Mrejesho wa mwezi mmoja baada ya kuacha kazi

Kuacha kazi ili ujiajili unahitaji uwe na akili maalumu, watu wana Mahindi yanaozea ndani hayana soko, nimeshuhudia Songea mwaka Jana mamia ya heka za mbaazi Wakulima wamegoma kuvuna, sababu gharama za kuvuna ni kubwa kuliko bei ya mbaazi.

Kuna Dada yangu aliacha kazi eti anaenda kulima matikiti, kilio alichonacho sasa....

Tuwe tunafuatilia siasa kidogo, wengine alipoingia tu Mtukufu kwa kauli zake za mwanzo tuliona ana mtazamo mbaya na secta binafsi, na ndio kinachotokea.
 
Hongera sana kwa ujasiri na hatua uliyochukua. Kuna baadhi ya kazi za kuajiriwa ni kama utumwa flani hivi huku return yake ikiwa ndogo. Wengine hawana ujasiri wa kujitoa kwa kuwa hawana uhakika wa kusurvive bila kale kazawadi kanakotolewa kila mwisho wa mwezi japokuwa hakakidhi haja
 
Safi, ukimaliza mwaka mmoja pia usisahau kutupa mrejesho wa maendeleo yako.
 
ZUKINI NI NINI WANA JF?
 
nalilima Tz ni Lushoto ila nimejaribu kwanza robo heka likikubalindo ntakua nalima hili tu coz linakomaa kwa siku 50 unavuna mara4/5 halina comptition sokoni! wadudu hawaliathiri sana
 
nalilima Tz ni Lushoto ila nimejaribu kwanza robo heka likikubalindo ntakua nalima hili tu coz linakomaa kwa siku 50 unavuna mara4/5 halina comptition sokoni! wadudu hawaliathiri sana
Soko lake lipoje na utauzia wapi
 
kisutu nna namba ya dalali wa hilo zukini Ila nasikia Zenj ndo wana nunua bei nzuri hadi 2500 /kg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…