Huyu jamaa amenivunja moyo wa kujitolea

a hope

Senior Member
Oct 23, 2022
164
340
MWEZI uliopita midaa ya saa mbili usiku wakati narudi gheto niko mdogo mdogo na stress zangu, wakati nakaribia kufika gheto ghafla jamaa mmoja aliekuwa amesimama pembeni njiani akaniita "kaka samahani" ikabidi nisimame. Nimsikilize jamaa ana shida gani..

Baada ya salamu jamaa akaanza kunieleza yanayomsibu ni kuwa ana hali mbaya sana kiuchumi ana mke na mtoto mmoja na hana kitu chochote chakula ndani na tangu asubuhi ameondoka mke na mtoto wake hawajala kitu mpaka muda huu wanamsubili yeye arudi kutoka kazini ili wale hata chakula cha usiku na bahati mbaya huko kazini alikokuwa anategemea hajapata kitu chochote hivo anaomba kama katika matumizi yangu nimebakiza hata chenji Tsh. 1000/= anaomba nimpe akanunue hata dagaa wale hata usiku huu tuu. Kesho ataona afanyaje..

Daaah niliingiwa na huruma hasa ukizingatia jamaa ni mtu mzima kunizidi na kwa upande wangu pia nimepitia maisha magumu sana sana hivo nilikuwa naelewa fika jamaa anazungumzia nini ..

To shorten the story..niilimpa jamaa kiasi kidogo tu cha pesa ambacho niliamini kwa familia yake kingemtosha usiku huo na asubuhi yake basi siku hiyo ikapita..

Kesho yake mida ya saa moja kasoro jioni..nimetulia zangu gheto nashangaa mtu anagonga mlango..kufungua naomuona jamaa wa jana (niliimaki sauiti) ..ila ikabidi nijifanye kama simkumbuki..basi tukakaa njee

Baada ya salamu ..jamaa akaniuliza kama namkumbuka..nikajibu hapana sikukumbuki..basi jamaa akajitambulisha upya..

Wazo lilonijia kichwani ni kuwa jamaa kaja kutoa shukrani kwa msaada wa jana..

Na ni kweli baada ya salamu jamaa akanishukuru sana kwa msaada wa jana..ila akasema leo ana shida nyingine ila leo hajaja kuomba kama jana badala yake anaomba nimkopee kiasi fulani cha pesa ana shida sana sana na mimi ndio msaada wake wa pekee hana msaada mwingine ..daah nilishangaa

Kiukweli pesa aliyokuwa anataka ni ndogo ila ni zaidi ya niliyompa jana..

Iakini pia siku hiyo alarm kichwani kwangu iligonga kuwa leo ni kama napigwa maana jamaa alikuwa na kaharufu fulani ka pombe japo maelezo yake yalikuwa straight sana..

Basi badaa ya kulia sana nimkopee..nikaamua sio mbaya..nimepoteza vingapi....nikampa nusu ya pesa aliyokuwa anahitaji..akashukuru sana..akaondoka..

Aisee sijakaa hata nusu saa nashangaa mtu huyu hapa tena anagonga mlango..kutoka ni jamaa

Nikamuuliza nini tena ndugu yangu..akasema anaomba saana sana yupo chini ya miguu yangu..jamaa alietakiwa kumsaidia kwa kiasi kile cha pesa amekataa kata kata kumsaidia anadai anataka hela yote ndipo atamtatulia shida yake..daah nilichoka..nikamwambia ndugu yangu mimi sina hela hata hiyo nusu niliuokuazima nimechukua ya watu..

Jamaa akalia sana sana..daah nikaona sasa hii ni kelo na kuondoa kelo..kishingo upande sana nikampa nusu tena kwaiyo ikawa pesa imekamilika aliyohitajii..jamaa akashukuru sana akaondoka ila nikamsisitiza sana kuwa hiyo pesa niliyomuazima ni ya watu hivo kesho ajitahidi kurejesha..jamaa akanihakikishia kuwa kesho pesa inarudi..basi siku hiyo ikapita..

Kesho yake mida ile ile ya saa moja kasoro jioni jamaa huyu hapa..tena alinikuta nimekaa nje namsubili kwa hamu maana nilikuwa nawaza ikifika saa mbili usiku huyu jamaa hajaonekana nihesabu maumivu ile hela nimepigwaa...maana hadi muda huo nilikuwa sijui anakaa wapi japo alisema ni mtaa mmoja

Kwaiyo nilivomuona jamaa..nikafurahi sana nikajua pesa yangu hii hapa...aisee daah

Basi kama kawaida baada ya salamu jamaa akanishukuru sana kwa msaada wa jana na kumuamini

Ghafla badala ya kunipa pesa yangu..nikashangaa jamaa anaanza kueleza tena shida zake..mara anaomba tena nimkopee hela nyinginee..

Nilishtuka ikabidi nimuangalie jamaa vizuri usoni..nikawaza au jamaa ni chizi...lakini mbona mavazi yake ni ya kawaida tu..nikawaza au amelewa ..lakini mbona hana dalili japo kweli kulikuwa na kaharufu ka pombe..kwa mbali..

Nikamwambia kwa ukali kuwa leo pesa sina kwanza nilikupa pesa ya watu..na nadaiwa..jamaa akaendelea kulia lia..pale..hapo mimi tayari nimechafuka roho..

Ikabidi nimbane kuwa ile pesa ya jana ana uhakika ni kweli alikuwa na shidaa..akagomaa gomaa baada ya kumbana sana akaniambia kweli ile pesa ya jana alikuwa hana shida ilikuwa ni fix tu ila leo ndio anashida kweli..daah nilichoka..nikawaza inawezekana hata ile ya juzi ilikuwa ni fix pia ila nikakaushaa..basi jamaa akaondokaa..ila amenifanya nimekuwa muoga sana..nikimuona muhitaji napita mbali kabisaa saivi..

Ila nimejifunza kitu kama haujajiandaa kisaikolojia kupokea negative return ya msaada wako usimsaidie mtu..kwa sasa mambo ni mengi.

ROBERT HERIEL kuna mada moja alilizungumzia hili..alikuwa sahihi

Nawasilisha..
 
Wapo wengi tu watu wa aina hiyo? Kuna wale wanaofanya matatizo yao kama mitaji. Kuna m1 ana uvimbe flani hivi chini ya kitovu. Huu ni mwaka karibia wa 8 namwona anatembea na karatasi anaomba mchango akafanyiwe upasuaji. Mwenyewe anatembea wilaya za mkoa wa morogoro. Kilosa, kilombero na morogoro mjini.

Week mbili zilizopita nilimtolea uvivu. Nikampa ukweli wake.
 
Omba Mungu sana usije akakuinia. Inawezekana kuna ramani anachora. Mimi sitoi lift, sitoi hela kwa mtu nisiye mjua...kama ni shida nimepitia nyingi sana ila aijawahi kuomba kwa mtu alnisiye mjua. Nilisaidiwa na ndugu na jamaa wanaonizunguka, pale ambapo nilikwama kabisa.

Kila mtu ana ndugu na kila mtu ana jamaa zake. Haiwezekani mtu geneuine ashindwe kusaidiwa na watu wake wa karibu hadi aombe mtu barabarani. Ukiona mtu wa aina hiyo ujue siyo genuiene
 
sure..nakubali mkuu
 
Wapo wengi tu watu wa aina hiyo? Kuna wale wanaofanya matatizo yao kama mitaji. Kuna m1 ana uvimbe flani hivi chini ya kitovu. Huu ni mwaka karibia wa 8 namwona anatembea na karatasi anaomba mchango akafanyiwe upasuaji. Mwenyewe anatembea wilaya za mkoa wa morogoro. Kilosa, kilombero na morogoro mjini.

Week mbili zilizopita nilimtolea uvivu. Nikampa ukweli wake.
Yaan ni changamoto..yaani bora hata huyo ana tatizo linaonekana..sasa huyu anatengeneza tatizo maana yake ana nature ya utapeli na wizi..
 
MWEZI uliopita midaa ya saa mbili usiku wakati narudi gheto niko mdogo mdogo na stress zangu..wakati nakaribia kufika gheto ghafla jamaa mmoja aliekuwa amesimama pembeni njiani akaniita "kaka samahani"..ikabidi nisimame.. nimsikilize jamaa ana shida gani..

baaada ya salamu jamaa akaanza kunieleza yanayomsibu ni kuwa ana hali mbaya sana kiuchumi..ana mke na mtoto mmoja na hana kitu chochote chakula ndani ..na tangu asubuhi ameondoka mke na mtoto wake hawajala kitu mpaka muda huu wanamsubili yeye arudi kutoka kazini ili wale hata chakula cha usiku na bahati mbaya huko kazini alikokuwa anategemea hajapata kitu chochote..hivo anaomba kama katika matumizi yangu nimebakiza hata chenji sh.1000/= anaomba nimpe akanunue hata dagaa wale hata usiku huu tuu..kesho ataona afanyaje..

Daaah niliingiwa na huruma hasa ukizingatia jamaa ni mtu mzima kunizidi..na kwa upande wangu pia nimepitia maisha magumu sana sana...hivo nilikuwa naelewa fika jamaa anazungumzia nini ..

To shorten the story..niilimpa jamaa kiasi kidogo tu cha pesa ambacho niliamini kwa familia yake kingemtosha usiku huo na asubuhi yake..basi siku hiyo ikapita..

Kesho yake..mida ya saa moja kasoro jioni..nimetulia zangu gheto nashangaa mtu anagonga mlango..kufungua naomuona jamaa wa jana (niliimaki sauiti) ..ila ikabidi nijifanye kama simkumbuki..basi tukakaa njee

Baada ya salamu ..jamaa akaniuliza kama namkumbuka..nikajibu hapana sikukumbuki..basi jamaa akajitambulisha upya..

Wazo lilonijia kichwani ni kuwa jamaa kaja kutoa shukrani kwa msaada wa jana..

Na ni kweli baada ya salamu jamaa akanishukuru sana kwa msaada wa jana..ila akasema leo ana shida nyingine ila leo hajaja kuomba kama jana badala yake anaomba nimkopee kiasi flani cha pesa ana shida sana sana..na mimi ndio msaada wake wa pekee..hana msaada mwingine ..daah nilishangaa

Kiukweli pesa aliyokuwa anataka ni ndogo ila ni zaidi ya niliyompa jana..

Iakini pia siku hiyo alarm kichwani kwangu iligonga kuwa leo ni kama napigwa maana jamaa alikuwa na kaharufu flani ka pombe..japo maelezo yake yalikuwa straight sana..

Basi badaa ya kulia sana nimkopee..nikaamua sio mbaya..nimepoteza vingapi....nikampa nusu ya pesa aliyokuwa anahitaji..akashukuru sana..akaondoka..

Aisee sijakaa hata nusu saa nashangaa mtu huyu hapa tena anagonga mlango..kutoka ni jamaa

Nikamuuliza nini tena ndugu yangu..akasema anaomba saana sana yupo chini ya miguu yangu..jamaa alietakiwa kumsaidia kwa kiasi kile cha pesa amekataa kata kata kumsaidia anadai anataka hela yote ndipo atamtatulia shida yake..daah nilichoka..nikamwambia ndugu yangu mimi sina hela hata hiyo nusu niliuokuazima nimechukua ya watu..

Jamaa akalia sana sana..daah nikaona sasa hii ni kelo na kuondoa kelo..kishingo upande sana nikampa nusu tena kwaiyo ikawa pesa imekamilika aliyohitajii..jamaa akashukuru sana akaondoka ila nikamsisitiza sana kuwa hiyo pesa niliyomuazima ni ya watu hivo kesho ajitahidi kurejesha..jamaa akanihakikishia kuwa kesho pesa inarudi..basi siku hiyo ikapita..

Kesho yake mida ile ile ya saa moja kasoro jioni jamaa huyu hapa..tena alinikuta nimekaa nje namsubili kwa hamu maana nilikuwa nawaza ikifika saa mbili usiku huyu jamaa hajaonekana nihesabu maumivu ile hela nimepigwaa...maana hadi muda huo nilikuwa sijui anakaa wapi japo alisema ni mtaa mmoja

Kwaiyo nilivomuona jamaa..nikafurahi sana nikajua pesa yangu hii hapa...aisee daah

Basi kama kawaida baada ya salamu jamaa akanishukuru sana kwa msaada wa jana na kumuamini

Ghafla badala ya kunipa pesa yangu..nikashangaa jamaa anaanza kueleza tena shida zake..mara anaomba tena nimkopee hela nyinginee..

Nilishtuka ikabidi nimuangalie jamaa vizuri usoni..nikawaza au jamaa ni chizi...lakini mbona mavazi yake ni ya kawaida tu..nikawaza au amelewa ..lakini mbona hana dalili japo kweli kulikuwa na kaharufu ka pombe..kwa mbali..

Nikamwambia kwa ukali kuwa leo pesa sina kwanza nilikupa pesa ya watu..na nadaiwa..jamaa akaendelea kulia lia..pale..hapo mimi tayari nimechafuka roho..

Ikabidi nimbane kuwa ile pesa ya jana ana uhakika ni kweli alikuwa na shidaa..akagomaa gomaa baada ya kumbana sana akaniambia kweli ile pesa ya jana alikuwa hana shida ilikuwa ni fix tu ila leo ndio anashida kweli..daah nilichoka..nikawaza inawezekana hata ile ya juzi ilikuwa ni fix pia ila nikakaushaa..basi jamaa akaondokaa..ila amenifanya nimekuwa muoga sana..nikimuona muhitaji napita mbali kabisaa saivi..

Ila nimejifunza kitu kama haujajiandaa kisaikolojia kupokea negative return ya msaada wako usimsaidie mtu..kwa sasa mambo ni mengi.

ROBERT HERIEL kuna mada moja alilizungumzia hili..alikuwa sahihi

Nawasilisha..

Pole Sana Mkuu. Wengine mpaka yawakute Kwanza ndio mtie akili
 
Kuna wajinga wengi wa hivi siku hizi na wanasababisha hata wahitaji wa kweli wasisaidiwe. Kuna fala mmoja pale mkumbusho stand alikuaga anaomba eti katoka church hana nauli na anakaa mbali nauli buku ndio inamfikisha. Nilimpakaga buku mbili...nikashangaa baada ya wiki kajimix tena nikampotezea. Cha kushangaza niliendeleaga kumuona pale jioni akiwafuata watu tofautitofauti na anaonekana kama gentleman flani wa uswazi
 
kabisa kabisa nimejifunza kitu
 
Back
Top Bottom