Mradi wa Gesi Mtwara-Dar ni "White Elephant"?

Mradi wa Gesi Mtwara-Dar ni "White Elephant"?

Kumbe wewe unapenda porojo na mizaha. Yaani hujui kuwa kuna mgao mkali sana wa umeme?

hakuna mgao,kuna tatizo la miundombinu ya kusambazia umeme,tunazalisha megawtt 1500 matumiz yetu megawatt 950
 
Mkuu, naona umeandika tu bila ushahidi. Unaishi Mkoa gani Tanzania ambako kuna mgawo wa umeme?
Dodoma kuna mgawo wa kufa mtu!!! Kuanzia wiki iliyopita umeme ni shida!!!
 
Tanzania hatuna mgawo wa umeme. Ni wapi kuna huo mgawo? Sisi huku Songea hatuna kabisa ijapokuwa bado tunatumia umeme wa majenereta

wakati mwingine ni vyema kuweka pembeni mahaba uliyonayo kwa chama tawala. Unatumia umeme wa majenereta halafu unasema hakuna mgao!??? I see ww ni zaidi ya nyumbu
 
...@ Lizaboni we gamba kwenye ukweli sema ukweli achana na mahaba yako ya chama! Alafu mijitu kama nyinyi ndy mnakufa na tai shingoni nyambaf
 
Hata kama una cheo serikalini ndugu ni bora some time ukawa na na mchango utakaosaidia nchi isonge mbele. Mikoa karibu yote Kuna mgao. Nilikua Iringa juzi ni mgao, Leo nipo Tukuyu Mbeya toka asubuhi ya saa 1 hakuna umeme. Tuache maigizo kwenye mambo ya msingi jamani

Nimekaa Sumbawanga wiki nzima bila mbao
 
Juhudi za kuondoa tatizo la umeme zinaonekana kuwa ngumu kila kukicha, mvua nyingi zinazoendelea kunyesha nchi nzima zimeshindwa kupunguza mgao wa umeme, Mradi wa gesi Mtwara hadi Dar es Salaam ulitoa matumaini ya kumaliza tatizo la umeme nchi surprisingly tatizo linaendelea, mradi uliogharimu taifa ma billioni ya dola, huwa najiuliza hizi pesa za huu mradi zingetumika kujenga na kuzalisha umeme huko huko mtwara then ukaingia kwenye grid ya taifa manufaa yangekuwa makubwa kiasi gani?

Naomba kuwasilisha.

Ni vema kufahamu taratibu za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kupata majibu ya maswali uliyouliza.

Uzalishaji

Umeme una njia mbalimbali za kuzalishwa.

Njia ya kwanza ni kuzalisha umeme kwa kutumia maji ya maporomoko (hydro)- kama kule Kidatu, Hale, Nyumba ya Mungu. Hii ni njia nafuu kuliko njia zote za kuzalisha umeme

Njia ya pili ni kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta- hii ni njia ghali kutokana na bei za mafuta kuwa juu

Njia ya Tatu ni kuzalisha umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe- hii ni njia nafuu pia lakini ina athari kwa mazingira

Njia ya nne ni kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia- hii ni njia nafuu na haina athari kwa mazingira

Njia ya tano/sita ni kuzalisha umeme kwa kutumia upepo, jua, joto ardhi (geothermal)

Narejea kusisitiza kati ya njia zooote hizo, njia ambayo inazalisha umeme kwa bei ya chiiini kabisa ni MAJI. Faida za umeme wa maji ni umeme unaozalishwa unakuwa wa bei nafuu sana. Changamoto za kutegemea maji kuzalisha umeme ni inapotokea ukame, basi uzalishaji unaporomoka. Changamoto nyingine ni kwamba uwekezaji kwenye kujenga mitambo ya kuzalisha umeme ni mkubwa. Umeme ambao Waziri wa Nishati amesema Tanzania itaununua kutoka Ethiopia kwa bei nafuu ni umeme unaozalishwa kwa MAJI. Gharama halisi ya umeme wa maji ni Cent za Kimarekani 4 kwa unit, gharama za kuusafirisha cent za kimarekani 2 unit, faida ya kuuza ni cent 1.4 kwa unit....ndio maana jumla ya gharama ya kununua umeme huo wa Ethiopia ni Cent 7.4 kwa unit. Bei hiyo ya kununua umeme wa Ethiopia ipo chini kabisa kushinda hata bei ya umeme unaozalishwa hapa nchini kwa kutumia mafuta ambao unauzwa kwa kati ya cent za kimarekani 40-60 kwa unit, au umeme unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia unaogharimu cent za kimarekani kati ya 8-12 kwa unit.

Manelezu, umeuliza swali zuri-----bomba la gesi ni white elephant? Jibu ni hapana. Bomba lile linatumika kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo gesi hiyo ikishafika Dar inatumika kuzalisha umeme pale Kinyerezi. Kwa sasa tanesco imeshajenga kinu kimoja cha kuzalisha umeme wa MW 150 pale Kinyerezi ambacho kilizunduliwa mwezi Oktoba angalia Tanzania inaugurates Kinyerezi I gas power plant | ESI-Africa.com

Mradi wa pili wa Kinyerezi utaanza kujengwa muda si mrefu na kampuni ya Somitomo ya Japan Construction at the Kinyerezi III power plant

Awamu ya tatu na ya nne ya Kinyerezi itajengwa pia mwakani na makampuni kutoka China.

Miradi yote hii itakapokamilika, ndipo gesi inayosafirishwa kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam itatumika zaidi kuzalisha umeme wa kutosha utakaoingizwa kwenye gridi ya taifa

Lakini ni vizuri kutambua.....kuzalisha umeme pale kinyerezi peke yake haitoshi........umeme ukishazalishwa ni lazima uingizwe kwenye gridi ya taifa na kusafirishwa kwenda sehemu mbalimbali. Kwa msingi huo, TANESCO ina miradi ya usafirishaji wa umeme katika sehemu mbalimbali nchini....moja ya miradi mipya ya usambazaji ni ule unaotoka Dar-es-Salaam- chalinze- Same-Tanga- Moshi- Arusha........(North East Transmission Line)........ umeme utakaozalishwa Kinyerezi utasafirishwa katika njia hiyo na kuteremeshwa maeneo yote hayo niliyotaja. Vilevile, upo mradi wa North West Transmission Line unaokwenda hadi Kigoma

Sasa umeme huo ukishasafirishwa kwenda sehemu mbalimbali, hatua ya mwisho ni distribution kwa watumiaji ambao ni wananchi, maofisi, viwanda nk

KWahiyo ndugu yangu vuta subira....miradi yote hii itakapokamilika ndani ya miezi 24 matatizo ya umeme yatakuwa ni historia
 
Mkuu, naona umeandika tu bila ushahidi. Unaishi Mkoa gani Tanzania ambako kuna mgawo wa umeme?

Yaani wewe ndio Wa kuulizwa unaishi nchi gani sio ataa mkoa gani.yaani ujui Arusha mwezi Wa tano huu umeme aujilikani utawaka saa ngapi au utazima saa gani.ni shida zaidi ya huo mgao.Mwanza .Lindi.Kilimanjaro.nikwamba tuko kimya atujui ataa pakulalamikia.
 
Ni vema kufahamu taratibu za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kupata majibu ya maswali uliyouliza.

Uzalishaji

Umeme una njia mbalimbali za kuzalishwa.

Njia ya kwanza ni kuzalisha umeme kwa kutumia maji ya maporomoko (hydro)- kama kule Kidatu, Hale, Nyumba ya Mungu. Hii ni njia nafuu kuliko njia zote za kuzalisha umeme

Njia ya pili ni kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta- hii ni njia ghali kutokana na bei za mafuta kuwa juu

Njia ya Tatu ni kuzalisha umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe- hii ni njia nafuu pia lakini ina athari kwa mazingira

Njia ya nne ni kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia- hii ni njia nafuu na haina athari kwa mazingira

Njia ya tano/sita ni kuzalisha umeme kwa kutumia upepo, jua, joto ardhi (geothermal)

Narejea kusisitiza kati ya njia zooote hizo, njia ambayo inazalisha umeme kwa bei ya chiiini kabisa ni MAJI. Faida za umeme wa maji ni umeme unaozalishwa unakuwa wa bei nafuu sana. Changamoto za kutegemea maji kuzalisha umeme ni inapotokea ukame, basi uzalishaji unaporomoka. Changamoto nyingine ni kwamba uwekezaji kwenye kujenga mitambo ya kuzalisha umeme ni mkubwa. Umeme ambao Waziri wa Nishati amesema Tanzania itaununua kutoka Ethiopia kwa bei nafuu ni umeme unaozalishwa kwa MAJI. Gharama halisi ya umeme wa maji ni Cent za Kimarekani 4 kwa unit, gharama za kuusafirisha cent za kimarekani 2 unit, faida ya kuuza ni cent 1.4 kwa unit....ndio maana jumla ya gharama ya kununua umeme huo wa Ethiopia ni Cent .4 kwa unit. Bei hiyo ya kununua umeme wa Ethiopia ipo chini kabisa kushinda hata bei ya umeme unaozalishwa hapa nchini kwa kutumia mafuta ambao unauzwa kwa kati ya cent za kimarekani 40-60 kwa unit, au umeme unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia unaogharimu cent za kimarekani kati ya 8-12 kwa unit.

Manelezu, umeuliza swali zuri-----bomba la gesi ni white elephant? Jibu ni hapana. Bomba lile linatumika kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo gesi hiyo ikishafika Dar inatumika kuzalisha umeme pale Kinyerezi. Kwa sasa tanesco imeshajenga kinu kimoja cha kuzalisha umeme wa MW 150 pale Kinyerezi ambacho kilizunduliwa mwezi Oktoba angalia Tanzania inaugurates Kinyerezi I gas power plant | ESI-Africa.com

Mradi wa pili wa Kinyerezi utaanza kujengwa muda si mrefu na kampuni ya Somitomo ya Japan Construction at the Kinyerezi III power plant

Awamu ya tatu na ya nne ya Kinyerezi itajengwa pia mwakani na makampuni kutoka China.

Miradi yote hii itakapokamilika, ndipo gesi inayosafirishwa kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam itatumika zaidi kuzalisha umeme wa kutosha utakaoingizwa kwenye gridi ya taifa

Lakini ni vizuri kutambua.....kuzalisha umeme pale kinyerezi peke yake haitoshi........umeme ukishazalishwa ni lazima uingizwe kwenye gridi ya taifa na kusafirishwa kwenda sehemu mbalimbali. Kwa msingi huo, TANESCO ina mradi ya usafirishaji wa umeme katika sehemu mbalimbali nchini....moja ya miradi mipya ya usambazaji ni ule unaotoka Dar-es-Salaam- chalinze- Same-Tanga- Moshi- Arusha........(North East Transmission Line)........ umeme utakaozalishwa Kinyerezi utasafirishwa katika njia hiyo na kuteremeshwa maeneo yote hayo niliyotaja. Vilevile, upo mradi wa North West Transmission Line unaokwenda hadi Kigoma

Sasa umeme huo ukishasafirishwa kwenda sehemu mbalimbali, hatua ya mwisho ni distribution kwa watumiaji ambao ni wananchi, maofisi, viwanda nk

KWahiyo ndugu yangu vuta subira....miradi yote hii itakapokamilika ndani ya miezi 24 matatizo ya umeme yatakuwa ni historia

Nimekuelewa mkuu..maelezo mazuri ..tunaitakia nchi yetu kheri. .kwakweli watanzania tumechoka na mgao wa umeme.
 
Lizaboni, waziri wako Prof mpaka anaamua kununua umeme kutoka Ethiopia bado hujoana tatizo la umeme nchi hii!!!!!!
Kwa taarifa yako Kidatu na Mtera wanazalisha almost 0MW, Kinyerezi wanazalisha 70MW out of expected 150MW, Symbion only 70MW out of 130MW Kianzi inasuasua na around 50MW out of 180MW.
Ndo maana nakuuliza mara kwa mara ulisomea chuo gani name nifuate nyayo.
 
mwijage,simbachawene,masaju,muhongo wote wamerudi tena kupewa na wizara na masaju kuwa attorney general,hawa ndo wanajua gesi yetu inamilikiwa na nani,kuna kitu hapaaaaaaaaa
 
Juhudi za kuondoa tatizo la umeme zinaonekana kuwa ngumu kila kukicha, mvua nyingi zinazoendelea kunyesha nchi nzima zimeshindwa kupunguza mgao wa umeme, Mradi wa gesi Mtwara hadi Dar es Salaam ulitoa matumaini ya kumaliza tatizo la umeme nchi surprisingly tatizo linaendelea, mradi uliogharimu taifa ma billioni ya dola, huwa najiuliza hizi pesa za huu mradi zingetumika kujenga na kuzalisha umeme huko huko mtwara then ukaingia kwenye grid ya taifa manufaa yangekuwa makubwa kiasi gani?

Naomba kuwasilisha.

Unaposoma mitazamo kama hii ndio unaona maradhi ya TZ.
Mungu ibariki TZ :A S 109:
 
Mkuu, naona umeandika tu bila ushahidi. Unaishi Mkoa gani Tanzania ambako kuna mgawo wa umeme?

Watu wasiokuelewa wanakuona kama shabiki maandazi; kumbe lengo la michango yako ni KUAMSHA HASIRA ili watu waichukie serikali yao.
 
Ninyi muache kufanyia mzaha mambo yanayoleta machungu kwa watanzania.Hapa nilipo tangu asubuhi hakuna umeme.Acheni mizaha jamani.
Mkuu, naona umeandika tu bila ushahidi. Unaishi Mkoa gani Tanzania ambako kuna mgawo wa umeme?
 
Kuna MW 450 ambazo zilikuwa kwenye matarajio. Sijui kama ndio kinachoendelea. Naendelea kushangaa ya TRA na TPA kwanza....mengine muda ndio utayaongea vizuri maana kuongea kitu usichokijua itakuwa ni uzushi.
 
Mkuu, naona umeandika tu bila ushahidi. Unaishi Mkoa gani Tanzania ambako kuna mgawo wa umeme?
Usiumize kichwa na wanaokurupuka magufuli kawapoteza ktk front page za magazeti wameibukia jf huku eakizidiwa hawakawii kusepa
 
Back
Top Bottom