Mrejesho: Matusi na kejeli ya mume wangu

Ndoa ikishaingia shubiri ni hatari tupu, inakuwa jela na zaidi ya mateso. Ukikutana na tapeli wa mapenzi usipoangalia waweza kufwa. Nakupa pole, maisha lazima yasonge, jipe moyo.

Ushauri: Jipumzishe na mahusiano kwa mda, rebound ya haraka inaweza kukuumiza zaidi.
 
HAKIKA
 
teh teh poleni aisee ! we nijulie hali mimi tu mume anahu?????????????????????????????????????????????????? teh kidding ! hajambooooooooooooooo anabet km wewe mxiew
hahahhaah we leta kiburi akati hizo hela zake ndo unanunulia luku na kujaza friji heheeee
 
Habari za mchana wapendwa wana JF

Kwanza kabisa natoa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia pumzi na afya njema

Napenda kutoa mrejesho wa uzi wangu ambao niliuleta kwenye hili jukwaa umepita muda kidogo, uzi huo ''Maneno ya kejeli ya mume wangu'' https://www.jamiiforums.com/threads/maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.876139/ na mrejesho wa awali Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu
https://www.jamiiforums.com/threads/mrejesho-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.983952/
Nashukuru Mungu kesi imeisha mahakamani ingawa si kwa matarajio ambayo nilikuwa nayo. Nimepewa talaka yangu na mahakama, hii ni baada ya mahakama kujiridhisha kwamba hii ndoa haiwezi kurekebishika. Ndoa tulifunga ya kiislamu na tuliishi pamoja kwa miaka mitano bila kuwa na mtoto, tulifuata taratibu zote za dini katika kutafuta suluhu lakini ilishindikana.

Pamoja na kutoa talaka, mahakama iliamua kumuachia nyumba ambayo nilichangia gharama nyingi tu kwa kuwa eti hapakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kuwa nilichangia. Ifahamike kwamba nyumba nilimkuta nayo lakini hakuwa anaishi hapo maana ilikuwa haijaisha. Baada ya kuoana tulikubaliana kuimalizia kisha kuhamia pale. Kulikuwa na risiti na tuliandika gharama zote za manunuzi na ufundi, lakini kwa makusudi kabisa alizificha kwa hiyo sikuweza kuzipata.

Mimi sikuwa na shida sana na nyumba kwani nilivyoondoka nilimuambia anirudishie gari yangu ambayo niliipata kabla ya ndoa. Gari nilinunua kabla ya ndoa, baada ya kufunga naye ndoa nikampa awe anatumia yeye kwani nilipewa gari la ofisi kutumia. Mwaka 2014 ile gari ikapata ajali, kwani alidumbukia kwenye maji injini ikafa kabisa.

Kwa sababu ilikuwa na bima kubwa waliweza kunilipa milioni 6.6, lakini hizo hela zilipitia kwenye account ya ndugu yangu ambaye nilinunua gari kwenye yadi yake. Hela ililipwa kwenye account ya ndugu yangu kwa sababu nilikuwa sijabadilisha jina. Nilikuwa sina mpango wa kununua gari nyingine ila akawa ananishawishi kweli niongezee hela kununua gari jingine.

Kuna mama mmoja akawa anauza gari yake kwani alikuwa anaenda Marekani kuishi huko, gariilikuwa nzuri sana kwani aliitumia muda mfupi, tukaenda vizuri kuiona hiyo gari na tukakubaliana tutaichukua.

Kwa sababu nilikuwa nasafiri nje ya nchi kikazi niamuambia ndugu yangu ampe hela mume wangu cash, halafu nikampa kama 2.4 ikawa milioni 9. Basi mimi nikiwa nimesafiri alienda kuchukua zile hela kwa ndugu yangu kama nilvyomuagiza na akaenda kulipia gari. Kweli gari ikaja tukawa tunaitumia.

Baada ya miezi kadhaa nikakumbuka suala la kubadili jina ili liwe na jina langu. Sikumoja naagalia kwenye file ili nichukue kadi nikawa siioni. Kumbe kadi alishaenda kuificha anakojua yeye. Kuuliza ananiambia una gari wewe, na huna uthibitisho kwamba nilipokea hela yoyote kutoka kwako na huyo ndugu yako.

Alifanikiwa kuiuza ile gari hivyo kupoteza ushahidi mahakamani ingawa ndugu yangu aliyeniuzia alikuja kutoa ushahidi kama alimpa hela, kosa ni kuwa hakuandikisha na yeye kwani wanamfahamu kuwa ni mume halali wa ndoa. Kwa upande wetu tuliomba ile gari ikamatwe na mahakama lakini hakimu alikataa kwa sababu anazozijua yeye.

Niliambulia kiwanja tu, ambacho ni mali yangu binafsi. Huyu mwanaume toka tumeoana hakuwa na kazi ya kumuingizia kipato cha kutosha kwani alifukuzwa alikokuwa anafanya, na pia alikuwa na kesi kwa hiyo hakuweza kuajiriwa tena.

Rafiki zangu na baadhi ya jamaa wamenishauri nikate rufaa mahakama kuu ila mimi mwenyewe siko tayari maana huyu mwanaume anaweza kunifanyia lolote, ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa RPC wa mkoa fulani zamani ambaye naye ni dhulmati na maisha yake hayaeleweki saizi.

Familia yangu hasa mama amenisihi niachane na hii kesi na niwe na amani kabisa kwani nitapata vingi zaidi ya hivyo alivyochukua. Namshukuru Mungu kwani miaka miwili baada ya kuachana naye (toka October 2015) nimepata baraka nyingi na kupata zaidi ya vile alivyochukua. Naamini Mungu ni mwema na anajua ukweli wote. Nimeamua kumuachia yeye kwani ndio hakimu mkuu, maisha lazima yaendelee na nimejifunza mengi sana kutokana na hili.

Naona amerudiana na yule mchepuko wake kwani nimeshawaona wako pamoja si mara moja.

Niwashukuru sana wa JF kwa michango na ushauri wenu. Ni matumanini yangu kwamba nanyi mmejifunza kupitia hili.

Mbarikiwe sana

Asanteni.
Ubarikiwe Dada,mungu atakuongezea zaidi na zaidi .Amani ni zaidi kuliko mtalaka wako.
 
Ila hata wewe kwa mwandiko wako inaonekana una matatizo yako mengi umeyaficha
Sidhani kama nia yake ni kuelezea matatizo yao. Wameshindwana baas. Ameeleza ni jinsi gani amenyimwa haki zake za msingi.
 
Asante kwa ushauri, ila siwezi kukata rufaa kwani hizi kesi zina stress nyingi na mambo mengi sana, Ninachotaka ni amani ya moyo na uzima wangu
Pole karibu pia upumzishe akili ila kama utaonayafaa basi tulia kwanza bila kuingia kwenye mahusiano maana ni pasua kichwa hiyo stay relaxed
 
Sidhani kama nia yake ni kuelezea matatizo yao. Wameshindwana baas. Ameeleza ni jinsi gani amenyimwa haki zake za msingi.

una akili sana wewe mdada ! nimekupa point sana hapa ! watu bwana!
 
Bora mapenzi yangejulikana kua ni vita basi ujipange kwa zana za kutosha..tatizo unaingia na kamoyo kako kamoja kakikutana na moto ndio ivyo tena.
 
pole sana uyo mpotezee kabisa nadhani lesson kubwa don't trust anybody 100% na kuuziana au kupeana vitu kienyeji ushahidi ni muhimu
 
Hili ndio fundisho kubwa kwangu na wengine
 
Habari za mchana wapendwa wana JF

Kwanza kabisa natoa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia pumzi na afya njema

Napenda kutoa mrejesho wa uzi wangu ambao niliuleta kwenye hili jukwaa umepita muda kidogo, uzi huo ''Maneno ya kejeli ya mume wangu'' https://www.jamiiforums.com/threads/maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.876139/ na mrejesho wa awali Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu
https://www.jamiiforums.com/threads/mrejesho-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.983952/
Nashukuru Mungu kesi imeisha mahakamani ingawa si kwa matarajio ambayo nilikuwa nayo. Nimepewa talaka yangu na mahakama, hii ni baada ya mahakama kujiridhisha kwamba hii ndoa haiwezi kurekebishika. Ndoa tulifunga ya kiislamu na tuliishi pamoja kwa miaka mitano bila kuwa na mtoto, tulifuata taratibu zote za dini katika kutafuta suluhu lakini ilishindikana.

Pamoja na kutoa talaka, mahakama iliamua kumuachia nyumba ambayo nilichangia gharama nyingi tu kwa kuwa eti hapakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kuwa nilichangia. Ifahamike kwamba nyumba nilimkuta nayo lakini hakuwa anaishi hapo maana ilikuwa haijaisha. Baada ya kuoana tulikubaliana kuimalizia kisha kuhamia pale. Kulikuwa na risiti na tuliandika gharama zote za manunuzi na ufundi, lakini kwa makusudi kabisa alizificha kwa hiyo sikuweza kuzipata.

Mimi sikuwa na shida sana na nyumba kwani nilivyoondoka nilimuambia anirudishie gari yangu ambayo niliipata kabla ya ndoa. Gari nilinunua kabla ya ndoa, baada ya kufunga naye ndoa nikampa awe anatumia yeye kwani nilipewa gari la ofisi kutumia. Mwaka 2014 ile gari ikapata ajali, kwani alidumbukia kwenye maji injini ikafa kabisa.

Kwa sababu ilikuwa na bima kubwa waliweza kunilipa milioni 6.6, lakini hizo hela zilipitia kwenye account ya ndugu yangu ambaye nilinunua gari kwenye yadi yake. Hela ililipwa kwenye account ya ndugu yangu kwa sababu nilikuwa sijabadilisha jina. Nilikuwa sina mpango wa kununua gari nyingine ila akawa ananishawishi kweli niongezee hela kununua gari jingine.

Kuna mama mmoja akawa anauza gari yake kwani alikuwa anaenda Marekani kuishi huko, gariilikuwa nzuri sana kwani aliitumia muda mfupi, tukaenda vizuri kuiona hiyo gari na tukakubaliana tutaichukua.

Kwa sababu nilikuwa nasafiri nje ya nchi kikazi niamuambia ndugu yangu ampe hela mume wangu cash, halafu nikampa kama 2.4 ikawa milioni 9. Basi mimi nikiwa nimesafiri alienda kuchukua zile hela kwa ndugu yangu kama nilvyomuagiza na akaenda kulipia gari. Kweli gari ikaja tukawa tunaitumia.

Baada ya miezi kadhaa nikakumbuka suala la kubadili jina ili liwe na jina langu. Sikumoja naagalia kwenye file ili nichukue kadi nikawa siioni. Kumbe kadi alishaenda kuificha anakojua yeye. Kuuliza ananiambia una gari wewe, na huna uthibitisho kwamba nilipokea hela yoyote kutoka kwako na huyo ndugu yako.

Alifanikiwa kuiuza ile gari hivyo kupoteza ushahidi mahakamani ingawa ndugu yangu aliyeniuzia alikuja kutoa ushahidi kama alimpa hela, kosa ni kuwa hakuandikisha na yeye kwani wanamfahamu kuwa ni mume halali wa ndoa. Kwa upande wetu tuliomba ile gari ikamatwe na mahakama lakini hakimu alikataa kwa sababu anazozijua yeye.

Niliambulia kiwanja tu, ambacho ni mali yangu binafsi. Huyu mwanaume toka tumeoana hakuwa na kazi ya kumuingizia kipato cha kutosha kwani alifukuzwa alikokuwa anafanya, na pia alikuwa na kesi kwa hiyo hakuweza kuajiriwa tena.

Rafiki zangu na baadhi ya jamaa wamenishauri nikate rufaa mahakama kuu ila mimi mwenyewe siko tayari maana huyu mwanaume anaweza kunifanyia lolote, ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa RPC wa mkoa fulani zamani ambaye naye ni dhulmati na maisha yake hayaeleweki saizi.

Familia yangu hasa mama amenisihi niachane na hii kesi na niwe na amani kabisa kwani nitapata vingi zaidi ya hivyo alivyochukua. Namshukuru Mungu kwani miaka miwili baada ya kuachana naye (toka October 2015) nimepata baraka nyingi na kupata zaidi ya vile alivyochukua. Naamini Mungu ni mwema na anajua ukweli wote. Nimeamua kumuachia yeye kwani ndio hakimu mkuu, maisha lazima yaendelee na nimejifunza mengi sana kutokana na hili.

Naona amerudiana na yule mchepuko wake kwani nimeshawaona wako pamoja si mara moja.

Niwashukuru sana wa JF kwa michango na ushauri wenu. Ni matumanini yangu kwamba nanyi mmejifunza kupitia hili.

Mbarikiwe sana

Asanteni.
 
Yupo jamaa ila hatujaanza uhusiano rasmi, nilitaka kumalizana na kesi kwanza kwani hukumu imetoka mwisho wa mwezi uliopita
Pole sana...ila kuwa makini kwa huyu mwingine asije akawa ni tapeli km yule aliyepita.....
 
Back
Top Bottom