Mradi wa EACLC Ubungo kuleta ajira zaidi ya 65,000

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichoko Ubungo Dar es Salaam, ambacho kinatarajiwa kutoa zaidi ya ajira 15,000 za moja kwa moja, na zisizo rasmi takribani 5,000

Katika uzinduzi huo uliofanyika leo Rais Samia amesema: "Kituo hiki cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki kitachangia jitihada zetu za kuhakikisha Tanzania inakuwa chaguo namba moja kwa wafanyabiashara na wasafirishaji wa bidhaa kwa Afrika Mashariki na Kati."

Soma: RC Chalamila amtaka mkandarasi Barabara ya Ubungo - Kimara kuongeza kasi

Mradi huo ulianza kutekelezwa Mei 2023 na umetajwa kugharimu Sh. Bilioni 282.7 hadi kufikia hatua ya kukamilika kwake, ikielezwa kuwa hiyo ni hatua kubwa katika kukuza ajira, hasa kwa vijana na wanawake.

Halikadhalika, kituo hicho kinatajwa kuunga mkono uwekezaji wa ndani na kimataifa, huku kikiunga mkono viwanda vya uzalishaji wa ndani na kuongeza thamani kwa bidhaa za Tanzania.

Chanzo: Jambo tv
 
Ahadi kila siku vijana hawana ajira. Bila mabadiliko ya mifumo na sheria ni kupoteza muda na kuwapa pesa wachina tu
 
Back
Top Bottom