Wakuu, habari zenu...
Wiki moja iliyopita, nilileta post humu, nikimuelezea huyu demu wangu wa ajabu na adimu sana kwa nyakati hizi kutokea..
Nilieleza kwamba, huyu demu hata niende nimtoe out, hanaga gharama kabisa, na simzuii yeye kuitafuna cent yangu, lah!
Nilielezea ukubwa wa mapenz yake na vile asivyopenda makuu,.. Ana sifa zote na sikosi chochote na wakati wowote kwake, lakini hapendi matumizi makubwa...
Nilipoleta hapa furaha na sifa za huyo demu wangu, wengi wakasema, sijiongezi,.. Mara kitonga, wengine ananivizia anilipue,.. Nikayachukua nikayafanyia Kazi nisije nikampoteza mtamu huyu...
Hot Friday jion, nikawa nae maeneo mazuri saana, nimpe uhuru wa kujiachia, lakini kaishia kula pizza tu na juice... Nikaona isiwe tabu, nikaona busara ile pesa ambayo niliitenga weekend kwa ajili yake, nimpe awe huru kwa matumizi ayatakayo mwenyewe...
Ajabu sana;... Ile pesa kaenda shopping bhana, kakusanya zawadi na Jana jioni kaniletea aliponitembelea home, .. Kaniambia Ile pesa nilompa ndio kaamua kununua zawadi!
Wakuu,.. Hii nayo imekaaje, maana kama ni timing ya kunilipua, basi huo mzinga utakua sio wa mchezo!
Ila ninachoamini mimi, ni mapenz tu, nimebahatika,.... Au niendelee kuchukua tahadhari?