Wana bodi habari,
Mkuu Mlachake alianzisha uzi siku chache huko nyuma na kuwataja baadhi yetu kuwa tuunganishe nguvu ili tutoke na kitu. Wazo lako halikuokotwa na kunguru bali tulilichukua na kulifanyia kazi vizuri. Limeleta mwangwi chanya kwa wote walioitikia.
Baadhi ya Wana-Jf tulijikusanya na kufanikiwa kuanzisha kikundi ili tupate kuanzisha mradi wa ufugaji. Asante sana Mlachake kwa kuwataka wale uliowataja wafanye kitu.Tumefanya. Kwa sasa tuna shamba na tunalipanua zaidi, na tayari mifugo ya kwanza imeshafika shambani.
Changamoto zipo na lazima tuzikabili kiume kabisa, naamini kupitia vikundi tunaweza kufaidi fursa za nchi yetu, na mimi nawashauri wenzangu wenye mitaji midogo waunganishe nguvu ili hatimaye wawe na kitu cha kufanya.
Siku moja tutakualika Mkuu Mlachake ili uje uone matokeo ya wazo lako.