Mrejesho: Matusi na kejeli ya mume wangu

N
Habari za mchana wapendwa wana JF

Kwanza kabisa natoa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia pumzi na afya njema

Napenda kutoa mrejesho wa uzi wangu ambao niliuleta kwenye hili jukwaa umepita muda kidogo, uzi huo ''Maneno ya kejeli ya mume wangu'' https://www.jamiiforums.com/threads/maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.876139/ na mrejesho wa awali Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu
Nashukuru Mungu kesi imeisha mahakamani ingawa si kwa matarajio ambayo nilikuwa nayo. Nimepewa talaka yangu na mahakama, hii ni baada ya mahakama kujiridhisha kwamba hii ndoa haiwezi kurekebishika. Ndoa tulifunga ya kiislamu na tuliishi pamoja kwa miaka mitano bila kuwa na mtoto, tulifuata taratibu zote za dini katika kutafuta suluhu lakini ilishindikana.

Pamoja na kutoa talaka, mahakama iliamua kumuachia nyumba ambayo nilichangia gharama nyingi tu kwa kuwa eti hapakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kuwa nilichangia. Ifahamike kwamba nyumba nilimkuta nayo lakini hakuwa anaishi hapo maana ilikuwa haijaisha. Baada ya kuoana tulikubaliana kuimalizia kisha kuhamia pale. Kulikuwa na risiti na tuliandika gharama zote za manunuzi na ufundi, lakini kwa makusudi kabisa alizificha kwa hiyo sikuweza kuzipata.

Mimi sikuwa na shida sana na nyumba kwani nilivyoondoka nilimuambia anirudishie gari yangu ambayo niliipata kabla ya ndoa. Gari nilinunua kabla ya ndoa, baada ya kufunga naye ndoa nikampa awe anatumia yeye kwani nilipewa gari la ofisi kutumia. Mwaka 2014 ile gari ikapata ajali, kwani alidumbukia kwenye maji injini ikafa kabisa.

Kwa sababu ilikuwa na bima kubwa waliweza kunilipa milioni 6.6, lakini hizo hela zilipitia kwenye account ya ndugu yangu ambaye nilinunua gari kwenye yadi yake. Hela ililipwa kwenye account ya ndugu yangu kwa sababu nilikuwa sijabadilisha jina. Nilikuwa sina mpango wa kununua gari nyingine ila akawa ananishawishi kweli niongezee hela kununua gari jingine.

Kuna mama mmoja akawa anauza gari yake kwani alikuwa anaenda Marekani kuishi huko, gariilikuwa nzuri sana kwani aliitumia muda mfupi, tukaenda vizuri kuiona hiyo gari na tukakubaliana tutaichukua.

Kwa sababu nilikuwa nasafiri nje ya nchi kikazi niamuambia ndugu yangu ampe hela mume wangu cash, halafu nikampa kama 2.4 ikawa milioni 9. Basi mimi nikiwa nimesafiri alienda kuchukua zile hela kwa ndugu yangu kama nilvyomuagiza na akaenda kulipia gari. Kweli gari ikaja tukawa tunaitumia.

Baada ya miezi kadhaa nikakumbuka suala la kubadili jina ili liwe na jina langu. Sikumoja naagalia kwenye file ili nichukue kadi nikawa siioni. Kumbe kadi alishaenda kuificha anakojua yeye. Kuuliza ananiambia una gari wewe, na huna uthibitisho kwamba nilipokea hela yoyote kutoka kwako na huyo ndugu yako.

Alifanikiwa kuiuza ile gari hivyo kupoteza ushahidi mahakamani ingawa ndugu yangu aliyeniuzia alikuja kutoa ushahidi kama alimpa hela, kosa ni kuwa hakuandikisha na yeye kwani wanamfahamu kuwa ni mume halali wa ndoa. Kwa upande wetu tuliomba ile gari ikamatwe na mahakama lakini hakimu alikataa kwa sababu anazozijua yeye.

Niliambulia kiwanja tu, ambacho ni mali yangu binafsi. Huyu mwanaume toka tumeoana hakuwa na kazi ya kumuingizia kipato cha kutosha kwani alifukuzwa alikokuwa anafanya, na pia alikuwa na kesi kwa hiyo hakuweza kuajiriwa tena.

Rafiki zangu na baadhi ya jamaa wamenishauri nikate rufaa mahakama kuu ila mimi mwenyewe siko tayari maana huyu mwanaume anaweza kunifanyia lolote, ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa RPC wa mkoa fulani zamani ambaye naye ni dhulmati na maisha yake hayaeleweki saizi.

Familia yangu hasa mama amenisihi niachane na hii kesi na niwe na amani kabisa kwani nitapata vingi zaidi ya hivyo alivyochukua. Namshukuru Mungu kwani miaka miwili baada ya kuachana naye (toka October 2015) nimepata baraka nyingi na kupata zaidi ya vile alivyochukua. Naamini Mungu ni mwema na anajua ukweli wote. Nimeamua kumuachia yeye kwani ndio hakimu mkuu, maisha lazima yaendelee na nimejifunza mengi sana kutokana na hili.

Naona amerudiana na yule mchepuko wake kwani nimeshawaona wako pamoja si mara moja.

Niwashukuru sana wa JF kwa michango na ushauri wenu. Ni matumanini yangu kwamba nanyi mmejifunza kupitia hili.

Mbarikiwe sana

Asanteni.
Mwanamke akisha kuwa tajiri hakuna ndoa tena mnapenda kupora sana nyinyi sijui ni nani aliyewaroga. Ujinga mtupu...
 
Hongera Mamy
Hizi ndoa hizi jamani basi tu
Usipoolewa /kuoa taabu
Ukiolewa/kuoa nako taabu
Sijui kipi ni kipi
Ndoa ni ushenzi tuu kwanza huyu mwanamke anaonekana aliolewa afanye fujo apore nyumba na mali zingine ila kakosa shida tuuup
 
Acha ujinga wewe unadhani kila mwanamke anaishi kwa kutegemea mali za mwanaume.
 
Yote uliyoeleza ni sawa na pengine pasi na shaka yako sahihi but jambo moja hukulijua,nalo ni, "Mwanamke ndiye mwenye uwezo wa kusababisha ndoa idumu au ivunjike (akishirikiana na mume wake)". Wanaume tuna kazi ya kuanzisha tu,kuifanya iwepo (and virse is true), akishirikina, na mke wake.

Mwisho; Maisha ni lazima yaendelee. Sana tu!..
 
Acha ujinga wewe unadhani kila mwanamke anaishi kwa kutegemea mali mwanaume.
za
Nimeacha ujinga lakini uliyeolewa naye maskini sana au unavihela kuliko wewe? Elimu yake kubwa kuliko yako au ipo chini ya ile ya kwako? Mimi hupenda kuwa chini ya mtu kiuchumi, kielimu, kiumri hata kimadaraka lakini ukiniuliza unapenda kuwa chini ya mtu nitakwambia hapana. Na ndiyo maana mimi ni mjinga ila nimeacha ujinga leo kwa amri yako. Asante dada au mama
 
Habari za mchana wapendwa wana JF

Kwanza kabisa natoa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia pumzi na afya njema

Napenda kutoa mrejesho wa uzi wangu ambao niliuleta kwenye hili jukwaa umepita muda kidogo, uzi huo ''Maneno ya kejeli ya mume wangu'' https://www.jamiiforums.com/threads/maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.876139/ na mrejesho wa awali Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu
https://www.jamiiforums.com/threads/mrejesho-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.983952/
Nashukuru Mungu kesi imeisha mahakamani ingawa si kwa matarajio ambayo nilikuwa nayo. Nimepewa talaka yangu na mahakama, hii ni baada ya mahakama kujiridhisha kwamba hii ndoa haiwezi kurekebishika. Ndoa tulifunga ya kiislamu na tuliishi pamoja kwa miaka mitano bila kuwa na mtoto, tulifuata taratibu zote za dini katika kutafuta suluhu lakini ilishindikana.

Pamoja na kutoa talaka, mahakama iliamua kumuachia nyumba ambayo nilichangia gharama nyingi tu kwa kuwa eti hapakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kuwa nilichangia. Ifahamike kwamba nyumba nilimkuta nayo lakini hakuwa anaishi hapo maana ilikuwa haijaisha. Baada ya kuoana tulikubaliana kuimalizia kisha kuhamia pale. Kulikuwa na risiti na tuliandika gharama zote za manunuzi na ufundi, lakini kwa makusudi kabisa alizificha kwa hiyo sikuweza kuzipata.

Mimi sikuwa na shida sana na nyumba kwani nilivyoondoka nilimuambia anirudishie gari yangu ambayo niliipata kabla ya ndoa. Gari nilinunua kabla ya ndoa, baada ya kufunga naye ndoa nikampa awe anatumia yeye kwani nilipewa gari la ofisi kutumia. Mwaka 2014 ile gari ikapata ajali, kwani alidumbukia kwenye maji injini ikafa kabisa.

Kwa sababu ilikuwa na bima kubwa waliweza kunilipa milioni 6.6, lakini hizo hela zilipitia kwenye account ya ndugu yangu ambaye nilinunua gari kwenye yadi yake. Hela ililipwa kwenye account ya ndugu yangu kwa sababu nilikuwa sijabadilisha jina. Nilikuwa sina mpango wa kununua gari nyingine ila akawa ananishawishi kweli niongezee hela kununua gari jingine.

Kuna mama mmoja akawa anauza gari yake kwani alikuwa anaenda Marekani kuishi huko, gariilikuwa nzuri sana kwani aliitumia muda mfupi, tukaenda vizuri kuiona hiyo gari na tukakubaliana tutaichukua.

Kwa sababu nilikuwa nasafiri nje ya nchi kikazi niamuambia ndugu yangu ampe hela mume wangu cash, halafu nikampa kama 2.4 ikawa milioni 9. Basi mimi nikiwa nimesafiri alienda kuchukua zile hela kwa ndugu yangu kama nilvyomuagiza na akaenda kulipia gari. Kweli gari ikaja tukawa tunaitumia.

Baada ya miezi kadhaa nikakumbuka suala la kubadili jina ili liwe na jina langu. Sikumoja naagalia kwenye file ili nichukue kadi nikawa siioni. Kumbe kadi alishaenda kuificha anakojua yeye. Kuuliza ananiambia una gari wewe, na huna uthibitisho kwamba nilipokea hela yoyote kutoka kwako na huyo ndugu yako.

Alifanikiwa kuiuza ile gari hivyo kupoteza ushahidi mahakamani ingawa ndugu yangu aliyeniuzia alikuja kutoa ushahidi kama alimpa hela, kosa ni kuwa hakuandikisha na yeye kwani wanamfahamu kuwa ni mume halali wa ndoa. Kwa upande wetu tuliomba ile gari ikamatwe na mahakama lakini hakimu alikataa kwa sababu anazozijua yeye.

Niliambulia kiwanja tu, ambacho ni mali yangu binafsi. Huyu mwanaume toka tumeoana hakuwa na kazi ya kumuingizia kipato cha kutosha kwani alifukuzwa alikokuwa anafanya, na pia alikuwa na kesi kwa hiyo hakuweza kuajiriwa tena.

Rafiki zangu na baadhi ya jamaa wamenishauri nikate rufaa mahakama kuu ila mimi mwenyewe siko tayari maana huyu mwanaume anaweza kunifanyia lolote, ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa RPC wa mkoa fulani zamani ambaye naye ni dhulmati na maisha yake hayaeleweki saizi.

Familia yangu hasa mama amenisihi niachane na hii kesi na niwe na amani kabisa kwani nitapata vingi zaidi ya hivyo alivyochukua. Namshukuru Mungu kwani miaka miwili baada ya kuachana naye (toka October 2015) nimepata baraka nyingi na kupata zaidi ya vile alivyochukua. Naamini Mungu ni mwema na anajua ukweli wote. Nimeamua kumuachia yeye kwani ndio hakimu mkuu, maisha lazima yaendelee na nimejifunza mengi sana kutokana na hili.

Naona amerudiana na yule mchepuko wake kwani nimeshawaona wako pamoja si mara moja.

Niwashukuru sana wa JF kwa michango na ushauri wenu. Ni matumanini yangu kwamba nanyi mmejifunza kupitia hili.

Mbarikiwe sana

Asanteni.
Kila litokealo lina sababu kuwa na amani
 
Pole na Hongera. Ila Sisi Wanawake ukiona unaanza kufuatilia anaishi na Nani hizo ni dalili mbaya. Please kaa mbali naye. Story zake usizitafute na hama karibu yake. Utakuja na uzi hapo kuomba ushauri ikiwa too late. Stay away ohhhhhh. Sis viumbe wa jabu sana
 
Sijabahatika kwani sijawi na uhusiano na mwanume mwingine toka tuachane
Tuliaa mpaka akili ikae sawa utampata tu mshukuru Mungu kwa kila jambo huwezi jua Mungu kakuepushia nini hivyo alivyo kufanyia vikawa ni vidogo fanya kazi yako mambo yasonge
 
Asante kwa ushauri
 
Mal
Ndoa ni ushenzi tuu kwanza huyu mwanamke anaonekana aliolewa afanye fujo apore nyumba na mali zingine ila kakosa shida tuuup
Hahah , yaani unadhani kila mwanamke yuko after money.
 
Imeshapita miaka mitano sasa, lete mrejesho kuhusu mahusiano mapya, uliolewa tena au upo kwenye mahusiano tu? Vipi kuhusu ex-husband, alioa au?
 
Back
Top Bottom