Mrejesho: Matusi na kejeli ya mume wangu

Mrejesho: Matusi na kejeli ya mume wangu

Mimi sijamlamu jaji, tatizo kubwa lilikuwa kwenye ushahidi si unajua hizi kesi zilivyo. Lakini hata mchango wangu haukuonekana hata kidogo kama mwanamke, hili nalo linashangaza. Huyu mwanaume ana matatizo ingekuwa inawezekana ningekupa details za huyu jamaa halafu ukafuatilia mtaani utashangaa. Hakuna hata ndugu yake upande wa baba yake anaongea naye. Mtu alidiriki kumuambia baba yake kama atachoma nyumba yake moto kama ataendelea kunitetea, Mpaka leo ninavyoandika wazazi wake hawaongei naye, sembuse mimi.
Kama hiki ulichoandika ndio ukweli mtupu (nafsi ikishuhudie) mama naomba nikupe pole kwa herufi kubwa "POLE". Pole saana Madame,
Kama mtu haongei vizuri na Baba yake mzazi kwa sababu ya utetezi juu yako na naamini baba yake ni mtu timamu basi "aliyekuwa mumeo" ana matatizo saana.

Kwa kuwa hutaki tena kesi, wewe tulia. Kua na amani ya moyo muombe Mungu atakupa mwenza mwingine mwaminifu Madame...
Usiwaone wanaume wote manyang'au. Pole saana aisee
 
Pole sana my dear, endelea na maisha yako angalia mbele zaidi achana na huyo ambaye amekosa mwelekeo wa maisha .Mungu atakupa mara 1000 zaidi ya ulivyopoteza. Pole Mungu akutie nguvu na aendelee kukulinda. Walimwengu hawana maaana kabisa
 
basi sawa ila we nae mambo yako na mmeo baki nayo wewe
 
This is what happens when you use people instead of using things!!! Ndoa ni zaidi ya ku.to.MBA. na & mali jamani!!
 
Mimi sijamlamu jaji, tatizo kubwa lilikuwa kwenye ushahidi si unajua hizi kesi zilivyo. Lakini hata mchango wangu haukuonekana hata kidogo kama mwanamke, hili nalo linashangaza. Huyu mwanaume ana matatizo ingekuwa inawezekana ningekupa details za huyu jamaa halafu ukafuatilia mtaani utashangaa. Hakuna hata ndugu yake upande wa baba yake anaongea naye. Mtu alidiriki kumuambia baba yake kama atachoma nyumba yake moto kama ataendelea kunitetea, Mpaka leo ninavyoandika wazazi wake hawaongei naye, sembuse mimi.
Pole sana dada. Kuna shida sana kwenye sheria zetu kuhusu umiliki wa mali kwa mume na mke. Unless, property iwe kwa jina lako, wakati wa divorce mwanamke unatakiwa ku-prove kwamba umechangia kwenye kupatikana hiyo mali wakati wa ndoa. Vinginevyo mwanamke unapoteza kila kitu.
Tatizo kubwa linakuja, mara nyingi tunaponunua mali kwenye ndoa, huwa tunaacha majina yawe ya waume zetu tukidhani kwamba tupo salama sababu ya ndoa. Siku ikitokea divorce tunapoteza kila kitu kwa kushindwa ku-prove contributions zetu. Kuna wadada wananunua gari kwa pesa zao wanaachia wanaume waandike majina yao. It's ok kum trust mume, ila ni very risk kama ni mume kimeo. Pia, kama mnanunua ardhi wote, ni vizuri kuweka majina yenu wote wawili kwenye umiliki.

Mimi na mume wangu, wote waili tuna uwezo wa kifadha usiotofautiana sana. Mi nilianza kununua gari kabla yake, niliagiza Japan kwa jina langu then baadae naye akanunua lake kwa jina lake. Tumeendelea kuishi hivyo kwenye magari. Mi nilimkuta ana kiwanja ila hajaanza kujenga. Tulipoanza ujenzi, nilimuweka wazi ili nichangie gharama kwa ujenzi, inabidi kiwanja kikae kwa majina yetu yote mawili. Wala hakusita,tukabadilisha majina, na hadi leo tunanunua ardhi kwa majina yetu wote.
 
Asante dada, ni kweli , hata hicho kiwanja kwa bahati tu niliandika jina langu la sivyo ingekuwa shida. All in all maisha yanaendelea na Mungu yu pamoja nami.
 
Kama hiki ulichoandika ndio ukweli mtupu (nafsi ikishuhudie) mama naomba nikupe pole kwa herufi kubwa "POLE". Pole saana Madame,
Kama mtu haongei vizuri na Baba yake mzazi kwa sababu ya utetezi juu yako na naamini baba yake ni mtu timamu basi "aliyekuwa mumeo" ana matatizo saana.

Kwa kuwa hutaki tena kesi, wewe tulia. Kua na amani ya moyo muombe Mungu atakupa mwenza mwingine mwaminifu Madame...
Usiwaone wanaume wote manyang'au. Pole saana aisee
Asante sana, sina sababu ya kudanganya maana hakuna faida yoyote, baba yake hadi alienda kuripoti polisi kuhusu kutishiwa na mwanae. Nashikuru sana familia yake ilikuwa pamoja nami na tunawasiliana vizuri na hawa wazazi kwani hakuna baya tulilotendeana.
 
Pole sana ulipata mwanaume sio mwelewa,je umebatika kupta ujauzito....
 
Habari za mchana wapendwa wana JF

Kwanza kabisa natoa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia pumzi na afya njema

Napenda kutoa mrejesho wa uzi wangu ambao niliuleta kwenye hili jukwaa umepita muda kidogo, uzi huo ''Maneno ya kejeli ya mume wangu'' https://www.jamiiforums.com/threads/maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.876139/ na mrejesho wa awali Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu
Nashukuru Mungu kesi imeisha mahakamani ingawa si kwa matarajio ambayo nilikuwa nayo. Nimepewa talaka yangu na mahakama, hii ni baada ya mahakama kujiridhisha kwamba hii ndoa haiwezi kurekebishika. Ndoa tulifunga ya kiislamu na tuliishi pamoja kwa miaka mitano bila kuwa na mtoto, tulifuata taratibu zote za dini katika kutafuta suluhu lakini ilishindikana.

Pamoja na kutoa talaka, mahakama iliamua kumuachia nyumba ambayo nilichangia gharama nyingi tu kwa kuwa eti hapakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kuwa nilichangia. Ifahamike kwamba nyumba nilimkuta nayo lakini hakuwa anaishi hapo maana ilikuwa haijaisha. Baada ya kuoana tulikubaliana kuimalizia kisha kuhamia pale. Kulikuwa na risiti na tuliandika gharama zote za manunuzi na ufundi, lakini kwa makusudi kabisa alizificha kwa hiyo sikuweza kuzipata.

Mimi sikuwa na shida sana na nyumba kwani nilivyoondoka nilimuambia anirudishie gari yangu ambayo niliipata kabla ya ndoa. Gari nilinunua kabla ya ndoa, baada ya kufunga naye ndoa nikampa awe anatumia yeye kwani nilipewa gari la ofisi kutumia. Mwaka 2014 ile gari ikapata ajali, kwani alidumbukia kwenye maji injini ikafa kabisa.

Kwa sababu ilikuwa na bima kubwa waliweza kunilipa milioni 6.6, lakini hizo hela zilipitia kwenye account ya ndugu yangu ambaye nilinunua gari kwenye yadi yake. Hela ililipwa kwenye account ya ndugu yangu kwa sababu nilikuwa sijabadilisha jina. Nilikuwa sina mpango wa kununua gari nyingine ila akawa ananishawishi kweli niongezee hela kununua gari jingine.

Kuna mama mmoja akawa anauza gari yake kwani alikuwa anaenda Marekani kuishi huko, gariilikuwa nzuri sana kwani aliitumia muda mfupi, tukaenda vizuri kuiona hiyo gari na tukakubaliana tutaichukua.

Kwa sababu nilikuwa nasafiri nje ya nchi kikazi niamuambia ndugu yangu ampe hela mume wangu cash, halafu nikampa kama 2.4 ikawa milioni 9. Basi mimi nikiwa nimesafiri alienda kuchukua zile hela kwa ndugu yangu kama nilvyomuagiza na akaenda kulipia gari. Kweli gari ikaja tukawa tunaitumia.

Baada ya miezi kadhaa nikakumbuka suala la kubadili jina ili liwe na jina langu. Sikumoja naagalia kwenye file ili nichukue kadi nikawa siioni. Kumbe kadi alishaenda kuificha anakojua yeye. Kuuliza ananiambia una gari wewe, na huna uthibitisho kwamba nilipokea hela yoyote kutoka kwako na huyo ndugu yako.

Alifanikiwa kuiuza ile gari hivyo kupoteza ushahidi mahakamani ingawa ndugu yangu aliyeniuzia alikuja kutoa ushahidi kama alimpa hela, kosa ni kuwa hakuandikisha na yeye kwani wanamfahamu kuwa ni mume halali wa ndoa. Kwa upande wetu tuliomba ile gari ikamatwe na mahakama lakini hakimu alikataa kwa sababu anazozijua yeye.

Niliambulia kiwanja tu, ambacho ni mali yangu binafsi. Huyu mwanaume toka tumeoana hakuwa na kazi ya kumuingizia kipato cha kutosha kwani alifukuzwa alikokuwa anafanya, na pia alikuwa na kesi kwa hiyo hakuweza kuajiriwa tena.

Rafiki zangu na baadhi ya jamaa wamenishauri nikate rufaa mahakama kuu ila mimi mwenyewe siko tayari maana huyu mwanaume anaweza kunifanyia lolote, ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa RPC wa mkoa fulani zamani ambaye naye ni dhulmati na maisha yake hayaeleweki saizi.

Familia yangu hasa mama amenisihi niachane na hii kesi na niwe na amani kabisa kwani nitapata vingi zaidi ya hivyo alivyochukua. Namshukuru Mungu kwani miaka miwili baada ya kuachana naye (toka October 2015) nimepata baraka nyingi na kupata zaidi ya vile alivyochukua. Naamini Mungu ni mwema na anajua ukweli wote. Nimeamua kumuachia yeye kwani ndio hakimu mkuu, maisha lazima yaendelee na nimejifunza mengi sana kutokana na hili.

Naona amerudiana na yule mchepuko wake kwani nimeshawaona wako pamoja si mara moja.

Niwashukuru sana wa JF kwa michango na ushauri wenu. Ni matumanini yangu kwamba nanyi mmejifunza kupitia hili.

Mbarikiwe sana

Asanteni.
Siku zote Mungu ndiye mlipaji
 
Back
Top Bottom