CHAKUHAWATA wawageuza Walimu upatu, wagawana Tsh. Milioni 400 za Wanachama

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,402
7,310
Chama cha Kulinda na Kutetea Haki za Walimu Tanzania (CHAKUHAWATA) wanao jiita viongozi wanawagana Tsh Milion 400 za walimu ambazo wametoa ada kwa chama iko.

Chama icho kimeweka ada ya Tsh. 5,000 kwa Wanachama..

Ngazi ya Wilaya wanaweka wakala (anaejiita Mwenyekiti au Katibu msaidizi) yeye huyu kila Mwalimu mmoja anayefanikiwa kumshawishi katika Tsh Elfu 5, yeye anapata 3,000 kwa Mwaka mzima kwa kila aliyejiunga katika eneo lake ili kuongeza nguvu ya kutafuta Walimu.

Baada ya Mwaka mmoja atakuwa anapata Tsh. 2,000, Mwaka wa tatu atakuwa anapata Tsh. Elfu 1,500 kwa kila Mwalimu atakaeweza kumshawishi ajiunge na chama icho na kiasi kinachobaki kinaenda ngazi wanayoita ya Taifa.

Baada ya miaka mitatu wakala wilaya atakua anapata kwa gawio kwa 30% ya fedha zinazokusanywa kwenye wilaya yake.

Chama iko kinagawana fedha kinyume na Katiba yao walioitunga wenyewe toleo la mwaka 2015, nilipomuuliza kiongozi wao ngazi ya Taifa alinijibu kuwa Walimu:

'Tulishàwapunguzia mzigo wa 2% na wasitusumbue kuhusu fedha zinafanya nini hizi ni zetu sisi tuliobuni wazo la kuanzisha chama watupe maua yetu, kama anataka utetezi arudi huko wanakokata 2% ,yeye kama amejiunga na CHAKUHAWATA ajitahidi kufuata utaratibu wa kazi zake asiteleze kukutwa na kosa, sisi hatutunzi fedha, nikamuuliza sio dhumuni la kuanzisha chama, akaniambia habari ndio hiyo sheria zimelala Tanzania, acha sisi tujipatie ridhiki' alisema Twalibu Nyamkunga Katibu Mkuu wa chama iko.

Nilitamfuta Mwenyekiti Sabibi ambaye ni Mwalimu Mstaafu alisema kimsingi wao wakati wanaanzisha chama ilikuwa kupunguza makato, ila ishu ya utetezi hatuna uwezo nayo, tumefanikiwa la kuwapunguzia Wanachama wetu mzigo wa makato ndio maana Walimu hawana shida Elfu 5, hata kama ni kinyume cha Sheria kuanzisha chama kuwa cha kipato badala kuwafanya jukumu la Utetezi.

Nilienda Shule ya Msingi Mwandiga kuongea na baadhi ya Walimu nilikutana na mwalimu Fanikio akiwa na Walimu wenzake walimchagua Fanikio aseme kwa niaba yao alisema tuliwaomba viongozi wetu watupe ufafanuzi fedha za ada zinazokusanywa zinaenda wapi mpaka leo hawajatokea.

Tuliwahi kumuita Mzee Sabibi atueleze fedha zinaenda wapi alituambia kwa sasa ni ngumu kufanya utetezi kwa sababu elfu tano ni fedha ndogo kwa sababu kila wilaya inawakala wa kushawishi wanachama katika elfu tano yeye anachukua elfu Tatu, pia akatueleza wamepokea NOTISI YA KUSITISHA shughuli za chama chetu kwa sababu msajili amesthukia hatufanyi kazi ya Utetezi kwa miaka 7 notisi yenye namba DA.27/380/21/144 Kwa sababu ya ukiukwaji wa Katiba yetu, tunagawana fedha tunazokusanya, kwa kweli tulimuuza maswali mengi na yeye alitujibu bila kufichaficha.

Alisema kimsingi chama kila wilaya kinatakiwa kuwa na uongozi na fedha ili zitoke lazima kuwe na katibu na Mweka Hazina ila kwa sababu ndio tunatafuta Wanachama tukaona kila wilaya tuwe na wakala ambae anajitambulisha Mwenyekiti au Katibu msaidizi.

Baada ya mazungumzo kwa kina walimu waliniuliza mbona nimewauliza sana kuhusu chama chao, nikawajibu nilitaka tupeane uelewa tu.

Kimsingi nilichogundua serikali kupitia msajili ajachukua hatua kusimamia sheria kama ofisi yake ilitoa notisi kuzuia kazi cha chakuhawata mpaka wafuate walioandika katika katiba yao ambayo ni takwa la sheria ya ajira na mahusiano Kazini.

Kwasababu fedha zote zinakusanywa kama ada zinaganywa kuanzia wilayani mpaka ngazi ya Taifa ambayo ni kosa la kisheria rejea sheria ya ajira na mahusiano kazini 2006 na marejeo yake (2019) kifungu cha 461(c).

"Masharti ya Usajili 46(1) -:Mashart ya kusajiliwa chama cha wafanyakazi (a)Ni chama halali cha wafanyakazi (b)Ni umoja usio wa Kipato.

Pia ukisoma Mahitaji ya Katiba kifungu cha 47(1)(a)Kueleza kwamba ni chama kisicho cha kipato

Ndio maana mawakala wengi wa chama cha chakuhawata hataki kujiita makatibu sababu wanajua watatakiwa kuwa na likizo bila malipo sasa wanajua elfu tano haina uwezo wa kumlipa mshahara, ila wameamua kufanya kama chanzo cha kipato katika maisha ya kila siku

Majibu ya CHAKUHAWATA soma hapa - CHAKUHAWATA wajibu tuhuma za viongozi wao kugawana Tsh. Milioni 400 za michango ya Wanachama
 
Naomba kuwauliza nyie walimu:

1. Kule kwenye international forum ikitokea mwaliko ni mwakilishi yupi mtamtuma? kutoka chama gani?

2. Je ILO inatambua kwamba ndani ya nchi yetu kuna chama zaidi ya kimoja kinachotetea maslahi ya watumishi wa kada moja?

3. Serikali imeingia mkataba na vyama vyote hivi au ni geresha?

4. Makato halisi kwa mujibu wa sheria ni yapi? Je ni 2% au ni kiasi chochote mtu anachoamua?

Ufahamu wangu ni mdogo juu ya mambo haya, naomba wadau mnisaidie.
 
CHAKUHAWATA WAWAGEUZA WALIMU UPATU ,WAGAWANA MILION 400

Chama cha Kulinda na Kutetea Haki za Walimu Tanzania (CHAKUHAWATA)wanao jiita viongozi wanawagana Tsh Milion 400 za walimu ambazo wametoa ada kwa chama iko .

Chama icho kimeweka ada ya Tsh 5000 kwa wanachama..

Ngazi ya Wilaya wanaweka wakala(anaejiita Mwenyekiti au Katibu msaidizi) yeye huyu kila mwalimu mmoja anaefanikiwa kumshawishi katika Tsh Elfu 5,yeye anapata 3000 kwa Mwaka mzima kwa kila aliejiunga katika eneo lake ili kuongeza nguvu ya kutafuta walimu ,baada ya Mwaka mmoja atakua anapata Tsh elfu 2000 mwaka wa tatu atakua anapata Ths Elfu 1500 kwa kila mwalimu atakae weza kumshawishi ajiunge na chama icho na kiasi kinachobaki kinaenda ngazi wanayoita ya Taifa .

Baada ya miaka mitatu wakala wilaya atakua anapata kwa gawio kwa 30% ya fedha zinazokusanywa kwenye wilaya yake ..

Chama iko kinagawana fedha kinyume na Katiba yao walioitunga wenyewe toleo la mwaka 2015 ,nilipomuuliza kiongozi wao ngazi ya Taifa alinijibu kuwa Walimu Tulishàwapunguzia mzigo wa 2% na wasitusumbue kuhusu fedha zinafanya nini hizi ni zetu sisi tuliobuni wazo la kuanzisha chama watupe maua yetu ,kama anataka utetezi arudi huko wanakokata 2% ,yeye kama amejiunga na CHAKUHAWATA ajitahidi kufuata utaratibu wa kazi zake asiteleze kukutwa na kosa ,sisi hatutunzi fedha ,nikamuuliza sio dhumuni la kuanzisha chama ,akaniambia habari ndio hiyo sheria zimelala Tanzania, acha sisi tujipatie ridhiki alisema Twalibu Nyamkunga Katibu Mkuu wa chama iko.

Nilitamfuta Mwenyekiti Sabibi ambae ni Mwalimu Mstahafu alisema kimsingi wao wakati wanaanzisha chama ilikua kupunguza makato ,ila ishu ya utetezi hatuna uwezo nayo..tumefanikiwa ilo la kuwapunguzia wanachama wetu mzigo wa makato ndio maana walimu hawana shida Elfu 5 ,hatakama ni kinyume cha sheria kuanzisha chama kuwa cha kipato badala kuwafanya jukumu la Utetezi.

Nilienda shule ya msingi Mwandiga kuongea na baadhi ya walimu ,nilikutana na mwalimu Fanikio akiwa na walimu wenzake walimchagua Fanikio aseme kwa niaba yao alisema tuliwaomba viongozi wetu watupe ufafanuzi fedha za ada zinazokusanywa zinaenda wapi mpaka Leo hawajatokea mpaka Leo.

Tuliwahi kumuita Mzee Sabibi atueleze fedha zinaenda wapi ,alituambia kwa sasa ni ngumu kufanya utetezi kwa sababu elfu tano ni fedha ndogo kwa sababu kila wilaya inawakala wa kushawishi wanachama katika elfu tano yeye anachukua elfu Tatu ,pia akatueleza wamepokea NOTISI YA KUSITISHA shughuli za chama chetu kwa sababu msajili amestukia hatufanyi kazi ya Utetezi kwa miaka 7 notisi yenye namba DA.27/380/21/144 Kwa sababu ya ukiukwaji wa Katiba yetu ,tunagawana fedha tunazokusanya ,kwa kweli tulimuuza maswali mengi na yeye alitujibu bila kufichaficha

Alisema kimsingi chama kila wilaya kinatakiwa kuwa na uongozi ,na fedha ili zitoke lazima kuwe na katibu na Mweka hazina ila kwa sababu ndio tunatafuta wanchama tukaona kila wilaya tuwe na wakala ambae anajitambulisha Mwenyekiti au Katibu msaidizi,

Baada ya mazungumzo kwa kina walimu waliniuliza mbona nimewauliza sana kuhusu chama chao ,nikawajibu nilitaka tupeane uelewa tu.

Kimsingi nilichogundua serikali kupitia msajili ajachukua hatua kusimamia sheria kama ofisi yake ilitoa notisi kuzuia kazi cha chakuhawata mpaka wafuate walioandika katika katiba yao ambayo ni takwa la sheria ya ajira na mahusiano Kazini.

Kwasababu fedha zote zinakusanywa kama ada zinaganywa kuanzia wilayani mpaka ngazi ya Taifa ambayo ni kosa la kisheria rejea sheria ya ajira na mahusiano kazini 2006 na marejeo yake (2019) kifungu cha 461(c)
"Mashart ya Usajili 46(1) -:Mashart ya kusajiliwa chama cha wafanyakazi (a)Ni chama halali cha wafanyakazi (b)Ni umoja usio wa Kipato.

Pia ukisoma Mahitaji ya Katiba kifungu cha 47(1)(a)Kueleza kwamba ni chama kisicho cha kipato

Ndio maana mawakala wengi wa chama cha chakuhawata hataki kujiita makatibu sababu wanajua watatakiwa kuwa na likizo bila malipo sasa wanajua elfu tano haina uwezo wa kumlipa mshahara, ila wameamua kufanya kama chanzo cha kipato katika maisha ya kila siku
Aliyeandika hii habari ni mwalimu?
 
Back
Top Bottom