Mrejesho kwa Mlachake

Malila, Mama Joe, Maundumula hii habari ya chatu ni kweli kabisa, nilipokuwa dodoma kipindi cha mvua kubwa hawa chatu wadogo na kenge walikuwa wakisombwa na maji kutoka milimani halafu wanakuja kukwama kwenye miti karibu na maeneo yetu sasa kimbembe wakiwa na njaa usiku hapalaliki maana huwa wanalia kwa milio ya aina mbalimbali ili kuwavuta wanyama.. anaweza kulia kama ndama, mbuzi, mbwa au kucheka kama binadamu lakini kwa mzoefu utaigundua ile sauti yake maana huwa ni kali na nyembamba.. anaweza kulia kwa dk 3 kama ndama, dk 3 kama mbuzi etc..
Njia nyingine kujua uwepo wa nyoka, ukiona ng'ombe wamesimamisha masikio na kutoa miguno basi hapo jua mgeni yupo karibu na eneo la tukio

Njia ya asili ya kukabiliana na nyoka wewe fuga bata maji halafu waache wazurule, nyoka anogopa bata vibaya sana maana huwa anachanwa na ule mdomo kama tambala na kuwafanya wakimbie makazi yao

miaka ya 1990s jamaa wa wizara ya afya walikuwa wakipuliza dawa kwenye nyumba za wafanyakazi wa serikali na walikuwa wanatupia vidonge fulani hivi kwenye vichaka na nyoka wote walikuwa wanakimbia makazi
 
Last edited by a moderator:
Asante Narubungo naona hapa napata ujuzi mbalimbali, mie nilikuwa najua kufuga mbwa ndo suluhisho. Makazi mapya mara nyingi yana matatizo muhimu kusafisha mazingira kwanza, sasa tatizo ukamiliki shamba jirani na mtu hana hata mpango wa kusafisha ni machaka tu yaani inakuwa kazi kweli, ndo maana ni bora kuwa na watu wenye malengo mnafanana la utaingia gharama kuchoma au kufyeka kwa mtu mwingine.
 
Asante Narubungo naona hapa napata ujuzi mbalimbali, mie nilikuwa najua kufuga mbwa ndo suluhisho. Makazi mapya mara nyingi yana matatizo muhimu kusafisha mazingira kwanza, sasa tatizo ukamiliki shamba jirani na mtu hana hata mpango wa kusafisha ni machaka tu yaani inakuwa kazi kweli, ndo maana ni bora kuwa na watu wenye malengo mnafanana la utaingia gharama kuchoma au kufyeka kwa mtu mwingine.

ni vizuri sana kutumia njia za asili kumfukuza nyoka, mbwa huwa anamvutia chatu! mimi nilishawahi kuwa muhanga wa nyoka i.e kuna siku nyoka mweusi aliingia kwenye banda la kuku kama 70 hivi, aligonga kuku kama 20 na wengine kuwarushia mate na kama ujuavyo akili mbovu za kuku wa kisasa walianza kuwadonoa wenzao waliokufa.. siku ya pili nilikuwa na kazi ya kuzika, huwezi amini nilibaki na kuku 6 tu!

kufyeka vichaka ni sawa lakini pia ni lazima utambue kuna mimea/miti huwa inawavutia nyoka mfano muembe, mbohora (passion), mnyaa na mimea fulani huwa inafanana na kitunguu maji kwahiyo usiipande karibu na makazi ya binadamu/mifugo. Epuka kurundika mawe... uwe unachoma mipira ya mataili kweye vichaka bila kusahau kumwaga oil chafu kwenye uzio wa mabanda.
kama unafuga paka usimtese huwa wanatabia ya kukukomoa kwa kukuletea nyoka nyumbani
 
Kama ukifuga kienyeji unaweza usipande majani maalumu kwa chakula chao, lakini ukitaka kufuga kisasa na kwa malengo maalumu ya biashara ni lazima upate mbegu nzuri za majani. mbuzi wanakula aina nyingi za majani miti, hivyo eneo lenye vichaka linafaa sana kwa mbuzi,na ndo maana unaona sehemu kame mbuzi wanaishi.

Mkuranga kuna chatu wale wadogo, ni vizuri kuchoma hilo eneo ili kuwafukuza kama wapo, mimi walinyonga mbuzi 11 hivi wakati naanza. Na kama utafuga huria, inabidi uwe makini, mbuzi wanazurura sana kwa hiyo eka 30 kwa mbuzi huria inabidi usiwe na jirani mkorofi. Vijito vyenye maji ya kudumu kule Mkuranga vina mamba na chatu hukaa kando ya vijito hivyo.

bado vibaka sio wengi inategemea uko Mkuranga ipi. Mhimu, mtafute LAT akupe majina ya mbegu bora za majani ili uoteshe ktk shamba hilo.
Unanitisha na hawa Chatu..Watu wanapona kweli???
 
Back
Top Bottom