Mrema awaponda CHADEMA live Bungeni

Mrema awaponda CHADEMA live Bungeni

Lakini na ninyi watu wa Vunjo.........si bora hata mngemchagua yule Meela wa "gamba party" tujue moja!!
 
Hana jipya siunaona anasema nayeye anastahili kulipwa posho yake kwakuwa alikuwa Naibu waziri? Alikuwa anatafuta huruma ya ccm ili imlipe, ila kiukweli Mrema nimganga njaa
Huyu jamaa ana mtindio wa ubongo,kwani cheo cha unaibu waziri mkuu kipo kwenye katiba??
 
Mwacheni mzee wa watu arudishe fadhila kwa magamba party za kumpeleka india kwa matibabu.
 
Huyu jamaa ana mtindio wa ubongo,kwani cheo cha unaibu waziri mkuu kipo kwenye katiba??
Anadai Cheo chochote kinachokuwa created na Rais basi kinatambulika kisheria na yeye alipewa cheo hicho na Baba wa Taifa JK Nyerere kwa hiyo anapaswa kulipwa.
 
Mrema ndie mgombea pekee wa upinzani aliyepata asilimia 28% ya kura zote ambayo haijawai kufikiwa na mgombea yeynte wa Upinzani sasa anawashangaa wanaoendesha maandamano kumpinga Rais wakati yeye ndo alipaswa kufanya hivyo. Anasahau ya kuwa kura zake zilikuwa 1.8m wakat Dr. Slaa ni 2m na ushee. Hajui kutofautisha alama za nyakati 1995 chama cha upinzani kilichokuwa na watu wengi ni chake, 2010 kila chama kina wafuasi wengi CUF, CDM, TLP, NCCR, UDP, UPDP etc. Anazeeka vibaya huyu mzee.
 
Unajua wagogo wanasema "mbwa aliyekonda umwaibisha mwenye mbwa!!" Mrema anawaabisha wapiga kura wa Vunjo! Nadhani watu wa Vunjo wanastahili mbunge mwenye hadhi kuliko huyu Mrema ambaye ni bidhaa iliyokwisha muda wake kuuzwa. Inabidi kutupwa kwenye jalala.
 
Unajua wagogo wanasema "mbwa aliyekonda umwaibisha mwenye mbwa!!" Mrema anawaabisha wapiga kura wa Vunjo! Nadhani watu wa Vunjo wanastahili mbunge mwenye hadhi kuliko huyu Mrema ambaye ni bidhaa iliyokwisha muda wake kuuzwa. Inabidi kutupwa kwenye jalala.
A Political Man is a like Medicine Come Up wit an Expire Date.
 
Mrema ni mtu wa kuhurumia bure, yule mzee pumzi imepungua sana na nguvu zimemwishia. Hana tofauti na Esau wa kwenye biblia alieuza uzaliwa wake wa kwanza kwa chakula cha dengu. Kila chama alichojiunga nacho kilijifia na hii tlp aliyonayo ni marehemu zamani na Mrema ameamua kushuka nayo shimoni. Ushauri wangu kwa wana tlp, imarisheni chama sasa kwa kumu-ignore Mrema. Mwachani agange njaa yake ninyi wekeni mkakati kivyenu, maana mkichelewa zaidi jamaa ataondoka nacho kurudi kwa baba mbinguni.
.
 
Licha ya kunywa kikombe kwa mzee mwasapile lakn fikra za mrema bado finyu2! Wadau huyu mzee ndo bac tena hana jipya.
 
Mrema si ana haki ya kusema?Chagga Mafioso development.......
 
mrema wakati anatoka ccm c alikuwa anaanzisha maandamano na anaingia mitini sasa leo yakiwa kwa wenzake ndo anaona si sahihi????
 
huyo mzee akili zake zinamtosha mwenyewe kwani TLP wanataka kumtimua kwa sababu gani km siyo uchizi wake naona kisukari alichonacho kinamletea uwehu
 
Huyu ndio alikuwa Mrema bana

mremahabari.jpg
 
Huyo anaishi kwa siasa za uongo, damu yake ni rangi ya kijani, hayo matukio yanayotokea ni mwamko wa kisiasa ulimwenguni . Kwamba sasa
hivi watu hawadanganyiki tena. Je ? atasema nini hayo yaliyoanza kutokea leo Senegal. kwa hiyo yeye asubiri muda si mrefu ataenda
kulima ndizi atengeneze mbege.
 
mhe Mrema yuko live bungeni anaponda maandamano
Mrema is a full psychiatric case. Either uwe mpinzani au chama tawala issue ni what do you stand for.. Mrema ni worse hajui kanisa anasimamia nini. Na kwa bunge letu kama huna hoja au anything of substance unachoweza kufanya ni kuponda upinzani na kusifia bajeti kuwa ni nzuri...na kumsifia aliyeleta hoja... imagine waziri analeta hoja kwa maana ya kufanyiwa improvement mibunge useless wanasimama na kusema ni nzuri sana...
 
Sijui wale jamaa kule walimchagua kwaa lipi .Wacha waone moto baada ya kumpa kula za badala ya kura mchovu huyu .
 
Back
Top Bottom