Heisenberg
JF-Expert Member
- Apr 26, 2017
- 1,688
- 2,982
Habari za leo wakuu, Poleni na majukumu pia hongereni kwa kusheherekea vyema Sikukuu ya EID, japo kwangu haikuwa njema sana kutokana na shida nilizopitia.
Juzi nilikuja na Uzi nikiomba msaada nifanye nini juu ya majanga yaliyonikuta
Rejea:-
www.jamiiforums.com
Leo nimeona Nilete mrejesho wa nini kimefanyika juu ya hili tukio.
Kikao cha Familia ya binti kimekaa leo Saa 4 asubuhi juu ya shauri la jamaa kudai mahari yake.
Watu wenye busara wamekaa na kuongea na kijana kuwa arudishe Moyo na waendelee na Process zao za uchumba kuelekea Ndoa.
Lakini kijana Amekuwa na Roho ngumu ssna kiasi cha kuto kusamehe. Hii ni kwasababu ameniona mara nyingi kwenye simu ya Mchumba wake na amesha muonya mara nyingi lakini binti amekuwa kiziwi, hivyo basi jamaa hawezi kuendelea na huo uchumba hivyo arudishiwe Mahari yake ajue nini cha kufanya.
Pia akaomba kama familia haina uwezo kwa wakati huo watoe chochote Tu hata elfu 10, ili mradi mahari imerudishwa.
Icho kikao mara kikageuga msiba watu karibia wote wakawa wanalia kwa kinachoenda kutokea.
Binti akaitwa kwenye kikao. Nae akawa analia. Akaulizwa kama anampenda jamaa, akasema anampenda sana kwani jamaa hakumpa muda wa kumsikiliza laa sivyo wangeyamaliza. Pia binti akaomba msamaha kwa kuiingiza familia kwenye matatizo.
Jamaa amepigiwa Magoti na mama yake na mama wa binti, ndio amekubali kuendelea na uchumba.
Mida ya saa 8 nimepigiwa simu na Deligation ya kikao nimepewa Onyo kubwa sana juu ya mahusiano yangu na binti. Nimekili sitarudiana naye tena na nimekata mawasiliano naye..
Nikaomba pia niongee na jamaa, nikaongea nae nimemuomba msamaha yeye kama mwanaume mwenzangu. Na jamaa amenisamehe kwa moyo mkunjufu kabisa.
Leo ndio nimeamini kuwa nimeachachana na huyu binti. Roho imeniuma sana maana yeye ndio mwanamke wa Ndoto yangu
Najiona kama nimeanza upya maisha bila huyu binti. Japo sikuwa na nafasi nae sana lakini nilikuwa nina amani.
Napenda kuwashukuru Nyote kwa michango yenu hadi kufikia kulimaliza Suala hili.
Juzi nilikuja na Uzi nikiomba msaada nifanye nini juu ya majanga yaliyonikuta
Rejea:-
Nimevunja uchumba wa watu
Habari za eid Kuna binti niponae kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa toka mwaka huu uanze. Nimekuwa nikimpenda sana kiasi cha kujitoa sana kifedha na ki hali kwa muda wote huu. Lakini binti amekuwa akinisisitiza kuwa yeye ni mchumba wa jamaa fulani na wanasubiri ndoa tuu. Hiyo hali...