Mrejesho: Nimevunja uchumba wa watu

Mrejesho: Nimevunja uchumba wa watu

Na huyu huyu jamaa anaweza akarudi muda wowote akala,

au itapita miaka miwili hivi, kimnya, wakikutana anapiga

jamaa kakosea kinoma, ishu ikifika levo hiyo,ni kuondoka tu, ratio ya wanawake kwa wanaume ni 3/1 halafu bado unang'ang'ania kukaa na mtu ambae kwanza ulishamkataza juu ya huyo mtu na ameendelea kuwa nae? Afu ukoo mzima unajua kuwa umechapiwa? Kuchapiwa kunasameheka kama ni siri ya ndani walau, sio kwa levo hiyo
Aibu kwakweli...

Ila huwez jua huy mwanaume amewaza nini mpaka kumsamehe huyo dada. Ukute anampangia malipizi atakuja kujutia huko mbele. Umuumize mwanaume na kumdhalilisha kiasi hiki alafu akusamehe bure?? Subutuu
 
Habari za leo wakuu, Poleni na majukumu pia hongereni kwa kusheherekea vyema Sikukuu ya EID, japo kwangu haikuwa njema sana kutokana na shida nilizopitia.

Juzi nilikuja na Uzi nikiomba msaada nifanye nini juu ya majanga yaliyonikuta
Rejea:-

Leo nimeona Nilete mrejesho wa nini kimefanyika juu ya hili tukio.

Kikao cha Familia ya binti kimekaa leo Saa 4 asubuhi juu ya shauri la jamaa kudai mahari yake.

Watu wenye busara wamekaa na kuongea na kijana kuwa arudishe Moyo na waendelee na Process zao za uchumba kuelekea Ndoa.

Lakini kijana Amekuwa na Roho ngumu ssna kiasi cha kuto kusamehe. Hii ni kwasababu ameniona mara nyingi kwenye simu ya Mchumba wake na amesha muonya mara nyingi lakini binti amekuwa kiziwi, hivyo basi jamaa hawezi kuendelea na huo uchumba hivyo arudishiwe Mahari yake ajue nini cha kufanya.

Pia akaomba kama familia haina uwezo kwa wakati huo watoe chochote Tu hata elfu 10, ili mradi mahari imerudishwa.

Icho kikao mara kikageuga msiba watu karibia wote wakawa wanalia kwa kinachoenda kutokea.

Binti akaitwa kwenye kikao. Nae akawa analia. Akaulizwa kama anampenda jamaa, akasema anampenda sana kwani jamaa hakumpa muda wa kumsikiliza laa sivyo wangeyamaliza. Pia binti akaomba msamaha kwa kuiingiza familia kwenye matatizo.

Jamaa amepigiwa Magoti na mama yake na mama wa binti, ndio amekubali kuendelea na uchumba.

Mida ya saa 8 nimepigiwa simu na Deligation ya kikao nimepewa Onyo kubwa sana juu ya mahusiano yangu na binti. Nimekili sitarudiana naye tena na nimekata mawasiliano naye..

Nikaomba pia niongee na jamaa, nikaongea nae nimemuomba msamaha yeye kama mwanaume mwenzangu. Na jamaa amenisamehe kwa moyo mkunjufu kabisa.

Leo ndio nimeamini kuwa nimeachachana na huyu binti. Roho imeniuma sana maana yeye ndio mwanamke wa Ndoto yangu

Najiona kama nimeanza upya maisha bila huyu binti. Japo sikuwa na nafasi nae sana lakini nilikuwa nina amani.

Napenda kuwashukuru Nyote kwa michango yenu hadi kufikia kulimaliza Suala hili.
Umeona makwedeke wakipopompo na mazwezwede pamoja anaonekana mjanja for nothing.
 
Nimekuwekea na meseji ya mwanaume mwenzio ili ujue ni kwa namna gani umemuumiza. Ila hiyo laana haita kuucha hata kama sio kwako itakula watoto wako mpaka vitukuuView attachment 1120816
Mkuu hii Msg nimeiona na imeniumiza sana. Sikujua kama hili suala lingefikia huku. Anyway limekwisha
 
We endelea kujisifu tu ujinga, umewaumiza sana ndugu wa mwanamke na mwanaume pia, familia ya mwanaume ilishaanza vikao muda tu na miezi miwili ijayo harusi ilikuwa inafanyika mkoa S. Umevunja vikao mpuuzi wewe kwa tamaa zako za ngono! Unajua umempa mwenzio stress zisizokuwa za kawaida. Unajua ni mipango mingapi umemharibia, unajua gharama na muda aliotumia kutembea mikoa tofauti kuwataarifu ndugu? Unajua gharama za awali za maandalizi alizokuwa ametumia? Unawezaje kwenda Arusha saa 4 za usiku kwa mchumba wa mtu.
Usifikiri wewe ndo wa kwanza kupenda hata sisi kabla tulishakuwa na mademu ilipotokea wameolewa tuliwaacha waendelee na maisha yao. Lakini kwa maelezo yako unajiona kidume kwamba hata akiolewa utaendelea. Ipo siku utakuja kulia kilio kisicho na jina.
Mkuu nimeomba msamaha nimekubaliwa. Namshukuru Mungu
 
Ulisema kikao jmosi.

Wewe, mrembo na mchumba mnakaa mkoa tofauti na kwao binti.

Mchumba Kakukuta kwa mrembo saa 4 usiku kachukua tu vitu vyake kasepa na kusema neno halafu kasepa.

Mwendo wa masaa manne.

Jamaa kaenda kuomba kurudushiwa mahari Juzi leo tena yupo kwenye kikao.

Halafu kakusamehe na wewe kwa moyo mkunjufu. Na una ujasiri wa kupokea simu zao bila kuogopa.

Hii chai
Kikao sio Sabato kusema kwamba hakivunjwi.

Anyway karibu sana
 
Kweli dunia bado ina watu wazuri, how on earth do I accept that woman?

Watoto wa nje sometimes tunajitakia.
 
Back
Top Bottom