hakulijali joto kali ambalo lilikuwa likiandama mule ndani ya ile dari. Akawa ananyata taratibu uku akimulika hapa na pale bila mafanikio yeyote. Jasho likazidi kumtiririka hali iliyomfanya hasira kumkaa mara mbili yake endapo atamkamata Alice. Akafika sehemu akachoka viungo vyote vya mwili mule ndani na kujiegemeza pembeni huku ile tochi ikionekana kufifia kwa kukosa nguvu ya kumulika.

*******

Ujasiri wa hali ya juu ukawa umejijenga katika halmashauri ya kichwa cha Alice. Kamwe hakutaka kushikwa kwani aliona kama mwisho wake wa kuishi utakuwa umefika. Achieng ambaye alikuwa arafiki yake kwa muda mfupi mule hotelini akaona hana tena msaada kwa kutaka wafungue mlango ili waonekanike mule ndani na mapolisi ambao Alice alishawaona kupitia kitundu cha mlango. Wazo la kukikmbilia chooni na kujificha dhahiri lilikuwa sahihi kwa Alice. Akafanikiwa kujificha chooni na kujifungia mlango huku masikio yake yote akiyaelekeza katika mlango ambao Achieng alikuwa akitaka kufungua. Maneno yote ambayo Achieng alikuwa akihojiwa na mapolisi hadi kufikia hatua ya Achieng kupigwa makofi na mapolisi akilazimishwa aoneshe Alice alipo, akawa ameyasikia kwa utulivu nakuyahifadhi akilini. Akili ya ghafla ikajijenga katika kichwa chake, akapata wazo la kupanda juu ya sinki la kunawia mikono mule chooni kisha akafunua dari iliokuwa na chemba ya kuingilia na kuingia. Akajitahidi sana kuirudishia ile dari kama ilivyokuwa awali ili wasigundue lakini akashindwa kutokana na kumponyoka na kudondoka mpaka chini. Giza kubwa ambalo lilikuwa limetanda mule ndani ya dari halikumtisha kabisa Alice zaidi ya kujisogeza hivyo hivyo akivumilia joto kali la mule ndani. Akiwa bado mule mule ndani ya dari asijue aelekee wapi, ikambidi ajibanze katika kona ya mbao nakutulia huku akiamini lazima wale mapolisi watatafuta chooni kidogo na kuondoka zao.
 
89.
Hakupata kusikia maneno yeyote kutoka chini kutokana muundo wa ile dari ulivyojengeka. Alice akaendelea kubaki kimya asielewe hatma yake ni nini. Akiwa bado kazubaa peke yake darini ndani ya dakika kumi akashangaa mwanga mkali kumulika huku na kule. Mwanzoni akaupuuzia lakini ule mwanga ukazidi kuyasumbua macho yake huku akili yote akiiamishia kwa mapolisi huenda wameingia kwenye dari nakuanza kumtafuta. Akajificha vizuri nakuanza kuufutatilia ule mwanga kuona utaishia wapi. Ule mwanga ukazidi kusogea mpaka maeneo alipokuwapo, kisha ukaanza kufifia taratibu na hivyo kumpa fursa Alice kutambua ni polisi gani ambaye ametumwa kuingia mule ndani ya dari. Akauogelea ule mwanga kwa utaratibu ambao ukawa hauna nguvu ya kumulika mpaka eneo ambalo yule mtu alikuwa kama ameishiwa nguvu baada ya kuingia mule ndani.

“My God, Alooo….”

Alice akajiwahi kujizuia mdomo wake asipayuke baada ya kugundua kuwa yule mtu ni Aloyce. Macho yakamtoka sana. Ujasiri ambao alikuwa amejijengea ndani ya muda mfupi ukamyeyuka ghafla. Akaichukuwa ile tochi toka kwa Aloyce kwa utaratibu huku Aloyce akiwa hajitambui kwa kupitiwa na usingizi. Akaizima na kuitupia pembeni kisha akamgeukia Aloyce hivyo hivyo kukiwa giza nene.

“Aloyce?, Aloyce bado nakupenda na moyo wangu upo kwako lakini nataka ujue ukweli Aloyce. Yule aliyemuua mama yako na bomu siyo mama yangu mzazi. Aloyce mama yangu aliniacha Tanzania nikiwa mdogo sana. Nimehangaika sana mpaka kufikia hapa. Na hii yote Janet amefanya ili baba yako asinichukie. Nilimkataza sana asiweze kujilipua na kufa na mama yako. Sipendi nikavunja ndoa yangu kwako. Niambie kama hunipendi niko tayari nikurudishie pete yako sasa hivi Aloyce ila nakuomba usinifunge sina hatia mimi Alice?”

Alice akajikuta akiongea maneno mengi mbele ya Aloyce. Aloyce hakuweza kusikia hata neno moja kutokana na kupoteza fahamu muda mrefu kutokana na joto la mule ndani pia hakumaliza dripu ambayo alikuwa amewekewa hospitali. Alice akajitahidi japo kumshtua Aloyce bila mafanikio yeyote. Akajikuta maneno yote aliokuwa akiongea kama yamemrudia mwenyewe kutokana na Aloyce kutosikia wala kuwa na ufahamu wowote.

“Aloyce wangu amka basi mpenzi unione, amka niwe katika mikono salama, amka ujue ukweli wangu kwamba Janet siyo mama yangu, amka pliiiizzzz???”

Alice akajikuta machozi mazito yakimtoka yalioambatana na kwikwi, sio kwikwi ya maji la hasha! bali ni kwikwi ya kulia kwa uchungu. Akajikuta anahema kwa juu juu zaidi, akachukuwa mikono yake nakujishika kifua chake lakini bado kilikuwa na spidi kali kwa kuhema. Damu zikaanza kumtirirrika kutokea puani. Kizunguzungu kikaanza kumtawala kuashiria dalili ya ugonjwa wake wa kifafa upo karibu naye. Akajisachi ili atoe kile kichupa chake cha kupulizia pindi akibanwa na pumzi lakini hakuwa hata na pochi wala kitu chochote zaidi ya kuvisahau chini hali iliomfanya alegee nakuanza kutapatapa mwenyewe pembeni ya Aloyce huku povu likianza kumtoka pembeni ya mdomo wake.

******

Taarifa juu ya kifo cha rais wa Rwanda Kagwa Kwisereka zilienea Nigeria nzima. Baadhi ya vipande vya video ambavyo vilipatikana kupitia kamera za ulinzi zilizokuwa zimefungwa kwatika hoteli ya Darlington vikawa vimesaidia kuoneshwa katika baadhi ya televisheni za Nigeria, Rwanda na baadhi ya nchi jirani. Kila gazeti la Nigeria liliandika vyake huku magazeti ya udaku ya Nigeria yakichochea zaidi habari ya kifo cha rais Kagwa.

Kiongozi mkuu wa nchi ya Nigeria brigedia Oliefi akiongozwa na vikosi mbali mbali vya ulinzi kwa pamoja wakazika vipande vipande vya miili ya marehemu ambao hawakuweza kutambulika hata kwa sura. Miili mitatu tu ndio iliweza kutambulika na kuamuliwa kwenda kuzikiwa nchini Rwanda. Kichwa cha mke wa rais wa Rwanda, na kichwa kilichofahamika kuwa ni mama wa Alice ambaye aliolewa na mtoto wa rais wa Rwanda na ndio chanzo cha msiba ule kwa kujilipua kwa bomu pamoja na Rais mwenyewe wa Rwanda, Kagwa.

“Where is his son? " (Mtoto wake yupo wapi?)

Alihoji mkuu wa mazishi brigedia Oliefi kwa sauti ya chini chini.

“"He went seek a girl who responsible for this? (Alikwenda kumtafuta mhusika wa wa tukio hili)

“Where? (Wapi?)
 
90.

“Darlington hotel” (Hoteli ya Darlington)

“"But this should be included immediately after here we are transported to Rwanda for burial?" (Lakini anatakiwa awepo hapa mara moja, baada ya hapa tunasafirisha kwenda Rwanda kwa maziko?”

“ok papaa” (Sawa bosi)

Yule askari msaidizi akatii amri ya kiongozi mkuu wa msafara. Akawachukuwa wenzake zaidi ya kumi wakapanda ndani ya gari kwa ajili ya kumfuatilia Aloyce katika hoteli ya Darlington. Ikawachukua mwendo wa dakika ishirini nzima wakiwa njiani mpaka kufikia hoteli ya Darlington. Ule ulinzi ambao mapolisi wa Nigeria walikuwa bado wameuweka wa kuzuia mtu yeyote asiweze kutoka zaidi ya wafanyakazi wa hoteli bado ulikuwa ukiendelea. Wale mapolisi wakaingia hotelini moja kwa moja wakaelekezwa walipo mapolisi wenzao. Chumba kilikuwa kimevunjwa mlango huku Achieng akionekana kutetemeka sana kwa uwoga wa rundo la mapolisi wengine zaidi kuwasili.
.
“Where is the president’s son? (Mtoto wa rais yupo wapi?)

“Not yet Papaa!!, he went on and did not want any help so we still waited until now to come down” (Bosi bado, alipanda juu na hakutaka msaada wowote hivyo mpaka sasa tunamsubiri ashuke)

Hasira zikamjaa yule polisi aliyekuja kwa mara ya pili. Akaona wanazidi kuchelewa kwa kumsubiri mtu aliyekuwa juu ya dari. Akavua kofia yake ya upolisi.

“"Give me a torch?” (Nipe tochi?)

Akapewa na kupanda peke yake juu ya dari. Akatumia zaidi ya dakika mbili nzima kumulika bila majibu yoyote. Akazidi kusonga mbele zaidi kupitia dari mpaka alipokutana na mwanga mkali kuashiria kuna upenyo wa kutokea chini. Akazidisha kujikokota kwa kishindo. Akafika mpaka katika eneo hilo nakuona kitu.

“Shiit”

Yule polisi akastaajabu baada ya kuona dari imeharibika ishara ya kama mtu kuipasua. Akajirusha mpaka chini ya kile chumba aone vizuri.

“My god!” (Mungu wangu!)

Bado akaendelea kustaajabu baada ya kukutana uso kwa uso na mwili wa mtoto wa rais wa Rwanda ukiwa haujiwezi chini. Macho yake yote yalikuwa kama yametobolewa huku miguu ikiwa nyanga nyanga kwa kulowa na damu. Damu nyingi zilikuwa zikimtiririka kupitia shingoni mwake . hakuweza kuongea kutokana na koo lake kuharibiwa vibaya

*******

Alice aliendelea kujibiringisha mule ndani ya dari huku na kule mithili ya nyoka akiwa ndani ya maji akishindwa kuogelea. Akajihisi pumzi zote zikimuishia kutokana na joto kali ambalo lilikuwa bado likitawa;la ndani ya siling bodi. Akiwa bado katika hali ya kutokuwa na ufahamu Aloyce akashtuka. Akajiangalia vizuri mikononi mwake. Giza totoro ambalo lilikuwa limeteka dari huku nyaya nyaya za kila aina zikipita humo ndani ndizo zimkamchanganya zaidi. Hakuwa na kumbu kumbu yeyote juu ya kufika kwake hapo juu. Akajiangalia mara mbili mbili bila kujigundua yupo mazingira ya aina gani kutokana na giza kuwa nene. Tochi kubwa ambayo alikuwa ameishika mkononi ndicho kitu kilichoanza kumpa kumbukumbu.

“Alice iko wapi?, shenzi kwanini naua baba angu na mama angu?”

Aloyce akabaki akiongea mwenyewe. Akajaribu kuiwasha il tochi lakini haikuweza kuhakisi mwanga wa aina yeyote. Akatoa betri na kuzirudishia lakini bado hakuweza kuambulia mwanga wa aina yeyote. Kitendo cha kutaka kuondoka akajikuta kama amegusana na mwili wa mtu. Akili ya haraka haraka ambayo aliamua ni kupiga chini kwa nguvu kisha akadondoka na ule mwili ambao bado hakuutambua ni nani. Kwa baahati nzuri wakawa wamedondokea katika chumba cha hoteli na tena maeneo ya kitandani.

“Alice?, Alice?”

Aloyce akastaajabu baada ya kuona sura ya Alice. Macho yake yakamtoka baada ya kushuduia zile nguo ambazo alimnunulia kwa mara ya mwisho nakuzihifadhi katika brifkesi bila hata kumwambia. Hisia za kumpenda Alice hakuwa nazo zaidi ya hasira kumkaa mara mbili kila akikumbuka vifo vya wazazi wake baba na mama yake.

“Amuka? Amuka menyewe Alice?”

Aloyce akamtingisha kwa nguvu sana japo Alice ashtuke lakini fahamu bado hazikumrejea. Kwa hasira ambayo ilikuwa bado imemkaa Aloyce akatumia miguu yake kumpiga Alice maeneo ya kichwani na tumboni bila kujali kama ana mimba yake.

“Amuuuuka?”

Maumivu makali ambayo Alice alianza kuyapata kupitia tumbo lake lililokuwa na mimba yakanmfanya kurejewa kwa ufahamu, uchungu ukamshika mara mbilili. Akajihisi mimba inataka kutoka kwa uchungu aliokuwa akiusikia. Damu puani zilikuwa nyingi sana ila zikawa zimeshaganda kutokana na kumtoka kipindi cha nyuma. Macho yake yakamtoka kwa kutazamana na Aloyce.

“Aloyce mume wangu nisamehe mimi sina hatia?”

“Nani mume ako? Why naua dady na mumy angu?”

Aloyce akaichomoa bastola kiunoni mwake na kumnyooshea Alice akitaka kumuua. Akaanza kwa kumpiga mateke ya usoni na kifuani na hata mara nyngine akawa anatumia mkono mmoja kumpiga makofi.
 
91.
“Sali sala zako za mwisho shenzi wewe? Kumbe nakuja kuwa na mie ili uue dady angu? mama ako nakufa na wewe taifata ilipo shenzi kubwa”

Mkojo wa moto mithili ya chai inapochemka ukaanza kumtitririka Alice, akaijona mwisho wa maisha yake umekaribia, hakutaka kuamini kabisa kama Aloyce huyu waliefunga naye ndoa ndani ya masaa ishirini na nne sasa amebadilika. Laana zote akazipelekea kwa mama yake wa kufikia, Janet kwa kitendo alichokifanya cha kujitoa mhanga nakumsababishia matatizo katika ndoa ya muda mfupi.

“Eeeh mwenyezi Mungu nipokee nakuja kwako!!”

Alice akasali sala ya chini chini huku akiendelea kumuangalia Aloyce kwa macho ya huruma.

“Aloyce? Sisi wote ni binadamu, tumeumbwa na tutakufa. Safari yetu ni moja wote tutazikwa tu. Ila nakuomba kabla hujaniua nakuomba uamini kwamba yule hakuwa mama yangu mzazi na mama yangu mzazi alinitoroka nikiwa mdogo sana huko Tanzania. Janet aliamua kunilelea baada ya kuhangaika sana. Lakini nimekuwa mtu nisiye na bahati ya maisha. Haya sasa nakuomba niue tu Aloyce, niuuuuueeeeeee???”

Hasira zikamzidia Alice. Akaanza kutetemeka karibia maeneo yote ya mwili wake. Akamuamuru Aloyce abonyeze ile bastola nakumuua. Aloyce akawa bado mgumu kwa kutaka kumuua. Bumbuwazi likamjaa lililoambatana na udenda kumteremka. Akahema sana huku akitetemeka mdomo na mikono. Alice akatumia fursa hiyo kumsogelea mpaka karibu.

“Haya niue mimi Aloyce, niue nikamfuate huyo Janet huko mbinguni nikamseme. Niue nikamwambie alichoniafanyia maishani, niuuue Aloyce?”

Aloyce hakuweza kuongea chochote. Akawa kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Alice akampora ile bastola na kujioneshea mwenyewe.

“Aloyce umeshindwa kuniua wacha nijiue mimi?”

Bado Aloyce hakuweza kuongea chochote zaidi ya kutoa macho, akawa ni zaidi ya mtu aliyepooza. Alice akiwa katika hali ya kutaka kujiua mara akahisi kishindo kuashiria kuna mtu ama watu wanakuja kupitia dari. Ujasiri wa ghafla ukamuingia Alice katika halmashauri ya kichwa chake. Alichokifanya akatumia ile bastola kumpiga Aloyce miguu yote miwili na baada ya hapo akammalizia shingoni.

“Tutaonana kaburini Aloyce”

Kwa kujiamini Alice akafungua ule mlango ambao ulikuwa umepakana na jikoni kisha akaingia nakutaka kutorokea kwa nje ya hoteli ya Darlington lakini kabla hajatoka tu jikoni mara ghafla macho ya Alice yakakutana uso ka uso na yule mhudumu wa mapokezi akitoka na mapolisi nje. Alice akarudi nyuma kidogo nakujificha huku akiendelea kuwatolea macho. Nguo zake hazikuwa zikitamanika tena kutokana na kuchafuliwa na vumbi kali kutoka juu ya dari pia gauni lake lilichanganyikana na damu damu pindi alipokuwa akimuua Aloyce kwa kutumia bastola. Ule ujasiri ukaendelea kumjaa katika mwili wake hadi katika halmashauri ya kichwa chake. Akachungulia vizuri kwa upande wa nje. Kundi kubwa la mapolisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kipolisi ya ki Nigeria wakawa wanaingia ndani ya magari yao nakuondoka zao huku wakiliacha gari moja la ki polisi.

“Inamaana watakuwa hawajamuona Aloyce?”

Alice akabaki akiusemea moyo wake baada ya kuona mapolisi wakiondoka ndani ya ile hoteli na kuacha wapangaji wote wa hoteli ya Darlington kuwa huru wakitawanyika hapa na pale. Akili yake moja kwa moja ikamrudisha ndani, ndani katika chumba kile alichokifanya mauaji ya mchumba wake Aloyce ili kuhakikisha kama kweli mwili wa Aloyce umeshatolewa. Akajichanganya na ule umati wa wapangaji uliokuwa umetawanyika huku kila mmoja akionekana kuongea yake kwa kulaumu utaratibu uliofanywa wa kuwazuia kwa muda. Alice akiwa anazidi kusonga kuelekea kwenye chumba huku akitumia ngazi mara ghafla.
 
92.

“Alice, Alice?”

Sauti ya kike ikamuita kwa ukali. Alice akageuka kumuangalia ni nani. Woga ukajijenga upya katika ubongo wake. Hakutaka kuamini kama kuna mtu anayejua jina lake. Sauti ile ikazidi kumuita huku ikimuingia katika ngome ya masikio yake. Akaifananaisha na sauti ya mama yake wa kufikia, Janet.

“Mhh!!, lakini mama si alishajilipua na bomu? Sasa huyo ni nani?”

Alice bado akabaki akiongea peke yake akiendelea kutahamaki hapa na pale akikigeuza kichwa chake bila kugundua sauti inapotokea. Mapigo ya moyo yakaanza kubadilika mwendo. Yakasukuma mbavu zake nakusababisha matiti yake kutingishika. Akahisi mwili wote kumtetemeka. Sura ya mama yake wa kufikia, Janet ikawa mbele yake ikijikongoja kwa utaratibu huku ikimfuata. Nguo zilizombana na nywele ndefu ndizo zikamfanya Alice aendelee kutetemeka zaidi ya awali.

“Janet, Mama yangu?”

Midomo ya Alice ikabaki ikipishana kwa kujiuma uma. Moyo wake ukabaki kuamini lakini macho yake yakabaki kukataliana na anachokiona. Yule mwanamama akazidi kusogea mpaka karibu.

“Alice?”

“Mama ulikuwa wapi mama yangu? Ona matatizo yalionikuta Alice mimi. Kwanini mama umeamua kufanya hivyo. Au ulipenda niteseke hivi? Ona sasa nimempoteza Aloyce. Yote sababu yako mama?”
.
“Aliiiiccccceeeeeee?”

Yule mwanamke akatoa sauti ya ukali kwa Alice ambaye alikuwa ameshaanza kububujikwa na mchozi. Hakuwa akimjua Aloyce zaidi ya kumshangaa.

“Aloyce ndio nani Alice?”

Alice akastaajabu tena baada ya yule mwanamke kumfikia karibu nakumuongelesha kiswahili. Akamtolea macho usoni kwa makini. Akajihisi moyo wake kumcheka kwa kumfananisha yule mwanamke na mama yake wa kufikia, Janet. Akashusha pumzi huku akibaki na shauku kubwa ya kumjua ni nani na ametokea wapi.
 
93.

“Kwani wewe ni nani unayenijua jina langu kiufasaha?”

Alice akahoji kwa sauti ya ukali bila kumuogopa.

“Alice? Kweli kumbukumbu huna. Mimi ni rafiki yako mkubwa wa Tanzania.”

Alice akarudisha kumbukumbu kwa haraka haraka lakini hakuambulia kitu. Tanzania hakuwa na rafiki wa karibu zaidi ya marehemu Jamila. Na hata alipokuwa Rwanda hakuwa na rafiki wa karibu zaidi ya mama yake wa kufikia, Janet.

“Samahani nikumbushe mpendwa?”

Alice akashusha pumzi nakuwa mpole huku akimdadisi kutaka kumjua.

“Alice embu tusogee mpaka pale tusimame vizuri maana hapa watu wanapita pita sana na tutashindwa kuongea vizuri.”

Wakasogea mpaka eneo la pembeni ya ukuta nakuendelea na maongezi.

“Alice mimi naitwa Jacqueline Gaspery na tulikuwa wote katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania pale Diamond Jubilee miaka ilee!!”

Alice akainama chini kisha akarudisha kichwa chake juu na kumuangalia kwa mara nyingine uku akazilazimisha kumbukumbu zake zifanye kazi. Akatoa tabasamu baada ya kukumbuka kidogo.

“Yap, si ulikuwa na wewe mshindi wa tatu sijui?”

“Ndio!!, ona sasa umeshakumbuka! Kwanza pole kwa yaliokukuta kipindi kile, embu niambie ilikuwaje mpaka ukapokonywa ule ushindi maana mashindano yalirudiwa na mimi ndiye nikawa mshindi wa mashindano yale.”

Alice akainamisha kichwa chini kwa huzuni. Uso wake ukajazwa na machozi yaliochanganyikana na maumivu makali. Mwili ukabaki ukiendelea kumsisimka kila mara.

“Jacky?”

Alice akainamisha kichwa chake juu kwa na huzuni. Machozi yakawa yameshafuata utelezo na kudondoka tone moja moja mpaka chini.

“Usilie Alice we niambie tu?”

Mwili wa Alice ukazidi kumsisimka. Machungu yote aliokumbushiwa na Jacky yakaharibu kabisa ubongo wake. Akaamini kuwa kile ndicho chanzo cha maisha yake kukosa uelekeo. Akamkumbuka sana baba yake wa kufikia, John alivyomfanyia unyama. Akiwa katika kumjibu mara mapolisi wale wa ki Nigeria wakatokea wakipita maeneo yale wakiwa na machela huku wakionesha dhahiri wamebeba maiti kutokea ghorofa ya juu. Akili ya Alice ikahama moja kwa moja mpaka katika ile machela iliyobebwa na mapolisi.

“Aloyce?”
 
94.

Alice akashindwa kuuzuia mdomo wake. Akajikuta akimtaja Aloyce kwa sauti ya juu baada ya kuiona ile machela japokuwa kulionesha kuna maiti iliyofunikwa ndani yake. Wale mapolisi wakasimama nakumuangalia Alice. Mmoja wapo wa polis akamsogelea Alice alipokuwa amesimama na Jacky mpaka karibu.
Jacquline Gaspery mrembo nambari moja kutoka Tanzania. Kitendo cha yeye kugombea urembo wa Arusha nakuibuka mshindi kukampa nguvu sana ya kuweza kuiwakilisha Arusha vyema katika mashindano ya miss Tanzania. Jacky akapata nafasi ya kushiriki mashindano ya miss Tanzania kwa mara ya kwanza. Akahudhuria kambi ya Girrafe Green View na akiwa kambini aliweza kumuona binti mmoja mweupe na aliyekuwa karibu sana na mwalimu wake kwa kuuliza maswali ya hapa na pale juu ya mbinu za kuwa mshindi. Maswali yale yalimpa sana moyo Jacky nakujiona anaweza kufika mbali zaidi kwani kilichotakiwa kujiamini zaidi. Siku ya kilele cha mashindano ya miss Tanzania pale Diamond Jubilee, Jacky alikuwa muoga sana. Mwili wake ulikuwa ukimtetemeka sana na hata yeye mwenyewe akakiri kuwa ni sababu mojawapo ya yeye kutokuwa mshindi wa usiku ule. Taarifa juu ya mwili wa mrembo mwenzao kukutwa hotelini akiwa amekufa ilimshtua sana Jacky na warembo wenzake wote. Japokuwa Jacky alishakubaliana na ushindi uliokuwa umeenda kwa Alice lakini alistahajabishwa kusikia kuwa Alice anahusika na maujaji ya rafiki yake huyo ambaye walikuwa wakiishi chumba kimoja kambini hivyo Alice akapokwa ushindi.

Jacky hakuvunjika moyo baada ya mashindano kuhairishwa. Wakarudishwa kambi nyingine nakuongezwa wiki mbili kwa ajili ya kumuombeleza mwenzao aliokutwa amekufa hotelini (Jamila Said). Taarifa ya kutoroshwa kwa Alice na mama yake iliwafikia warembo wote waliokuwa kambini kwa muda. Wakalaani kila mmoja nakuamini huenda kweli Alice anahusika na mauaji ya Jamila. Muda wa mashindano kwa mara ukawadia wakashiriki kwa mara ya pili na Jacky akawa mshindi nambari moja wa mashindano ya mrembo wa Tanzania. Akatunukiwa tuzo ya kofia sambamba na zawadi ya gari la kifahari na mikataba mbali mbali ya kufanya kazi za urembo. Kwa baahati mbaya Jacky hakuweza kufanya vizuri katika mashindano ya mrembo wa Dunia. Hakuweza kuambulia nafasi za juu zaidi ya kuwa wa mwisho mwisho kutokana na waafrika kutokupewa nafasi za juu.
 
95.

Akarudi Tanzania kwa unyonge japokuwa alikuwa na mikataba minono. Malengo yake ya kuipa sifa Tanzania katika mashindano ya dunia yakapotea. Akarudi kufanyia kazi ile mikataba minono aliyopewa awali. Baada ya mwaka akaanzisha mahusiano na Okoye kijana kutoka Nigeria kwa njia ya mtandao. Wakawa karibu sana kiasi cha Okoye kupanda ndege kuja Tanzania kwa ajili ya Jacky. Mapenzi yao yakadumu kwa muda mrefu mpaka kuamua kufunga harusi kubwa katika Jiji la Arusha na kuimalizia nchini Nigeria. Maisha kwao yakawa kama tamthiliya nzuri na yakuvutia hata kuigwa na baadhi ya watu. Jacky akayahamishia mapenzi ya kitanzania nchini Nigeria. Akashika ujauzito wa Okoye kwa mara mbili mfululizo na kumzalia watoto wakiume na wa kike. Makazi yakawa ni Nigeria na hata miradi yao mingi ikawa ipo Nigeria. Kazi ya upolisi aliokuwa akiifanya Okeye ilimuongezea sifa sana licha ya kupata kipato cha kawaida. Okoye alikuwa si mtu wa mashihara awapo kazini nchini mwao Nigeria. Nyadhifa ya juu ya kuongoza msafara wa aina yeyote katika matukio mbali mbali ni kati ya vitu ambavyo Okoye alivitendea haki katika kazi yake ya upolisi. Sasa Okoye alikuwa katika kuhakikisha hali ya usalama inakaa vizuri baada ya kuamliwa na mkuu wake brigedia Oliefi kuhakikisha anamchukuwa Aloyce na kumpeleka kwenda sehemu wanapoaga miili ya marehemu na pia kuhakikisha Aloyce anapanda ndege wanaongozana naye mpaka Rwanda kwa ajili ya maziko ya wazazi wake. Okoye akiwa ndani ya hoteli ya Darlington akimfuatilia Aloyce anamkuta Aloyce kapanda juu ya dari akifuatilia mwanamke aliyetambulika jina la Alice. Hakumjua Alice vizuri lakini mapolisi wenzake waliokuwepo hapo wakamueleza kwa kifupi kuwa Alice anahusika katika kifo cha Wazazi wote wa Aloyce. Okoye akavua kofia yake nakuchukua tochi. Akajitahidi kumtafuta Aloyce na huyo Alice bila mafanikio yeyote lakini tundu kubwa aliokutana nalo ndani ya dari likamfanya ashuke kupitia tundu hilo nakukutana uso kwa uso na Aloyce akiwa hatamaniki kwa damu zilizomuenea maeneo ya shingoni na miguuni mwake. Aloyce alikuwa ameshapoteza maisha Hasira kali zikamganda Okoye na kuhaidiana na nafsi yake atamfanya vibaya Alice kwani akili ilimtuma moja kwa moja atakuwa anahusika pia katika kumuua Aloyce. Akawaamuru maaskari aliokuwa nao wauchukue mwili wa Aloyce nakuuweka katika machela kisha wakaanza safari ya kutoka hoteli ya Darlington wakiwa wameongozana. Kitendo cha kufika maeneo ya mapokezi kwa chini kabisa, Okoye akastaajabu mwanamke akitoa sauti kwa nguvu akilitaja jina la Aloyce. Okoye akazuia ule msafara wa mapolisi wenzake wasiendelee na safari. Akabadili uelekeo na kumfuata yule mwanamke. Japokuwa pembeni yake kulikuwa na mke wake Jacky, lakini hakulijali hilo kwani alikuwa kikazi zaidi. Hasira zikaendelea kumkaa Okoye huku akiamini huyo mwanamke atakuwa anajua fika Aloyce ni nani. Okoye akatoa pingu zake kiunoni huku akikaribia lile aneo alipo yule Mwananamke amesimama.

“Mume wangu Okoye vipi?”

“Nakuonmba uniache mara moja niko kikazi zaidi”

Jacky akaingilia kati kumsemesha Okoye ambaye alionekana sura yake kuikunja kwa hasira. Lugha ya Kiswahili ambayo Jacky alikuwa akimgfundisha ilikuwa imemkaa kisawa sawa, hivyo hata wale askari wenzake hawakuweza kutambua maneno wanayoongea Okoye na mkewe.

“Mama Oliseh huyu nimemsikia akimtaja Aloyce? Right?”

“Hapana bwana maneno yametokea kwa huku upande wa pembeni yetu na sijui ni mwanamke gani karopoka ila kwa huyu unamuonea kwani namjua fika nilipotoka naye.”

Okoye akabaki kuwa mpole kwa ghafla. Akamuanimi sana mkewe kwani katika maisha yao Jacky hajawahi kumwambia uongo wowote. Akatazama upande wa pili bila kumuona huyo msichana mwingine anayeambiwa.

“Yupo wapi sasa mbona simuoni huyo mwanamke unayeniambia?”

“Okoye, elewa sauti haijatoka hapa mume wangu?”

Okoye akamuangalia Alice mara mbilimbili juu mpaka chini. Akaliangalia vizuri lile gauni la alice kwa jinsi lilivyotapakaa damu. Mbnu mbali mbali za kipolisi alizokuwa nazo Okoye zikamfanya aamini kabisa kuwa zile damu za kwenye lile gauni hazikuwa za muda mrefu. Akatamani alisogeze lile gauni mbele ya macho yake lakini hakuwa na jinsi kutokana na maneno ya mkewe kuwa siye aliyetamka jina la Aloyce.

“Mke wangu”

“Abee!”
 
96.

“Baaadaye wacha niendelee na majukumu, tuna msiba mzito umetukbili na mbaya zaidi unamuhusisha raisi wa Rwanda na mke wake. Tutaonana labda baadaye nyumbani ama kesho maana shughuli ni ndefu!” Okoye akamuaga Jackky kisha akazirudishia pingu zake kiunoni nakuondoka na wenzake huku wakiwa wamebeba machela iliopkiza maiti.

Muda wote huo Alice alikuwa akitetemeka. Hakuwa akijitambua n mbaya zaidi hakuamini kama amenusurika mikononi mwa Okoye kwa jinsi alivyokuja na akivyoondoka.

“Asante sana Jacky, wewe ni rafiki wa kweli naaamini”

“Usijali sana Alice!, embu nimbie ukweli Alice unaonekana hauko sawa kabisa, kwani huyo Aloyce sijui ulioropoka unamjua?”

“Ni hadithi ndefu kidogo Jacky lakini nitakusimulia tu hata baadaye, kwa sasa akili yangu haijakaa sawa”

Alice akiwa bado yupo na Jacky katika maongezi yao mara tena akatokea mwanamke mwingine.

“Alice? Alice wajua wafanya mie niwekwe kwa hatia?”

Alikuwa ni Achieng, yule rafiki wa muda wa Alice pindi alipoingia mule chumbani kwake nakuingia chooni kisha akapanda juu ya dari na kumuacha akiwa sebuleni.
.
“Achieng, my friend. Kwanza unatakiwa uanze kwa salamu mbona upo hivyo?”

“Ohh soryy maze, wajua nilikuwa katka panic ya juu, but siyo fresh vile wanifanyaga Alice?”

“Haya, Jacky huyu ni rafiki yangu wa humu humu hotelini nimemjua na ametokea Kenya anaitwa Achieng. Achieng?”

“Yes, Alice!”

“Huyu ni my best friend wa siku nyingi na ametokea Tanzania ninapoishi. Na alikuwa miss Tanzania kipindi cha nyuma.”

“Nashukuru kwa kumjua”

“Asante, Achieng. Lakini mimi kwa sasa sipo tena Tanzania naishi huku huku Nigeria”

Kitendo cha kutambulishana pale wakijuana kikamfanya hata Achieng asahau mada iliyomleta pale ya kumlaumu Alice kwa kitendo cha kumuacha chumbani ppeke yake nakumletea matatizo. Achieng akajikuta amesahau kabisa. Story zikawanogea kwa maneno mbali mbali haswa ya urembo kwani Achieng alipenda sana ajue masuala ya urembo kiundani. Muda wote huo akili ya Alice haikuwa imekaa sawa.

“Jamani Achieng na Jacky? Samahanini mara moja nakuja naelekea chumbani kwangu mara moja”

“Akili ya Alice moja kwa moja ikahama na sasa ikahamia ni jinsi gani atajinasua pale hotelini kwa kubadilisha zile nguo kwani zilikuwa zimetapakaa damu japokuwa zilikuwa zimemganda. Mawazo ya Alice moja kwa moja yakawepo katika chumba alichokuwa amepangisha Aloyce mwanzoni wakati wa harusi kwani aliacha nguo wakati anabadilisha kuvaa gauni aliokuwa amenunuliwa na Aloyce. Akaingia ndani ya lifti mpaka ghorofa ya pili, kile chumba kilikuwa katika akili yake lakini alipofika mbele ya mlango wa kile chumba kikawa kimefungwa.

“Shiit, my God!” (Mungu wangu!)

Akajikuta nguvu za mwili kumlegea na akili kumchoka ghafla baada ya kukuta mlango umefungwa. Halamshauri ya kichwa chake ikapambanua kwa haraka zaidi ikamuamuru ashuke chini mpaka alipowaacha Jacky na Achieng. Akafanya hivyo.

“Achieng? Ujue nimesahau mkoba wako chumbani kwako si unakumbuka niliingia nao kwako?”
 
97.

“Yeah, nakumbuka upo tena nimeuweka pale juu ya kitanda changu kwani mapolisi walitaka kuuchukuwa ila nikawadanganya niwangu hata hawakuusachi wakanipa nami nikauwekaga pale kwa kitanda.”

Moyo wa Alice ukawa na furaha, furaha ya kuambiwa mkoba wake upo na wala haujasachiwa kitu chochote. Akachukuwa kadi ya kufungulia mlango kutoka kwa Achieng kisha akatumia tena lifti mpaka chumba alichokuwa akiishi Achieng. Akaingia kwa pupa nakujifungia kisha breki ya kwanza ikawa moja kwa moja mpaka katika kitanda cha Achieng. Macho yake yakawa sawa kwa kutazama ule mkoba wake. Akausogelea kwa karibu nakuanza kufungua zipu.

“Asante sana Mungu!”

Hakuamini kwa alichokikuta. Haukuwa umefunguliwa kabisa, akakuta burungutu la pesa ambazo alizichukuwa katika brifkesi ya Aloyce kipindi kile. Ule mkufu aliokuwa amenununuliwa akauchukuwa na kuuvaa shingoni mwake. Akachukuwa nguo ya kubadilisha. Kitendo cha kuvua lile gauni na kutaka kubadilisha tu akashangaa hodi ikipigwa katika chumba chake. Mawazo na akili yake moja kwa moja yakahamia huenda ni Achieng na Jacky wameamua kumfuata. Akaitikia kwa sauti ya juu huku akimalizia kubadilisha ile nguo. Akajiweka safi kwenda kufungua. Alipoukaribia mlango nafsi yake ikabishana naye. Moyo ukagoma kufungua ila akili ikamalazimisha kufungua, Macho yake hayakuweza kukabilliana na akili yake. Akajikuta akiinamisha mgongo nakuchungulia kupitia kile kitobo cha mlango. Akajikuta mwili wake kukosa ushirikiano. Miguu ikaanza kumtetemeka.

“Si Okoye huyu mume wa Jacky?”

Akausemea moyo huku akiligeuza jicho lake katika kamera ya ulinzi iliokuwa imehifadhiwa kenye kona ya chumba. Akili ikamrudisha Alivyofanya mwanzo kutoroka, ile akili ya kukimbilia chooni nakuingia katika dari. Akaanza safari ya kuingia chooni lakini kabla hajafika chooni akashangaa mlango ukigongwa huku sauti ya milio wa king’ora cha dharula ukiita mithili ya nyumba inapoungua. Mapigo ya moyo ya Alice yakazidi kuchukizwa na ule mlio wa king’ora cha dharula ndani ya ile hoteli. Ushupavu ukamuingia ndani ya akili yake upya. Nguvu za ajabu zikazidi kumjaa ndani ya choo. Akaliangalia paa vizuri nakupanda kwa kutumia sinki la chooni kama alivyofanya hapo awali. Ndani ya muda mchache Alice akawa tayari ndani ya dari huku akiwa na mkoba wake akiushikilia kwa kutumia shingo yake. Hakulijali giza totoro la mule ndani ya dari, akaendelea na safari ya kujikongoja huku akifuata ile njia ya mwanzo aliokuwa ameipita humo juu ya dari huku sauti za mlango kwa mbali zikiashiria kuendelea kuvunjwa.

“Asante mwenyezi Mungu!”

Furaha ya Alice ikaanza kuonekana baada ya kutumia mwendo mrefu akijikongoja ndani ya dari. Sasa akawa ameona upenyo, upenyo wa kutokea kwenye kadirisha kadogo sana cha kioo kalichofunguliwa uwazi kidogo kwa ajili ya kupitisha hewa. Kadirisha ambacho kalikuwa kamepakana na eneo la stoo ya kuhifadhia vyakua vya hotelini. Alice akapitia hako kadirisha nakujirusha mpaka nje. Hapakuwa na urefu sana hivyo aliweza kuinuka nakuendelea na safari nje ya hoteli ya Darlington. Kwa kutumia wigo wa magari yaliokuwa yamepaki hapo hotelini, Alice akajikuta akiweza kujificha ficha mpaka kufikia barabara kuu ambayo hata hakuielewa inalekea wapi na inatokea wapi.

*********
 
98.

Jacky na Achieng hawakuwa wakijuana sana ila kwakuwa tangu zamani Jacky alikuwa mtu wa watu na kitendo cha yeye kupenda sana masuala ya urembo kikamfanya Achieng avutiwe naye. Jacky akamsimulia mbinu mbali mbali Achieng zilizomfanya mpaka kufikia kuwa miss Tanzania na pia akamuhadithia mikataba minono aliopewa ya kufanya kazi katika nchi mbali mbali kupitia urembo. Achieng akapenda sana. Umri wake wa miaka ishirini na mbili ukamshawishi na yeye akirudi nchini kwao Kenya aweze kushiriki mashindano ya miss Kenya. Akatamani sana aendelee kubaki na Jacky katika maongezi hata kwa siku nzima. Ni Alice ndiye aliokuwa anamchelewesha Jacky kuondoka kutokana na Alice kuaga kuwa anaenda ndani kubadilisha nguo mara moja na kurudi. Kitendo cha Alice kurudi na kuchukuwa kadi ya Achieng na kwenda kwa ajili ya kuchukuwa mkoba wake kikamuongezea muda zaidi Jacky wakuendelea kupiga story na Achieng wakimsubiri Alice. Wakanogewa sana na michapo ya urembo waliokuwa wakipeana na kitu kilichokuja kuwakatisha ni ujio wa mme wa Jacky, Okoye kwa mara ya pili.

“Jacky, yule mwanamke uliokuwa umekaa naye yupo wapi?”

“yule rafiki yangu?” “Hapana hawezi kuwa rafiki yako yule ni muuaji haswa. Na ndiye anahusika kwa kifo cha Aloyce na wazazi wake ambaye ndio rais wan chi ya Rwanda.”

“Jesus!”

Jacky akaonekana kustaajabu lakini kwa upande wa Achieng hakuwa na wasiwasi kutokana na hapo awali kuwekwa hatiani kwa kudhaniwa huenda anajuana na Alice lakini baada ya kuonekana Alice hajuani naye kupitia kamera zao za ulinzi ikabidi Achieng aachiwe huru.

“Yupo kaelekea chumbani mara moja kubadilisha nguo”

“Chumba kipi?”

Jacky, Achieng na Okoye wakiwa na mapolisi zaidi ya kumi wakaongozana mpaka katika chumba cha Achieng ambapo ndipo Alice alikwenda kubadilisha nguo muda si mrefu. Okoye hakutaka kabisa kubisha hodi.

“kadi ya kufungulia ipo wapi?”

Okoye akauliza kwa sauti ya juu huku akiwa bado katika hasira kali.

“Kadi aliichukuwa mwenyewe akasema anakuja kubadilisha nguo mara moja kwani chumbani kwake kumefungwa na haoni kadi yake.”

Ikabidi Achieng aongope kwani alijua dhairi endapo atasema Alice ameenda kuchukuwa mkoba wake chumbani kwake na yeye atakuwa hatiani kwa mara ya pili hivyo atakuwa pabaya. Okoye kwa hasira huku akisaidiana na mapolisi wenzake wakaamuru kiwashwe king’ora cha dharula katika hiyo hoteli na kila mmoja awepo eneo la mapokezi asiweze kuelekea popote. Wakaanza zoezi la kuuvunja mlango ule wa chumbani kwa Achieng. Dakika mbili nzima zikawatosha kuubomoa ule mlango uliokuwa umetengenezwa kwa matilio ya chuma kwa mbali. Wakaingia ndani ya chumba cha Achieng huku kila mmoja wa maaskari akiwahi uvunguni na maeneo yaliokuwa yamejificha. Wakatafuta bila kuambulia chochote wakaingia na upande wa chooni kisha Okoye akangaliana na maaskari wenzake.

“As well as he has done it again.” (Amefanya vile vile tena!)

Wakajikuta wakiishiwa nguvu baada ya kugundua huenda Alice ametumia mbinu zile zile za kujficha eneo la juu ya dari kwa mara ya pili. Tochi kubwa takribani ya sita zikaagizwa. Tochi zenye mwanga mkali sana ambazo hutumika hata kumulikia wanyama pori msituni. Okoye akisaidiana na mapolisi wenzake wakaingia juu ya dari na kuwaacha Achieng na Jacky wakiendelea kuduwaa kwa kuwaangalia na kutokujua itakuwaje Alice akishikwa. Taa zikaendeleea kuangaza eneo lote la juu ya dari ya hoteli ya Darlington bila majibu yeyote. Wakazidi kusonga mbele hapa na pale kupitia juu ya dari bila kuambilia chochote. Wakapeana masharti ya kiaskari kuwa wabaki maaskari wanne na zile tochi kwa muda wa masaa mawili hadi matatu huenda Alice akajitokeza.

*******

OLISEH, mgahawa mkubwa na wa kifahari katika Jiji la Lagos, Nigeria. Mgahawa ambao unapenda kutumiwa na watu mashuhuri mara kwa mara kwa kupata vinywaji na chakula hata wakati mwingine kuigizia katika filamu zao mbali mbali. Mandhari ya mgahawa wa LISEH nikivutio tosha kwa kila mpita njia kutokana na kuwa barabarani sana na pia wahudumu waliojaa kwa kujua kazi zao. Mgahawa ambao haubagui mtu zaidi ya kuingiza chochote na kila inapofika ijumaa, mgahawa wa OLISEH huwa na ofa ya kuwapa huduma wale wasiojiweza kiuchumi na hata walemavu na hii ni kutokana na mmiliki wa mgahawa OLISEH OGBI kupitia maisha magumu mpaka kufanikiwa kuufungua mgahawa wa OLISEH. Njaa kali ilikuwa bado imemtawala Alice. Ule uvumilivu wa kukaa bila kupata chochote toka jana yake usiku sasa ukawa umemshinda. Akahisi kama kuwa na vidonda vya tumbo kwa jinsi tumbo lillivyokuwa likimsumbua kwa kuunguruma na kumkwangua. Mwendo mrefu aliokuwa ametembea kutokea hoteli ya Darlington alipotoroka ukawa umemchosha zaidi. Mwili wake ukagoma kuendelea na safari huku macho yake yakimlazimisha kuonana uso kwa uso na mgahawa wa OLISEH. Akili ikakubaliana na yeye hivyo akajikuta miguu ikimsogeza hatua kwa hatua mpaka katika mgahawa wa OLISEH.
.
“Welcome sister!”

Mhudumu wa mgahawa akampokea Alice kwa haraka. Alice hakukjijali kwa mavazi aliokuwa nayo kuonekana na uchafu sana kwa vumbi jeusi la alilolitoa kwenye dari zaidi ya akili yake yote kuhamia katika tumbo lake jinsi ya kupata chakula.

“Get me food” (Nipatie chakula)

Alice akamhoji yule mhudumu. Akaoneshewa ishara ya kuingia ndani. Akastaajabu sana kwa aliyoyakuta. Watu mbali mbali wasiojiweza walioonesha kufanana naye kwa mavazi machafu wakipata chakula huku wahudumu wakiwa karibu yao kuwasilkiliza. Akapiga moyo konde nakutafuta sehemu ya kuketi tayari kwa kuagiza chakula. Yule hudumu aliokuwa amempokea hakuwa mbali na Alice.

“What kind of food do you want” (Unahitaji chakula gani dada?)

Alice akiwa katika kujiuma uma kwa kuagizia chakula mara akahisi tumbo lake kumvuruga zaidi hali iliyochochea kichefu chefu cha haraka,. Akajihisi mimba iliokuwa tumboni mwake ikitaka kumtoka.

“Where is toilet?” (Chooni wapi?)

Haraka haraka Alice akaoneshwa chooni na kukimbia. Breki ya kwanza akatizamana na sinki kubwa la kunawia mikono ndani ya bafu. Mdomo wake ukaw a umeshindwa nguvu ya kulizuia tumbo lake hivyo kumfanya Alice atapike manjano. Akatapika sana, nyongo si nyongo. Tumbo likamuuma sana lakini akili yake moja kwa moja ikapambanua nakuona huenda mimba ya Aloyce alionayo inamletea matatizo. Akaona kule kutapika kumemuisha, akanawa vizuri sambamba nakuchukuwa maji kidogo huku akijisafisha nguo yake iliokuwa imejaa vumbi na kuleta uhafadhali kidogo na punde alivyomaliza akarudi alipokuwa ameketi akimsubiria yule mhudumu wa mwanzo aje tena kumhudumia. Akiwa katika hali ya kusubiri mara jicho lake likatazamana na taarifa ya habari katika televisheni iliokuwa mbele yake. Mwili wa rais wa Rwanda, Kagwa Kwisereka na mtoto wake Aloyce ndizo zilikuwa zikioneshwa mara mbili mbili huku mapolisi wakionekana kuwa karibu katika kuaga.

“Ina maana bado hawajawasafirisha?”
 
99.

Alice akajikuta akishika kifua chake kwa mshangao akiongea mwenyewe. Akiwa bado katika taharuki mara tena ikatokea picha yake kubwa ikimuonesha akiwa kanisani na Aloyce na vipande vya picha nyingine vingine vikimuonesha akiwa na kipaza sauti katika ukumbi wa Darlington.

“Jesus!”

Akastaajabu kwa mshangao mkubwa huku akindelea kuushika mkono wake katika kifua. Akajihisi mkojo unataka kumtoka, mikono yake ikaanza kukosa ushirikiano, akili ikazidi kumchemka.

“Hapa hakuna usalama, hapanifai hapa Alice mimi!”

Alice akajisemea kimoyo moyo huku akianza safari ya kutoka katika mgahawa wa OLISEH. Hatua mbili tatu zikamfanya aweze kutoka eneo la nje kabisa. Akili yake ikawa bado haiko sawa. Akiwa katika hali ya kutoka tena kinyume nyume huku akiangalia sehemu alipotoka ndani ya mgahawa mara ghafla mgongo wake ukagota katika gari iliokuwa imepaki pembeni, gari la polisi.

*******

Achieng na Jacky wakiwa bado ndani ya hotel ya Darlington katika chumba cha Achieng wakimsubiri Okoye ambaye ni mume wa Jacky atoke juu ya dari ambapo alipanda kwa madhumuni ya kumtafuta Alice. Kipupwe katika hoteli yote haswa maeneo ya vyumba vya wageni kilikuwa kimezimwa ili kupisha mapolisi waliokuwa wamepanda juu ya dari. Dakika thelathini nzima zikawa zimeshawachosha Achieng na Jacky kusubiri kama Alice atakamatwa huko juu ya dari. Achieng akawa mtu wa kwanza kuchoka kwa joto kali lililoanza kupenyeza katika miili yao baada ya kiyoyozi kuzimwa hotelini.

“Jacky, wajua mie mwenzako nasikia hot, yaani kuna mijoto balaa embu tukwende out!”

Wakatoka nje nakuacha mapolisi baadhi wakiwa chini na wengine wakiwa bado juu ya dari. Mapolisi bado walikuwa katika doria kali kila pembe ya hoteli ya Darlington. Achieng akiwa bado yupo nje na Jacky wakashangaa kumuona Okoye akiwafuata huku nguo zake hazitamaniki kwa uchafu alioutoa juu ya dari. Pembeni akiwa akashikiilia tochi ambayo hata bado haikuwa imezimwa japo kulikuwa ni mchana.

“Jacky mke wangu? Alice kapatikana, tumepigiwa simu sasa hivi na mhudumu wa mgahawa wa Oliseh na tumeambiwa kuwa yupo kwenye mgahawa wa Oliseh”

Jacky akabaki akiangaliana na Achieng . Wakabaki wote na bumbuwazi wasielewe Alice amefikaje fikaje nje. Wakapandishwa ndani ya gari la polisi la kazini kwa Okoye nakuanza kuelekea katika mgahawa wa Oliseh. Wakafika, kitendo cha kupaki gari lao nje hata kabla hawajashuka macho yao wote watatu yakakutana na mwanamke akirudi kinyume nyume akikaribia maeneo ya gari lao. Wakataka kupiga honi lakini haikusaidia zaidi ya kumuacha afike karibu. Kwa nguo zake zilivyokuwa uchafu sana moja kwa moja wakajua huenda ni kichaa. Okoye akashuka na kumfuata kwa hasira kumgombeza, kitendo cha kumfikia karibu yule mwanamke akageuza mwili wao nakuwatazama.

“Aliceeee???”

Wote kwa pamoja Achieng na Jacky wakajikuta wakitoa sauti kwa juu hali iliofanya mwili wa Okoye kujawa na furaha, nywele zake kusisimka baada ya kujihisi sasa alichokuwa anakitafuta amekifanikisha. Akachomoa pingu zake kiunoni mwake nakumfunga Alice kisha akamvuta kwa nguvu mpaka ndani ya gari. Alice akajitahidi kugoma lakini kwa nguvu za Okoye akajikuta akisalimu amri nakuingia ndani ya gari.

******

Okoye hakufanikiwa kabisa kusafirisha mwili wa wa rais wa Rwanda Kagwa Kwisereka pamoja na mtoto wake na mkewe kutokana na kubaki na mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya vifo hivyo. Amri kutoka kwa brigedia Oliefi ya kumtaka Okoye ahakikishe anakuwa na mtuhumiwa karibu mpaka baada ya mazishi kutokana na usalama wake endapo atafikishwa nchini Rwanda wananchi wangesababisha dhahama kubwa sana kwake. Alice akawa chini ya ulinzi katika mahabusu ya muda ya ‘Supreme’ nchini Nigeria. Si Jacky wala Achieng aliyekuwa na ubavu wa kumtetea Alice kutokana na mauaji aliofanya. Wakamtenga na kumuogopa sana Alice. Wakamfananisha Alice na Jasusi la dunia, Carlos. Wakawa wamejivua gamba rasmi kwa kutokutaka kumuona kabisa Alice. Wakawa wameafiki kabisa kitendo ch Okoye kumuweka Alice mahabusu. Wakatamani sana hata afe tu kuliko unyama alioufanya wakuwaua watu pasipo na hatia na tena kiongozi wa nchi.
 
100.




Alice akawa hajitambui nini hatma yake zaidi ya kuwekwa mahabusu na wafungwa wengine wakike. Ule ujauzito aliokuwa nao ukawa unamuumiza kila kukicha kwa maumivu makali. Kichefu chefu hakikuacha zaidi ya kuendelea kumtesa hata kama hakula lazima atapike nyongo.

“Ipo siku ukweli wangu utajulikana”

Alice akaendelea kujipa moyo huku akiongea peke yake. Mavazi maalumu ya wafungwa wa gereza la Ochie yakaupendezesha mwili wa Alice kutokana na nguo alizokuwa nazo kuwa chafu sana na zenye kunuka vumbi la juu ya dari alipokuwa amepanda kipindei kile. Alice akawa nusu mfungwa, mfungwa asiyejua nini hatma yake. Mfungwa mwenye ujauzito asijue atalea vipi.

Baada ya mazishi ya rais wa Rwanda Kagwa Kwisereka na mkewe na mtoto wake kufanyika katika Jiji la Butare nchini Rwanda huku mazishi yakiudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbali mbali za dunia. Nchi yote ya Rwanda ikapokea msiba kwa masikitiko sana. Upendo wa dhati ambao ulifanywa na rais wa Rwanda Kagwa enzi za uhai wake ukalipua vilio kwa baadhi ya kinamama na hata kinababa wakashindwa kabisa kujizuia. Kila mwananchi wa Rwanda akaonekana kuchukia sana kitendo kilichofanywa kwa raisi wao na familia yake huku baadhi ya wananchi wakihitaji wamuone mtuhumiwa mara moja na baadhi yao wakipendekeza achinjwe kabisa. Wakaichukia sana nchi ya Tanzania kutokana na kusikia kuwa mtuhumiwa ni mwanamke na anatokea nchini Tanzania. Msiba ukamalizika salama japo wengi wakabaki na vinyongo mioyoni mwao. Eneo maalumu lililoandaliwa kwa maziko ya miili hiyo likawa limeshakamilika. Mkuu wa kikosi cha usalama nchini Nigeria akaombwa amuwasilishe mtuhumiwa wa mauaji mara moja kwa siku ya kesho yake.

*****

Umati wa wananchi wa nchi ya Rwanda walikuwa na shauku kubwa ya kumjua mwanamke aliyetuhumiwa kufanya mauaji ya rais wao wa Rwanda, Kagwa Kwisereka. Ikawabidi mapolisi wa kipelelezi kufanya njia za ziada kubadili njia za kumshusha mtuhumiwa kutokana na kufurika sana kwa idadi ya wananchi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali. Okoye akisaidiana na Mapolisi wenzake wakamficha Alice katika boksi kubwa la kubebea mizigo kisha wakachanganya na mizigo mingine ili wananchi wasielewe kitu. Wakatoka katika uwanja wa ndege pasipo wananchi kujua kama kuna mtu kafichwa. Wananchi wakavumilia sana siku nzima mpaka asubuhi huku wakikimbilia kila ndege ilikokuwa ikishuka. Baadhi yao wakaonesha kukata tamaa lakini kwa wengine wakatandika nguo zao chini na kukaa hata kulala kwa kusubiri kumuona mtuhumiwa.

“Wewe iko ua si ndio?”

Alihoji Kamanda mkuu wa nchini Rwanda baada ya Alice kufikishwa katika ofsi yao mkuu.

“Hapana sijaua mimi?”

Alice kabla hajaachama mdomo wakekujitetea akashangaa anapigwa makofi na Okoye huku yule askari aliokuwa akimhoji akimpiga tumboni. Maumivu makali akayasikia Alice. Akajihisi kama anatoa damu nzito katika eneo la sehemu zake za siri, ile mimba aliokuwa nayo akajihisi kama inataka kumtoka.

“Peleka mara moja kule”

Yule mkuu wa mapolisi akaamuru mara moja. Wakamvalisha kitambaa kikubwa usoni mwa Alice, wakamchukuwa nakumpakiza katika gari tayari kwa kuondoka naye asipopajua.

“Ehh mwenyezi Mungu niokoe, niokoea katika mateso haya, sina hatia baba wa mbinguni. Niokoe Baba”

Alice akajikuta akisali kimoyomoyo huku macho yake yakiwa hayana uwezo wa kuangaza kutokana na kuzibwa kitambaa kikubwa cheusi usoni mwake. Hakujua anapopelewa.

Ikawawchukuwa nusu saa kwa mapolisi kufika katika gereza la nchini Rwanda. Wakamshusha Alice na kumpeleka moja kwa moja mpaka katika eneo maalumu linalotumika kunyonga watu wanye hatia ya kuua. Wakamvua kitambaa Alice, macho yake yakatazamana na kamba kubwa nene huku chini kukionesha kuwa na urefu.

“Baba Mungu, hivi ni kweli unaniacha mimi mja wako nipotee?. Okoa maisha yangu Baba kwa mara ya mwisho. Yote haya ni baba yangu mzazi, nimeshakusamehe huko ulipo na mwanao natangulia mbele za haki. Aloyce nakupenda na nakufuata huko uliko niandalie makao mume wangu.”

Alice akamaliza kusali sala yake kwa sauti ya juu. Mapolisi wakamzunguka kuashilia wamemuweka kamba vizuri katika shingo yake, wakaikaza kidogo kisha wakamrusha. Alice akabaki amening’inia huku akitapatapa kwa maumivu ya ile kamba shingoni mwake. Haikuchukuwa muda Alice akawa ameshaaga dunia.

MWISHO

toa maoni yako




BURE SERIES
 
Back
Top Bottom