Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,220
- 10,730
Kanisa la Free Church chini ya Mchungaji Masanja Mkandamizaji limeandika historia mpya ya kipekee baada ya kushuhudia uchumba ulioacha wengi midomo wazi na wengine wakibaki na mshangao.
Kauli mbiu iliyosikika ikitamba ilikuwa: “Mungu asiyewahi kuchelewa yupo!” — ishara kuwa hakuna linaloshindikana mbele za Mungu.
Hapo madhabahuni palishuhudia tukio ambalo si la kawaida: mwanaume mwenye umri ulioenda kwa mbali akamvisha pete binti, tofauti ya umri ikikisiwa kuwa si chini ya miaka 20. Wapo waliobaki wakisema umri ni namba tu, na kweli upendo uliojaa moyo na furaha ulimwagika kama mvua ya baraka.
Lakini kama ilivyo ada ya Watanzania, minong’ono haikukosekana. Huko mitandaoni wapo waliobaki wakicheka chini kwa chini; wengine wakihisi labda mzee kapata dogo dogo badala ya mwenza wa rika lake, wengine wakihisi huenda binti anaenda kuvuna mafao ya pensheni kwa tabasamu. Lakini katikati ya minong’ono na utani, ukweli ulio wazi ni mmoja tu: mapenzi hayana macho wala hofu.
Huyo jamaa ni mnafiki sana, ingawa sijajua anacheka kwa sababu ipi? Ila inaonekana kanisani hapo palikuwa moto sana kwenye uchumba huo. Mzee katumia ujana wake kuzisaka na sasa anakwenda kutulizwa na dogo dogo kwenye familia.