Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,731
- 40,836
Kuna habari za ndani sana zinazosema kuwa akitarajia muda si mrefu kuwekwa kizimbani aliyekuwa Waziri wa Viwanda Bw. Basil Mramba ameamua kuachilia umiliki wa hoteli yake ya Kibo Palace iliyoko Arusha karibu na cliniki ya AICC. Hili ni mojawapo ya maamuzu ambayo Bw. Mramba ameamua kufanya hasa baada ya uchunguzi wa chini chini ulionesha kuwa kutokana na nafasi yake aliweza kutumia madaraka yake vibaya kwa kujinufaisha.
Kuna dalili pia miradi yake mingine ambayo ameiandikisha kwa majina ya watu wengine ameanza taratibu kuiachilia ili kuharibu/kuficha ushahidi wa yeye au watu wake wa karibu kunufaika.
Vyanzo hivyo vilivyojikita katika kuta mbalimbali za jamhuri yetu vinaonesha pia kuwa Bw. Mramba ambaye ni mzazi mwenza wa mke wa Rais Mkapa ameshiriki kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha biashara za mama huyo zinafanikiwa na zinajikita katika maeneo mbalimbali. Bila ya Mramba inasemwa mama Mkapa asingeweza kujikita kwenye biashara zake.
Endapo Bw. Mramba atasimama kizimbani kama inavyotarajiwa atakuwa ni mtu mwingine aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri katika Muungano kusimamishwa Kizimbani. Kabla yake Waziri Nalaila Kiula alisimamishwa kizimbani kwa makosa ya ubadhirifu lakini baadaye aliweza kushinda rufaa yake na kuachiliwa huru.
Vyanzo hivyo vinaonesha pia kuwa siyo Mramba tu ambaye ameanza kusafisha sahani yake bali pia viongozi na mawaziri (na waliowahi kuwa mawaziri) ambao wameanza kuachilia miradi yao yenye "utata" hasa baada ya kugundulika kuwa Rais Kikwete hatozuia au kuingilia kati uchunguzi wowote dhidi yao au kujaribu kuwakingia kifua kama walivyotarajiwa.