Mrejesho: Matusi na kejeli ya mume wangu

Mrejesho: Matusi na kejeli ya mume wangu

Ingia tu ndugu yangu ndoa hazifanani

Sasa umeachia huku una kinyongo, maana unaandika as if ujaridhika,

Kama unaamua kusamehe, samehee moja kwa moja wala Usilaani, sijapenda hapo uliposema
"Naamini Mungu ni mwema na anajua ukweli wote. Nimeamua kumuachia yeye kwani ndio hakimu mkuu"

Je unapenda apate shida na adharirike huyo aliyekuwa mmeo?
 
Kata rufaa dadaake iyo nyumba mtagawana na ukishamaliza eda nitafute nilete posa aisee
Asante kwa ushauri, ila siwezi kukata rufaa kwani hizi kesi zina stress nyingi na mambo mengi sana, Ninachotaka ni amani ya moyo na uzima wangu
 
Mshauri mtaliki wako nae aje atoe stori ya upande wake ili kubalance story kisha nitacomment. La sivyo, kwa nilivyokuelewa kwa hii post fupi tu aisee nikiongea chochote kuhusu dizaini ya mwanamke wewe ntakukatisha tamaa bure.
 
Haiwezekani yeye ana matatizo tuuuuu... Tupe na kuhusu wewe kidogo madame, maana hatuwezi kukupa full hongera na pole bila kusikiliza upande wa pili. Anaweza kuja mumeo hapa naye akaanza kushuka essay basi ikawa tafrani.
Twambie ni kweli alipendelewa na Mahakama au Mahakama ilitenda haki, maana kuna sehemu unaonakena unamlaumu Jaji.

Mimi sijamlamu jaji, tatizo kubwa lilikuwa kwenye ushahidi si unajua hizi kesi zilivyo. Lakini hata mchango wangu haukuonekana hata kidogo kama mwanamke, hili nalo linashangaza. Huyu mwanaume ana matatizo ingekuwa inawezekana ningekupa details za huyu jamaa halafu ukafuatilia mtaani utashangaa. Hakuna hata ndugu yake upande wa baba yake anaongea naye. Mtu alidiriki kumuambia baba yake kama atachoma nyumba yake moto kama ataendelea kunitetea, Mpaka leo ninavyoandika wazazi wake hawaongei naye, sembuse mimi.
 
Mimi sijamlamu jaji, tatizo kubwa lilikuwa kwenye ushahidi si unajua hizi kesi zilivyo. Lakini hata mchango wangu haukuonekana hata kidogo kama mwanamke, hili nalo linashangaza. Huyu mwanaume ana matatizo ingekuwa inawezekana ningekupa details za huyu jamaa halafu ukafuatilia mtaani utashangaa. Hakuna hata ndugu yake upande wa baba yake anaongea naye. Mtu alidiriki kumuambia baba yake kama atachoma nyumba yake moto kama ataendelea kunitetea, Mpaka leo ninavyoandika wazazi wake hawaongei naye, sembuse mimi.
Wala usihangaike kujitetea humu ndg yangu ulichokisema ndicho hicho asie amini usimlazimishe kuamini
 
Habari za mchana wapendwa wana JF

Kwanza kabisa natoa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia pumzi na afya njema

Napenda kutoa mrejesho wa uzi wangu ambao niliuleta kwenye hili jukwaa umepita muda kidogo, uzi huo ''Maneno ya kejeli ya mume wangu'' https://www.jamiiforums.com/threads/maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.876139/ na mrejesho wa awali Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu
Nashukuru Mungu kesi imeisha mahakamani ingawa si kwa matarajio ambayo nilikuwa nayo. Nimepewa talaka yangu na mahakama, hii ni baada ya mahakama kujiridhisha kwamba hii ndoa haiwezi kurekebishika. Ndoa tulifunga ya kiislamu na tuliishi pamoja kwa miaka mitano bila kuwa na mtoto, tulifuata taratibu zote za dini katika kutafuta suluhu lakini ilishindikana.

Pamoja na kutoa talaka, mahakama iliamua kumuachia nyumba ambayo nilichangia gharama nyingi tu kwa kuwa eti hapakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kuwa nilichangia. Ifahamike kwamba nyumba nilimkuta nayo lakini hakuwa anaishi hapo maana ilikuwa haijaisha. Baada ya kuoana tulikubaliana kuimalizia kisha kuhamia pale. Kulikuwa na risiti na tuliandika gharama zote za manunuzi na ufundi, lakini kwa makusudi kabisa alizificha kwa hiyo sikuweza kuzipata.

Mimi sikuwa na shida sana na nyumba kwani nilivyoondoka nilimuambia anirudishie gari yangu ambayo niliipata kabla ya ndoa. Gari nilinunua kabla ya ndoa, baada ya kufunga naye ndoa nikampa awe anatumia yeye kwani nilipewa gari la ofisi kutumia. Mwaka 2014 ile gari ikapata ajali, kwani alidumbukia kwenye maji injini ikafa kabisa.

Kwa sababu ilikuwa na bima kubwa waliweza kunilipa milioni 6.6, lakini hizo hela zilipitia kwenye account ya ndugu yangu ambaye nilinunua gari kwenye yadi yake. Hela ililipwa kwenye account ya ndugu yangu kwa sababu nilikuwa sijabadilisha jina. Nilikuwa sina mpango wa kununua gari nyingine ila akawa ananishawishi kweli niongezee hela kununua gari jingine.

Kuna mama mmoja akawa anauza gari yake kwani alikuwa anaenda Marekani kuishi huko, gariilikuwa nzuri sana kwani aliitumia muda mfupi, tukaenda vizuri kuiona hiyo gari na tukakubaliana tutaichukua.

Kwa sababu nilikuwa nasafiri nje ya nchi kikazi niamuambia ndugu yangu ampe hela mume wangu cash, halafu nikampa kama 2.4 ikawa milioni 9. Basi mimi nikiwa nimesafiri alienda kuchukua zile hela kwa ndugu yangu kama nilvyomuagiza na akaenda kulipia gari. Kweli gari ikaja tukawa tunaitumia.

Baada ya miezi kadhaa nikakumbuka suala la kubadili jina ili liwe na jina langu. Sikumoja naagalia kwenye file ili nichukue kadi nikawa siioni. Kumbe kadi alishaenda kuificha anakojua yeye. Kuuliza ananiambia una gari wewe, na huna uthibitisho kwamba nilipokea hela yoyote kutoka kwako na huyo ndugu yako.

Alifanikiwa kuiuza ile gari hivyo kupoteza ushahidi mahakamani ingawa ndugu yangu aliyeniuzia alikuja kutoa ushahidi kama alimpa hela, kosa ni kuwa hakuandikisha na yeye kwani wanamfahamu kuwa ni mume halali wa ndoa. Kwa upande wetu tuliomba ile gari ikamatwe na mahakama lakini hakimu alikataa kwa sababu anazozijua yeye.

Niliambulia kiwanja tu, ambacho ni mali yangu binafsi. Huyu mwanaume toka tumeoana hakuwa na kazi ya kumuingizia kipato cha kutosha kwani alifukuzwa alikokuwa anafanya, na pia alikuwa na kesi kwa hiyo hakuweza kuajiriwa tena.

Rafiki zangu na baadhi ya jamaa wamenishauri nikate rufaa mahakama kuu ila mimi mwenyewe siko tayari maana huyu mwanaume anaweza kunifanyia lolote, ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa RPC wa mkoa fulani zamani ambaye naye ni dhulmati na maisha yake hayaeleweki saizi.

Familia yangu hasa mama amenisihi niachane na hii kesi na niwe na amani kabisa kwani nitapata vingi zaidi ya hivyo alivyochukua. Namshukuru Mungu kwani miaka miwili baada ya kuachana naye (toka October 2015) nimepata baraka nyingi na kupata zaidi ya vile alivyochukua. Naamini Mungu ni mwema na anajua ukweli wote. Nimeamua kumuachia yeye kwani ndio hakimu mkuu, maisha lazima yaendelee na nimejifunza mengi sana kutokana na hili.

Naona amerudiana na yule mchepuko wake kwani nimeshawaona wako pamoja si mara moja.

Niwashukuru sana wa JF kwa michango na ushauri wenu. Ni matumanini yangu kwamba nanyi mmejifunza kupitia hili.

Mbarikiwe sana

Asanteni.
Pole sana ila nikuulize kitu ,uko teyari kuwa mke wa pili?
 
Mwanamke akishakuwa na manenomaneno kama hivo, usimwamini.

Ningekuwa na uwezo ningekupa details za huyu mwanaume then uende mtaa anaoishi ufanye utafiti ungepata mengi zaidi ya haya ninayoongea. Hakuna mtu ambaye yuko mkamilifu kwa hiyo siwezi kusema mimi niko perfect la.
 
Ningekuwa na uwezo ningekupa details za huyu mwanaume then uende mtaa anaoishi ufanye utafiti ungepata mengi zaidi ya haya ninayoongea. Hakuna mtu ambaye yuko mkamilifu kwa hiyo siwezi kusema mimi niko perfect la.
Usitake kujustify mapungufu yako kwa mumeo eti kisa mumeo mtaani sijui "watu wanamuonaje au sjui haongei na nduguze and so on and so forth". Ukijaribu kuongelea matatizo yako na mumewako jitahidi kufocus kwenye suala mlilogombana kati yako wewe na mume wako ili usionekane uko too much defensive. Wanaojua mambo haya watakutilia shaka.
 
Barikiwa pia kwa moyo wa shukrani na hongera pia kwa ushujaa wako ktk kutafuta haki yako japo hujaipata km ulivyotarajia
 
Usitake kujustify mapungufu yako kwa mumeo eti kisa mumeo mtaani sijui "watu wanamuonaje au sjui haongei na nduguze and so on and so forth". Ukijaribu kuongelea matatizo yako na mumewako jitahidi kufocus kwenye suala mlilogombana kati yako wewe na mume wako ili usionekane uko too much defensive. Wanaojua mambo haya watakutilia shaka.
Nilichoongea mimi ndio nakijua kwa hiyo hakuna ulazima kukubali au kukataa. Waache watilie shaka kwani hawajui kilichonitokea.
 
Dhuluma haidumu, Mungu atakuona na utapata vingi kuliko hivyo alivyodhulumu.. gari kitu gani bwana unatoka barabarani tu paaap limebamizwa.. shukuru Mungu una uhai na unaonekana ni mchapa kazi utafanikiwa tu..
 
Back
Top Bottom