Mradi wa nyumba za kupanga wa Dr. Hussein Mwinyi Dar

Niliwahi kuandika huko nyuma (abt 3 years ago) kuwa huwezi kumjua fisadi kwa kuangalia gari, cheo, hadhi, nyumba anayoishi n.k Ufisadi hauwezi kupimwa kwa namna hiyo. Nilikataa kuwa ufisadi siyo dini, rangi, kabila wala hali ya maisha. Ufisadi NI VITENDO! Mtu hawi fisadi kwa sababu maelfu ya watu wanamuita fisadi; mtu hawi fisadi kwa sababu tunamchukia au anachukiza. Ufisadi ni VITENDO.

Katika hili ninachoona ni maelezo ya mradi wa Dr. Mwinyi. Hilo peke yake haliwezi hata kidogo kumfanya kuwa fisadi.

a. Je, mali hii imetangazwa katika tangazo la mali kwa mujibu wa sheria ya Maadili?
b. Je, inaendana na kipato chake
c. Je, katika kupata kiwanja, mkopo n.k ametumia cheo chake kuathiri mchakato wowote. Kwa mfano, mtu mwingine alikuwa apewe eneo hilo lakini kwa vile yeye ni Waziri akapata upendeleo wa pekee? Au, kama alipata mkopo Benki je vigezo vilivyotumika kumpa yeye mkopo vyaweza kutumika kumpa Mtanzania mwingine (asiye na cheo au ujiko wa kisiasa na nasaba kama wa wake) kumpatia mkopo?
d. Je, ujenzi wake wa hizo apts umezingatia vigezo vyote vya ujenzi? Je eneo hilo zilipojengwa lilikuwa zoned kwa ajili ya makazi ya watu?

So.. ni katika kutafuta majibu ya maswali haya ndipo tunaweza kusema "ufisadi" wa mtu fulani. Kumbuka... UFISADI NI VITENDO!
 
Mwanakijiji...Huyu muanzishaji wa thread inabidi aje hapa na kuteleza kila kitu kuhusiana na tuhuma hizi,taarifa yake iko nusunusu,haijajitosheleza kiasi cha watu kuanza kumrushia tuhuma Dk Mwinyi kuwa ni fisadi.....2010 hii,tutaona na kusikia mengi kwa kweli
 
Kiranga,
Ningekuwa bongo sasa hivi mbona hii ni kazi ndogo tu? Remember I am Jasusi, no?

Jasusi gani ujasusi wake hauvuki bahari kama majini ya mlingotini :)

Hapa ndipo pa kutuonyesha kwamba wewe ni Jasusi kweli, unavuta uzi underlings wanachambua makabrasha, wanayascan, wanakutupia, tunayaweka hapa mchezo unakwisha.

JF inakuwa JF, si kijiwe cha umbea.
 
Jamani mwacheni bwana mdogo..huyu dogo pamoja na kuwa ametoka familia ya rais mstaafu yupo cool.....sikatai kuwa baba yake alimpa viwanja sehemu nzuri...lakini naye ana akili ....alitumia viwanja vyake kuanza biashara ya kujenga na kupangisha nyumba....na kwa wale msiojuwa biashara hii ..unahitaji tu kuwa na eneo prime...mtaji wa kujenga unapewa na benki...wanabaki na hati...,na wengine wanakutaka malipo ya rent yapitie kwenye akaunti yao...its a good deal ...ukiamua kuuza nyumba unapata pesa maradufu......

Pia kitendo cha hussein kuweka jina lake kwenye mradi ni cha kupongezwa.....kwani angeweza kuandika jina la muhindi pale na msingejuwa....tuache wivu...tuwaunge mkono wenzetu pale wanapofanya mambo kwa uwazi..ili ku encourage ....wengine pia wawe wawazi!!!

Tabia ya kuita kila mtu fisadi inasababisha unafiki kwa viongozi ....tunawajuwa kina msutya wana hadi magorofa JAPAN....kwa ajili ya unafiki kaama huu...tumpongeze kijana amekuwa muwazi na anafanya juhudi kuongeza kile alichopewa na baba yake kama mbegu!!.....NADHANI furaha yenu mngependa kuona anauza na kutawanya ovyo kama teja!!!

kwa wale wenye maeneo sehemu nzuri na hawajui cha kufanyia ni bora wakaomba ushauri tu.....angalieni hata kijitonyama ,mwenge etc magorofa yanapanda ovyo...wengi wanakopa ..si mafisadi wote!
 
Hapana. Wote mafisadi. Baba fisadi, mwana fisadi. Si huyu ndiye aliyepewa tender ya kuingiza magari ya kijeshi wakati wa utawala wa baba yake na kuliletea jeshi magari yasiyofaa kutoka Dubai?

Kweli mkuu Jasusi, baba na mtoto wote ni mafisadi. Enzi ya baba yake ndio mandhali ya fukwe zetu zote kule baharini ziliharibiwa kwa kupewa wafanyabiashara wahindi; ndio wakati huo Ladwa akapewe ufukwe na kujenga Golden Tulip na Subash Patel akajenga Whitesands na Sea Cliff hotels !!

Kote huko walikuwa wanafisadi tu!! Mtoto nae akapewa unaibu waziri wa Afya enzi ya Mkapa chini ya mamaFisadi Anna Abdalla wakala magendo lukuki ya kuagiza dawa kule Medical stores Department!! Hata kama atasema kuwa amekopa hizo billioni kumi hiyo itakuwa ni gelesha tu ukweli ni kwamba huyu kijana ni mchafu!!

Mambo ya kufisadi viwanja huyu Hussein hajaanza leo ; hata pale Kawe alipojenga ile nyumba anayoishi ile sehemu ilikuwa part ya Tanganyika Packers wakafanya uhuni kiwanja kikamegwa na ramani ikabadishwa na watu wa ardhi na yeye akapewa hati ya Kiwanja!!
 
mtoa rushwa na mpokea rushwa wote lile neno alilotumia mwalimu mali manganya?

Hujaonyesha kwamba katoa wala kupokea rushwa lakini.

na kama unasema ni enterprneur tupe faili la biashara zake na kodi anayo lipa na pia uhaki katika kufanya biashara zake dhidi ya mtu mwingine.
A person is presumed innocent until proven guilty, the burden of proof is on the accusing party, not the accused.Ndiyo maana nasema toeni ushahidi.

na kumbuka kuna kisa kilitokea ilipokuwa ofisi ya zambia airways kuchukulia na familia ya kwanza wakati huo, wakati kiutaratibu hiyo sehemu ilitakiwa iwe available kwa applicant wa kwanza, sasa hiyo utasema ni fair play, kuna loliondo gate, kuna dhahabu kusafirishwa nje, kuna uwanja wa kia kukodishwa kwa $1000.00 kwa mwezi kwa miaka 25 nk hadithi ni ndefu hata hatuwezi kuimaliza leo , bali tunakupa viashiria vya mchezo mchafu.
Nilishasema familia hii inanuka rushwa, lakini huwezi kuiongeza hii kama rushwa kwa sababu tu familia hii inanuka rushwa, inabidi uionyeshe hii kama rushwa in it's own right.

Elewa kwamba ninapotaka vitu solid sina nia ya kumtetea Mwinyi per se, nina nia ya kutetea thorough examination hapa JF, tusije kuwa a virtual lynch mob iliyo tayari kum lynch mtu yeyote atakayepigiwa ukelele wa fisadi, ili mradi ana fit profile tu.

Mtoto wa mkubwa na ana ma deal makubwa kubwa, si lazima kila mtoto wa mkubwa mwenye deal kubwa awe fisadi, na kama ni fisadi, hatuitendei haki movement ya anti ufisadi kwa kuja na vikauli visivyo na viwango wala harufu ya credibility, katika kutumia upepo wowote unaovuma kutoka kwa hawa watu kuja kwetu kama uthibitisho wa ufisadi, tutakuwa sisi ndio mafisadi wa kweli, maana tutaifisadi haki ya mtu kuwa "innocent until proven guilty" in our court of JF opinion.
 
Kweli mkuu Jasusi, baba na mtoto wote ni mafisadi. Enzi ya baba yake ndio mandhali ya fukwe zetu zote kule baharini ziliharibiwa kwa kupewa wafanyabiashara wahindi; ndio wakati huo Ladwa akapewe ufukwe na kujenga Golden Tulip na Subash Patel akajenga Whitesands na Sea Cliff hotels !! Kote huko walikuwa wanafisadi tu!! Mtoto nae akapewa unaibu waziri wa Afya enzi ya Mkapa chini ya mamaFisadi Anna Abdalla wakala magendo lukuki ya kuagiza dawa kule Medical stores Department!! Hata kama atasema kuwa amekopa hizo billioni kumi hiyo itakuwa ni gelesha tu ukweli ni kwamba huyu kijana ni mchafu!!

Nasikia baba ni shareholer wa Sea Cliff Hotel
 
Nadhani hapa wote tunamiss point ya mleta hoja!!!

Kama waziri wa jamhuri, na unakuwa na biashara kubwa za namna hii, ile sheria ya JK ya biashara na siasa inakaa vipi hapa??

Nadhani si vibaya mawaziri kuwa na biashara za kusaidia kujikimu maisha, lakini ili la kuwa na top business people tena mawaziri inabidi mjadala ufanyike tuone lipi ni bora.
 
JK ana sheria? Mi nafikiri sheria zinapitishwa na bunge na kutafsiriwa na mahakama. the whole thing was a charade. Sheria yenyewe inasemaje? Ina mamlaka gani? Ina semaje kuhusu Azimio la Zanzibar?

Maana Azimio la Zanzibar linaruhusu biashara na uongozi, sasa JK alikuja na ku repudiate categorically Azimio la Zanzibar?

Maana tusije kutaka ku equate usanii wa JK kuuma na kupuliza, kutoa vitamko visivyo na uzito, vinavyo carry legal contradictions, visivyo katika code of conduct ya ethics za uongozi, na neno "sheria".

Ningependa kuijua kwa undani kama imekataza viongozi wasifanye biashara kabisa na sasa tunarudi kwenye Azimio la Arusha pole pole, maana wako wengi viongozi wenye biashara ati, tuanze kuwasakama wote.
 
Jamani mwacheni bwana mdogo..huyu dogo pamoja na kuwa ametoka familia ya rais mstaafu yupo cool...

This is not a good reason kumuacha "bwana mdogo"..

..sikatai kuwa baba yake alimpa viwanja sehemu nzuri...lakini naye ana akili ....alitumia viwanja vyake kuanza biashara ya kujenga na kupangisha nyumba...

Yaani, baba yake alitumia madaraka yake kumpa mtoto wake viwanja na hilo tunalivumilia kwa sababu aliyepewa ana akili na ametumia viwanja hivyo kuviendeleza?

.na kwa wale msiojuwa biashara hii ..unahitaji tu kuwa na eneo prime...mtaji wa kujenga unapewa na benki...wanabaki na hati...,na wengine wanakutaka malipo ya rent yapitie kwenye akaunti yao...its a good deal ...ukiamua kuuza nyumba unapata pesa maradufu......

can't argue with that.

Pia kitendo cha hussein kuweka jina lake kwenye mradi ni cha kupongezwa.....kwani angeweza kuandika jina la muhindi pale na msingejuwa....tuache wivu...tuwaunge mkono wenzetu pale wanapofanya mambo kwa uwazi..ili ku encourage ....wengine pia wawe wawazi!!!

Kuweka jina lake hakutoshi kuhalalisha jinsi alivyopata; labda yawezekana anatuthubutisha kuwa nimeweka na jina langu..! Uwazi mwingine siyo wa kuonesha uadilifu ni wa kujiamini kuwa hakuna lolote linaloweza kufanywa dhidi yangu.

Tabia ya kuita kila mtu fisadi inasababisha unafiki kwa viongozi ....tunawajuwa kina msutya wana hadi magorofa JAPAN....kwa ajili ya unafiki kaama huu...tumpongeze kijana amekuwa muwazi na anafanya juhudi kuongeza kile alichopewa na baba yake kama mbegu!!.

Hatuwezi kukubali hili kiurahisi hivyo. Sasa leo Kikwete akimmegea Ridhiwani ardhi (kumbuka Rais ndiye anashikilia ardhi kwa niaba ya umma) na akampatia viwanja vizuri mwanae na Ridhiwana akapata watu wa kumsaidia kuviendeleza tusihoji? Yawezekana naye Mkapa ndiyo alitumia hilo hilo kugawa viwanja kwa mke wake kwa sababu naye atakuja kuviendeleza..

Hatutaki watu walioko madarakani watumie nafasi zao kujinufaisha wao wenyewe na familia zao kwa kisingizio cha uwekezaji. Sasa wale ambao baba zao si marais au wakubwa watapata nafasi kweli katika taifa letu. Yawezekana ndio maana watu wengi na wenyewe wanataka kuingia kwenye hii system! Mwisho tutajikuta familia zisizozidi 20 Tanzania zinamilikia asilimia 80 ya utajiri wa taifa letu!

..
..NADHANI furaha yenu mngependa kuona anauza na kutawanya ovyo kama teja!!!

Not really.. nadhani watu wanahitaji kupata majibu ya kutosha tu ili wanapotoa pongezi basi wajue wanazitoa vizuri vinginevyo kina Lukaza na wale waliowekeza kwenye fedha za EPA nao waachiwe kwani wamezitumia vizuri.

kwa wale wenye maeneo sehemu nzuri na hawajui cha kufanyia ni bora wakaomba ushauri tu.....angalieni hata kijitonyama ,mwenge etc magorofa yanapanda ovyo...wengi wanakopa ..si mafisadi wote!

itakuwaje kuwa ni watu wale wale wenye connections zile zile?
 
J
Ningependa kuijua kwa undani kama imekataza viongozi wasifanye biashara kabisa na sasa tunarudi kwenye Azimio la Arusha pole pole, maana wako wengi viongozi wenye biashara ati, tuanze kuwasakama wote.

hiyo sheria haipo! inafikiriwa tu...
 
Hujaonyesha kwamba katoa wala kupokea rushwa lakini.
rushwa ina muonekana mwingi, mojawapo ni kutumia madaraka yako. wewe mwenyewe umesema tatizo ni wafanyakazi wa ardhi kuwa tetemekea wakubwa, sasa hapa inaonyesha cheo/jini limetumika ili kupata hicho alicho kipa

A person is presumed innocent until proven guilty, the burden of proof is on the accusing party, not the accused.Ndiyo maana nasema toeni ushahidi.
circurmstatial evidence ina mu-implicate, kupata nyumba/kiwanja ambapo wengine ni vigumu au haiwezekani kupata na tunasema watu wote ni sawa, labda uniambie leo hii hii ni kauli tu ya kisiasa na haina ukweli wowote.

Pili takukuru wakikufuata huwa wanaanza na circumstatial evidence ili ku-build up the case na hii pia inaendana na Sheria za Mali za Viongozi ilikuona kile kilicho au kuzaniwa kupatika kwa njia zisizo.
hata sheria za kodi na money koundering zinaweza kukazia jambo.

Nilishasema familia hii inanuka rushwa, lakini huwezi kuiongeza hii kama rushwa kwa sababu tu familia hii inanuka rushwa, inabidi uionyeshe hii kama rushwa in it's own right.

Elewa kwamba ninapotaka vitu solid sina nia ya kumtetea Mwinyi per se, nina nia ya kutetea thorough examination hapa JF, tusije kuwa a virtual lynch mob iliyo tayari kum lynch mtu yeyote atakayepigiwa ukelele wa fisadi, ili mradi ana fit profile tu.

Mtoto wa mkubwa na ana ma deal makubwa kubwa, si lazima kila mtoto wa mkubwa mwenye deal kubwa awe fisadi, na kama ni fisadi, hatuitendei haki movement ya anti ufisadi kwa kuja na vikauli visivyo na viwango wala harufu ya credibility, katika kutumia upepo wowote unaovuma kutoka kwa hawa watu kuja kwetu kama uthibitisho wa ufisadi, tutakuwa sisi ndio mafisadi wa kweli, maana tutaifisadi haki ya mtu kuwa "innocent until proven guilty" in our court of JF opinion.
nimeisha kupa msemo wa kiislamu haramu huza haramu., sasa chanzo cha mtaji ni batili je kinacho zaliwa hapo si batili? wewe ni corporate lawyer nafikiri unaweza kunielezea vizuri kwenye huu msemo.
 
nimeisha kupa msemo wa kiislamu haramu huza haramu., sasa chanzo cha mtaji ni batili je kinacho zaliwa hapo si batili? wewe ni corporate lawyer nafikiri unaweza kunielezea vizuri kwenye huu msemo.

kinachofanyika sasa hivi ni kuhalalisha fedha haramu kwa kuingiza kwenye biashara halali. (haihusianina masuala ya mwinyi), inakuwa pale mtu anaiba bilioni 1 ya fedha za umma halafu anaenda kujenga nyumba za kupanga, sasa akiisha jenga nyumba ya kupanga wale waliobiwa (wananchi) wanajipanga kutoa pongezi kwa jinsi alivyowekeza. Hawajui kwa kufanya hivyo wamehalalisha ule wizi na hivyo kuwafanya watu wengine nao watumie mbinu hiyo hiyo.

Inakuwa ni sawa na mtu ambaye anakuja na kukuibia jogoo lako, halafu wewe unakosa kitoweo halafu anarudi anakuuzia jogoo aliyekaangwa vizuri na limau kibao, kwa bei ya juu kuliko wewe mwenyewe ulivyotarajia. Kwa vile unaona amechukua muda kumkaanga jogoo yule na kumtia limau na mdalasini basi unafurahia kununua kitoweo hicho japo wajua jogoo ni lako!
 
nimeisha kupa msemo wa kiislamu haramu huza haramu., sasa chanzo cha mtaji ni batili je kinacho zaliwa hapo si batili? wewe ni corporate lawyer nafikiri unaweza kunielezea vizuri kwenye huu msemo.

Chanzo cha mtaji kipi batili? Unaweza kukitaja na ubatili wake uko wapi? So far kila kitu ni speculation tu, nimempa Jasusi challenge kutetea speculations zake (mind you, si kuthibitisha, kutetea tu beyond reasonable doubt, anaanza kutoa udhuru kwamba hayupo tanzania)

rushwa ina muonekana mwingi, mojawapo ni kutumia madaraka yako. wewe mwenyewe umesema tatizo ni wafanyakazi wa ardhi kuwa tetemekea wakubwa, sasa hapa inaonyesha cheo/jini limetumika ili kupata hicho alicho kipa.

As far as I am concerned, kila mtanzania anatakiwa kutetemekewa kiaina akiingia katika ofisi za serikali kuomba huduma, ardhi included. Sasa huyu mkuu akiingia sehemu wakamtetemekea wenyewe - kitu ambacho ni haki yake kama mtanzania- mtasema kukubali swift service ni rushwa? Mimi naona tuwapigie kelele ardhi kwamba kwa nini hawaharakishi vitu kwa watu wote kirahisi hivi, na kama kuna swala la fairnmess, swala hili liko katika authorities. Now ile story (naiita story bado, haina spine) ya Jasusi kwamba baba mwinyi alikwapua mighorofa na kumpa mwanawe, hii story ina uzito, na kama kuna mtu anaweza kuichunguza hii na kuibuka na kitu hapa ndipo moto unapoweza kuwakia.

circurmstatial evidence ina mu-implicate, kupata nyumba/kiwanja ambapo wengine ni vigumu au haiwezekani kupata na tunasema watu wote ni sawa, labda uniambie leo hii hii ni kauli tu ya kisiasa na haina ukweli wowote..

Circumstantial evidence inaweza kuku implicate wewe uko Malibu sasa hivi unatanua na mke wa mtu. We should rise above speculative "circumstantial evidence". Leteni vitu solid hapa.

Pili takukuru wakikufuata huwa wanaanza na circumstatial evidence ili ku-build up the case na hii pia inaendana na Sheria za Mali za Viongozi ilikuona kile kilicho au kuzaniwa kupatika kwa njia zisizo.
hata sheria za kodi na money koundering zinaweza kukazia jambo.

Ili Takukuru wakufuate inabidi kuwe na "reasonable doubt", sasa huyu jamaa mnashindwa hata kumuwekea "reasonable doubt". Ndiyo mana nikasema mnajiweka katika position ya mtu kuwa dismiss kirahisi kwamba mna wivu, au ni wapinzania wa kisiasa.

Leteni vitu concrete hapa.
 
I understand some of you are suprised at this level dough. How do you know he is the sole shareholder? Maybe he is representing someone else. And if it is him how do you know ana assets gani zakupata collateral? Mashamba, investments nyingine? Huyu mtu kaja na thread isiyo na malelezo yoyote na nyie mnaleta ujamaa hapa na kumsupport... Being rich does not make anyone mchafu and yes there are people worth several million dollars so what? Nchi ikiwa na matatizo ndio kila mtu awe maskini? Toeni sababu au muacheni mwinyi apete tuu. SO you think he stole 10billion and is using it to build apartments.. Are you insane.lol No one invests using their own money to do things like that.. It is almost always the bank's money.. (and nasema haya as a corporate lawyer often dealing with these types of arrangements and furthermore I myself do modest investment in real estate) So swala la watu walizoea mishara ha laki 5 ama 1.5m kuanza shangaa mtu anacheza na 10 million dollars (it doesnt mean hizo hela anakula.. it is an investment portfolio sio sawa na mshahara..) MwanaFA umepatia kusema kuwa kuna watu wana some kind of class-beef. I am not a fan of social strata myself but it is a natural consequence of human interaction a special in the Capitalistic world.

I myself plan to retire with around 100 million dollars..does that mean I have ufisadi in my plans..NO way. Its just personal ambition and vision. Mtu asi invest, fisadi..

Nashukuru mkuu tena umesema wewe una shugulika na haya mambo, this eductaion is what forum needs, people need to be eductaed and to change their mind. Katika kufanya hivyo wala haihitaji matusi, ulichaondika hapa kina impact kubwa ya kuonyesha mjibu maada ni professional na anayesoma anajifunza jambo fulani. we need your eductaion even more than this.

Sasa hivi kuna msukumo wa watu kupima viwanja vyao na ukipata hati ni mmoja ya vigezo vinzvyokuwezesha kupata mikopo. we may have many questions regarding this project. However how clean it is we can not avoid questions!

Jamani mwacheni bwana mdogo..huyu dogo pamoja na kuwa ametoka familia ya rais mstaafu yupo cool.....sikatai kuwa baba yake alimpa viwanja sehemu nzuri...lakini naye ana akili ....alitumia viwanja vyake kuanza biashara ya kujenga na kupangisha nyumba....na kwa wale msiojuwa biashara hii ..unahitaji tu kuwa na eneo prime...mtaji wa kujenga unapewa na benki...wanabaki na hati...,na wengine wanakutaka malipo ya rent yapitie kwenye akaunti yao...its a good deal ...ukiamua kuuza nyumba unapata pesa maradufu......

Pia kitendo cha hussein kuweka jina lake kwenye mradi ni cha kupongezwa.....kwani angeweza kuandika jina la muhindi pale na msingejuwa....tuache wivu...tuwaunge mkono wenzetu pale wanapofanya mambo kwa uwazi..ili ku encourage ....wengine pia wawe wawazi!!!

Tabia ya kuita kila mtu fisadi inasababisha unafiki kwa viongozi ....tunawajuwa kina msutya wana hadi magorofa JAPAN....kwa ajili ya unafiki kaama huu...tumpongeze kijana amekuwa muwazi na anafanya juhudi kuongeza kile alichopewa na baba yake kama mbegu!!.....NADHANI furaha yenu mngependa kuona anauza na kutawanya ovyo kama teja!!!

kwa wale wenye maeneo sehemu nzuri na hawajui cha kufanyia ni bora wakaomba ushauri tu.....angalieni hata kijitonyama ,mwenge etc magorofa yanapanda ovyo...wengi wanakopa ..si mafisadi wote!

Mkuu uko sahihi rejea majibu ya MKJJ hapo juu, kuna vitu hatuwezi kukwepa kuuliza! tuna experience , tumepitia kwenye EPA,Rich, Bot, Loliondo, mke wa Mwinyi na zile tuhuma, nikisema kila scaadal nchi hii, zinamweka kila kiongozi kikaangoni.

Kuna watu wanapeleka fedha nje, hakuna aliyeamini kuwa Chenge ana vijisent nje, watu wanapoona issue kama hizi ambazo wengine ni ndoto+ hiyo experience lazima watu waulize!

Kuuliza huku bado kunatupa kutafakari tulipo na tunaenda wapi, kuuliza huku huku ndiko tulikowapata wachafu nchi hii, kuuliza huku huku ndiko kunawaamsha watu waseme ukweli wanaoujua!

Sijaona kama kuuliza kumekuwa kosa la jinai tena hasa unapomuuliza kiongozi wa umma! Lazima pia tufike mahali tukubali dhana ya kuwa kiongozi wa umma! ndio maana Tanzania siku zote tuna reference point, hakuongoza MOBUTU nchi hii kiasi cha kuwa wanaokuja wote wawe na mind ya Mobutu, tuliongozwa na Nyerere na tunajua alikuwaje na hizi issue za ubinafsi!

Kweli watu imefikia hatua ya kusema 'fisadi alikuwa baba' fedha zikienda kwa mtoto ni clean? kwa sababu anawekeza Tanzania, Mkapa mbona basi naye wazo lake lilikuwa zuri tu la kuchukua kiwira si angeleta ajira?

Kiongozi gani leo ataandika proposal ya kwenda kwenye mabenki yatoe mikopo ya kujenga mashule? na wananchi walipe kwa kiasi kidogo kabisa? nani leo ataandika proposal serikalini kuwa zijengwe nyumba za bei nafuu kabisa ambazo mtu anaweza kulipa sh.300 kwa siku kama mabibo hostel?

Nani ataandika proposal na kuwaaminisha benki kuwa tunahitaji madampo? na kila ayemwaga uchafu alipie kiasi iadogo tuwalipe benki? nani ataandika poposal ya kupata mkopo wa kununua madawati ya shule ya msingiTanzania nzima na kila mtoto achangie sh.50 kwa mwezi mpaka anamaliza darasa la saba?

Hizi benki tusipozitumia kwa ajili ya kuleta maendeleao kwa wananchi kwa nia ya kuwashirikisha wananchi kulipa mikopo kwa bei nafuu nani atawaisaidia? mikopo hii inakuwa ya wachache wenye fedha?

Nani anawaza leo kuwawezesha wachimba madini wadogo kwa njia ya mikopo, ili wajikwamue waajiri watanzania badala ya wahandisi wetu kuishia kuwa second hand engineers in minings?

Kiongozi gani atasema serikali inachukua mkopo kama mdhamini tunahitaji vijana waliomaliza mechanical engineering, computer engineering kufanya innovation fulani ambazo kwazo tutaokoa fedha nyingi na tutazitumia humu humu ndani?

Mabenki hayawezi yakafadhili uchimbaji wa chuma?, badala ya kupoteza hela kununua kila chuma nje, zikwemo nondo? wakati chuma ipo imelala na makaa ya kuyeyushia yapo?

Hizi benki zisaidie kuleta maendeleao kwa raia, sipingi haya ya binafsi lakini viongozi wakianza haya, tujue hakuna kiongozi atakayewaza niliyoyaandika ndio nchi inabaki kama vile ni NYAMA FULANI IKO SAKAFUNI NA KILA RAIA ANAINIMEGA KUTOKANA NA NGUVU ZAKE!!

Leaders should think beyond that ! they should have a sense of thinking more about people!
 
kinachofanyika sasa hivi ni kuhalalisha fedha haramu kwa kuingiza kwenye biashara halali. (haihusianina masuala ya mwinyi), inakuwa pale mtu anaiba bilioni 1 ya fedha za umma halafu anaenda kujenga nyumba za kupanga, sasa akiisha jenga nyumba ya kupanga wale waliobiwa (wananchi) wanajipanga kutoa pongezi kwa jinsi alivyowekeza. Hawajui kwa kufanya hivyo wamehalalisha ule wizi na hivyo kuwafanya watu wengine nao watumie mbinu hiyo hiyo.

Inakuwa ni sawa na mtu ambaye anakuja na kukuibia jogoo lako, halafu wewe unakosa kitoweo halafu anarudi anakuuzia jogoo aliyekaangwa vizuri na limau kibao, kwa bei ya juu kuliko wewe mwenyewe ulivyotarajia. Kwa vile unaona amechukua muda kumkaanga jogoo yule na kumtia limau na mdalasini basi unafurahia kununua kitoweo hicho japo wajua jogoo ni lako!

Fine,

Lakini tuonyeshe link basi, na tusiishie hapo, tuwaandike magazetini, tususie biashara zao na za wote wanaofanya nao biashara, na zaidi ya yote tuwapeleke mahakamani na kutowapigia kura tena .

Lakini hatuwezi hata kuanza kuwandika magazetini kama hatuna data za kuonyesha links, kwani watatupiga suits za mabilioni ya fedha.

I am only adhering to a higher standard of conduct. Wenzetu hata wakikujua wazi unawaibia, au unafanya uhalifu, bila kuwa na concrete evidence hawakushtui ng'oo.

Hata kama huyu Mwinyi ni fisadi kweli, kitu ambacho uwezekano wacho siupingi kama nilivyosema mwanzo - hizi habari kwa kiduchu kiduchu zinaweza kuwa zinam tip off, ajiandae kuharibu ushahidi, ku forge documents, kuhonga watu, ili kesho keshokutwa mkipata ari na uwezo wa kumshitaki mnakuta hamna kitu.

Tusitake kufanya zeal yetu iharibu the serious anti-corruptiopn war.
 
Kiranga,

Nimesema siko Tanzania kwa sasa kwa sababu nilidhani watu wataniuliza ushahidi ambao najua unaweza kupatikana kirahisi . Lakini kama ni kutetea speculations zangu, hilo jumba la Mwinyi pale Seaview nimeshaonyeshwa mara nyingi, na nijuavyo lilikuwa mali ya National Housing kabla ya Mwinyi kuamua kuwarudishia wahindi nyumba zao zilizochukuliwa wakati wa utaifishaji. Nimekaa Upanga kuanzia mwaka 1973 na najua pale hakukuwa na open space, kama alivyosema August. Kwa hiyo ni wazi Daktari alipewa hilo jengo na baba yake. Asingeweza kulinunua kwa sababu wakati baba yake anakuwa rais mwaka uliofuata alienda kusomea udaktari Uarabuni. Unless mtu aniambie kuwa alirudi na mabilioni ya dinars kutoka kwa Waarabu, highly unlikely. Kwa hiyo kama ni kutetea speculations zangu I stand to be counted..

Hata jengo lake jingine pale Mikocheni kuna wazalendo walinionyesha.
 
Sasa Mkuu Jasusi ushahidi unaweza kupatikana kirahisi kwa nini tunaandikia mate wakati wino upo?

Kwa nini watu wasifanye kweli zaidi ya kutoa ghani na tungo hapa JF ambazo sanasana zinamshtua bwana Mwinyi tu?

Kwa nini Majasusi msitutoe kimasomaso na sie tukawa kama kina Taiwan huko, ambako ma ex presidente wanashitakiwa na kufungwa, seuze watoto zao?

Tunasubiri nini na ushahidi unapatikana "kirahisi"?
 
Kiranga,​

Nimesema siko Tanzania kwa sasa kwa sababu nilidhani watu wataniuliza ushahidi ambao najua unaweza kupatikana kirahisi . Lakini kama ni kutetea speculations zangu, hilo jumba la Mwinyi pale Seaview nimeshaonyeshwa mara nyingi, na nijuavyo lilikuwa mali ya National Housing kabla ya Mwinyi kuamua kuwarudishia wahindi nyumba zao zilizochukuliwa wakati wa utaifishaji. Nimekaa Upanga kuanzia mwaka 1973 na najua pale hakukuwa na open space, kama alivyosema August. Kwa hiyo ni wazi Daktari alipewa hilo jengo na baba yake. Asingeweza kulinunua kwa sababu wakati baba yake anakuwa rais mwaka uliofuata alienda kusomea udaktari Uarabuni. Unless mtu aniambie kuwa alirudi na mabilioni ya dinars kutoka kwa Waarabu, highly unlikely. Kwa hiyo kama ni kutetea speculations zangu I stand to be counted..​

Hata jengo lake jingine pale Mikocheni kuna wazalendo walinionyesha.​
kama Ujasusi wako kusema Dr. Mwinyi kasomea Uarabuni..basi wewe si Jasusi ni Unafanana na Shigongo..kwa Udaku..km ukisema hujui huwezi kuitwa Mjinga...!!!
 
kama Ujasusi wako kusema Dr. Mwinyi kasomea Uarabuni..basi wewe si Jasusi ni Unafanana na Shigongo..kwa Udaku..km ukisema hujui huwezi kuitwa Mjinga...!!!

Wewe ushaambiwa ushahidi unapatikana "kirahisi", kama vile Lira inavyoweza kuchanganywa na Dinar na Turkey ikaitwa "Uarabuni".
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom