Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Niliwahi kuandika huko nyuma (abt 3 years ago) kuwa huwezi kumjua fisadi kwa kuangalia gari, cheo, hadhi, nyumba anayoishi n.k Ufisadi hauwezi kupimwa kwa namna hiyo. Nilikataa kuwa ufisadi siyo dini, rangi, kabila wala hali ya maisha. Ufisadi NI VITENDO! Mtu hawi fisadi kwa sababu maelfu ya watu wanamuita fisadi; mtu hawi fisadi kwa sababu tunamchukia au anachukiza. Ufisadi ni VITENDO.
Katika hili ninachoona ni maelezo ya mradi wa Dr. Mwinyi. Hilo peke yake haliwezi hata kidogo kumfanya kuwa fisadi.
a. Je, mali hii imetangazwa katika tangazo la mali kwa mujibu wa sheria ya Maadili?
b. Je, inaendana na kipato chake
c. Je, katika kupata kiwanja, mkopo n.k ametumia cheo chake kuathiri mchakato wowote. Kwa mfano, mtu mwingine alikuwa apewe eneo hilo lakini kwa vile yeye ni Waziri akapata upendeleo wa pekee? Au, kama alipata mkopo Benki je vigezo vilivyotumika kumpa yeye mkopo vyaweza kutumika kumpa Mtanzania mwingine (asiye na cheo au ujiko wa kisiasa na nasaba kama wa wake) kumpatia mkopo?
d. Je, ujenzi wake wa hizo apts umezingatia vigezo vyote vya ujenzi? Je eneo hilo zilipojengwa lilikuwa zoned kwa ajili ya makazi ya watu?
So.. ni katika kutafuta majibu ya maswali haya ndipo tunaweza kusema "ufisadi" wa mtu fulani. Kumbuka... UFISADI NI VITENDO!