MBITIYAZA
JF-Expert Member
- Jan 22, 2017
- 14,947
- 26,084
Pole na hongera kwa hatua uliyochukua,Mungu ndiye mpaji atalipa kwa wakati wake.Anza maisha yako upya mali zinatafutwa.
nimekumiss dada la kubet !lol
Pole na hongera kwa hatua uliyochukua,Mungu ndiye mpaji atalipa kwa wakati wake.Anza maisha yako upya mali zinatafutwa.
Unajibebisha hatari nkasema hata chakula sijui kama kinapita vzr...mara umeshika kidevu cha jamaa mara umemlalia..Zitume nione
[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji134] [emoji134] [emoji134] aha wapi,ulinifananishaUnajibebisha hatari nkasema hata chakula sijui kama kinapita vzr...mara umeshika kidevu cha jamaa mara umemlalia..
Nitume wapi?
Asante sana, hiyoya kumuona ni bahati mbaya tu, huko barabarani si unajua macho hayana pazia. Nina miaka 2 toka tuachane kwa hiyo nakuwa muangalifu sanapole na hongera nyingi nyingi !ninachokuomba kwa sasa ni u move on !yaan hyo ya kusema umemuona mara kadhaa na mchepuko wake inaoenkana na ww unamfatilia ! pia sikushauri kuingia mapema kwenye mahusiano mengine !wanaume haaminiki hawa my dear ! kuwa makini mno tena usijioneshe una uwezo wowote ule !
again hongera kumuepeuka huyu tapeli wa mapenzi ! fumba macho na comments za waja
ha ha haa miss you too weekend hii kuna hela walipumzika kidogo! Ujambo wewe na mumeo?nimekumiss dada la kubet !lol
Hilo la kumpenda hapana aisee, yaani hata siwazi kuhusu yeye.Inaonekana mmeingia kwenye huo uhusiano kwanza au mkiwa mmekomaa sana au mkiwa hamuaminiani vya kutosha maana kuna kama hofu kwenye baadhi ya maamuzi ya pamoja anyway Mungu akujalie maisha mema na inaonekana uko well kidogo ila bado unampenda maana unajua vi detail vyake kidogo move on complitely
[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji134] [emoji134] [emoji134] aha wapi,ulinifananisha
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji87] [emoji87] [emoji87]Sema niweke hapa watu waone
Ok basi songa mbele ila usiache kutoa nafasi kwa mwingine usijekuwa kuwa mpwke daima upweke sio mzuri na uwe na uhakika hajafata good life maana inaonekana kwa mbali vyuma vina tu glisi sio kama wengine hadi fundi anaongeza bei kufunguaHilo la kumpenda hapana aisee, yaani hata siwazi kuhusu yeye.
hahaha asante mkuuOk basi songa mbele ila usiache kutoa nafasi kwa mwingine usijekuwa kuwa mpwke daima upweke sio mzuri na uwe na uhakika hajafata good life maana inaonekana kwa mbali vyuma vina tu glisi sio kama wengine hadi fundi anaongeza bei kufungua
Karibu sanahahaha asante mkuu
ha ha haa miss you too weekend hii kuna hela walipumzika kidogo! Ujambo wewe na mumeo?
Umesema mahakama imetoa taraka, unasemajr umeamua kumuacha wewe??Habari za mchana wapendwa wana JF
Kwanza kabisa natoa ninamshukuru Mungu kwa kunijalia pumzi na afya njema
Napenda kutoa mrejesho wa uzi wangu ambao niliuleta kwenye hili jukwaa umepita muda kidogo, uzi huo ''Maneno ya kejeli ya mume wangu'' https://www.jamiiforums.com/threads/maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.876139/ na mrejesho wa awali Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu
https://www.jamiiforums.com/threads/mrejesho-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.983952/
Nashukuru Mungu kesi imeisha mahakamani ingawa si kwa matarajio ambayo nilikuwa nayo. Nimepewa talaka yangu na mahakama, hii ni baada ya mahakama kujiridhisha kwamba hii ndoa haiwezi kurekebishika. Ndoa tulifunga ya kiislamu na tuliishi pamoja kwa miaka mitano bila kuwa na mtoto, tulifuata taratibu zote za dini katika kutafuta suluhu lakini ilishindikana.
Pamoja na kutoa talaka, mahakama iliamua kumuachia nyumba ambayo nilichangia gharama nyingi tu kwa kuwa eti hapakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kuwa nilichangia. Ifahamike kwamba nyumba nilimkuta nayo lakini hakuwa anaishi hapo maana ilikuwa haijaisha. Baada ya kuoana tulikubaliana kuimalizia kisha kuhamia pale. Kulikuwa na risiti na tuliandika gharama zote za manunuzi na ufundi, lakini kwa makusudi kabisa alizificha kwa hiyo sikuweza kuzipata.
Mimi sikuwa na shida sana na nyumba kwani nilivyoondoka nilimuambia anirudishie gari yangu ambayo niliipata kabla ya ndoa. Gari nilinunua kabla ya ndoa, baada ya kufunga naye ndoa nikampa awe anatumia yeye kwani nilipewa gari la ofisi kutumia. Mwaka 2014 ile gari ikapata ajali, kwani alidumbukia kwenye maji injini ikafa kabisa.
Kwa sababu ilikuwa na bima kubwa waliweza kunilipa milioni 6.6, lakini hizo hela zilipitia kwenye account ya ndugu yangu ambaye nilinunua gari kwenye yadi yake. Hela ililipwa kwenye account ya ndugu yangu kwa sababu nilikuwa sijabadilisha jina. Nilikuwa sina mpango wa kununua gari nyingine ila akawa ananishawishi kweli niongezee hela kununua gari jingine.
Kuna mama mmoja akawa anauza gari yake kwani alikuwa anaenda Marekani kuishi huko, gariilikuwa nzuri sana kwani aliitumia muda mfupi, tukaenda vizuri kuiona hiyo gari na tukakubaliana tutaichukua.
Kwa sababu nilikuwa nasafiri nje ya nchi kikazi niamuambia ndugu yangu ampe hela mume wangu cash, halafu nikampa kama 2.4 ikawa milioni 9. Basi mimi nikiwa nimesafiri alienda kuchukua zile hela kwa ndugu yangu kama nilvyomuagiza na akaenda kulipia gari. Kweli gari ikaja tukawa tunaitumia.
Baada ya miezi kadhaa nikakumbuka suala la kubadili jina ili liwe na jina langu. Sikumoja naagalia kwenye file ili nichukue kadi nikawa siioni. Kumbe kadi alishaenda kuificha anakojua yeye. Kuuliza ananiambia una gari wewe, na huna uthibitisho kwamba nilipokea hela yoyote kutoka kwako na huyo ndugu yako.
Alifanikiwa kuiuza ile gari hivyo kupoteza ushahidi mahakamani ingawa ndugu yangu aliyeniuzia alikuja kutoa ushahidi kama alimpa hela, kosa ni kuwa hakuandikisha na yeye kwani wanamfahamu kuwa ni mume halali wa ndoa. Kwa upande wetu tuliomba ile gari ikamatwe na mahakama lakini hakimu alikataa kwa sababu anazozijua yeye.
Niliambulia kiwanja tu, ambacho ni mali yangu binafsi. Huyu mwanaume toka tumeoana hakuwa na kazi ya kumuingizia kipato cha kutosha kwani alifukuzwa alikokuwa anafanya, na pia alikuwa na kesi kwa hiyo hakuweza kuajiriwa tena.
Rafiki zangu na baadhi ya jamaa wamenishauri nikate rufaa mahakama kuu ila mimi mwenyewe siko tayari maana huyu mwanaume anaweza kunifanyia lolote, ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa RPC wa mkoa fulani zamani ambaye naye ni dhulmati na maisha yake hayaeleweki saizi.
Familia yangu hasa mama amenisihi niachane na hii kesi na niwe na amani kabisa kwani nitapata vingi zaidi ya hivyo alivyochukua. Namshukuru Mungu kwani miaka miwili baada ya kuachana naye (toka October 2015) nimepata baraka nyingi na kupata zaidi ya vile alivyochukua. Naamini Mungu ni mwema na anajua ukweli wote. Nimeamua kumuachia yeye kwani ndio hakimu mkuu, maisha lazima yaendelee na nimejifunza mengi sana kutokana na hili.
Naona amerudiana na yule mchepuko wake kwani nimeshawaona wako pamoja si mara moja.
Niwashukuru sana wa JF kwa michango na ushauri wenu. Ni matumanini yangu kwamba nanyi mmejifunza kupitia hili.
Mbarikiwe sana
Asanteni.
Asante sana, hiyoya kumuona ni bahati mbaya tu, huko barabarani si unajua macho hayana pazia. Nina miaka 2 toka tuachane kwa hiyo nakuwa muangalifu sana