Rais Samia kuzindua Kituo cha Biashara cha - EACLC Ubungo Agosti 2, 2025

Rais Samia kuzindua Kituo cha Biashara cha - EACLC Ubungo Agosti 2, 2025

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
515
Reaction score
822
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki (East African Commercial and Logistics Centre – EACLC) kinachopatikana eneo la Ubungo, kwenye stendi ya zamani ya mabasi jijini Dar es Salaam.



Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA), Bw. Gilead Teri, amesema uzinduzi huo utafanyika rasmi Agosti 2, 2025.

“Kukamilika kwa kituo hiki kutachochea kasi ya biashara na kuongeza thamani ya mauzo, hasa kwa wafanyabiashara wa ndani na wale wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Bw. Teri.


Gilead amesema kuwa Kituo hicho kikubwa na cha kisasa kimekamilika na kipo tayari kwa uzinduzi. Mradi huu mkubwa ulianza kutekelezwa mnamo Mei 2023 na umetajwa kugharimu Shilingi bilioni 282.7 hadi kufikia hatua ya kukamilika kwake.
IMG-20250725-WA0009.jpg

Aidha kwa mujibu wa taarifa ya Gilead, EACLC kinatarajiwa kutoa zaidi ya ajira 15,000 za moja kwa moja, huku ajira zisizo rasmi zikiwa zaidi ya 5,000. Hii inatajwa kuwa ni hatua kubwa katika kukuza ajira, hasa kwa vijana na wanawake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho, Bi Catherine Wang, ametoa wito kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kununua au kukodisha maduka ndani ya kituo hicho. Amesema kuwa bado kuna nafasi chache za kibiashara zilizobakia, huku nyingine nyingi tayari zikiwa zimechukuliwa.

Kwa mujibu wa Manspaa ya Ubungo, Mradi huu unatekelezwa kwa mfumo wa ubia baina ya sekta binafsi na serikali (PPP), ambapo mwekezaji atakuwa na umiliki kwa kipindi cha miaka 32 kabla ya mradi kukabidhiwa rasmi kwa serikali ya Tanzania.

Awali Prof. Mkumbo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo amewai kunukuliwa akiwaondoa wasiwasi wananchi kuwa asilimia zaidi ya 90, watakaonufaika na fursa ya uwekezaji huo ni watanzania.

Soma Kitila Mkumbo: Soko la kimataifa EACLC Ubungo watakaopangishwa asilimia 95 ni watanzania
 
Baada ya miaka 32 mfumo wa biashara utakuwa umebadilika sana.yatabaki magofu tu.
 
FRIDA KAAYA ADAIWA KUVURUGA UCHAGUZI WA UWT WILAYA YA MOSHI MJINI

Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini Frida Kaaya amedaiwa kutaka kuharibu Uchaguzi wa UWT Wilaya ya Moshi Mjini baada ya kutuhumiwa kujaribu kuiba kura za Mgombea wake ambaye ni katibu wa CCM Kata ya Kiusa Yobineshi Mafie.

Katibu huyo amedaiwa kuchakachua kura wakati wa zoezi la kuhesabu kura ambapo kura zilizoharibika na za wengine alikuwa akimpatia mgombea wake jambo lililopelekea mabishano na wagombea wengine kabla ya Msimamizi wa Uchaguzi huo kuingilia kati.

Inadaiwa katibu huyo aliwaagiza makatibu wote wa CCM kata kwenda eneo la Mkutano na kumuombea kura mgombea wake huku baadhi yao wakihusishwa na vitendo vya rushwa hali iliyopelekea TAKUKURU kuwafukuza katika eneo hilo huku Mgombea udiwani kata ya Mjimpya Rashid Maarufu BABA MZAZI ambaye ni mtu wa karibu sana na Katibu huyo wa wilaya kufukuzwa eneo hilo baada ya kukuta akinunulia wajumbe chai na vinywaji.

Hata hivyo mgombea huyo alishindwa vibaya sana katika uchaguzi huo uliendeshwa kwa uwazi, haki na usawa na wagombea wote kukubari matokeo na kusaini fomu za matokeo kama kanuni zinavyoelekeza.

Katika hali ya kushangaza Katibu huyu wa CCM Wilaya alimshauri na kumsaidia mgombea wake kukata rufaa akidai kuwa hakuridhishwa na mchakato wa Uchaguzi hivyo anaomba uchaguzi urudiwe na huku akijinasibu kuwa atagharamia gharama zote za uchaguzi. Kitendo cha Katibu wa CCM wilaya kutumia nguvu kubwa kumsaidia mgombea wake, kumewavuruga wajumbe na kumshangaa kwa nini yeye ambaye kanuni za Uchaguzi zinamtambua kama mkurugenzi wa Uchaguzi anajiingiza kwenye makundi ya kuwabeba wagombea.

Tunaomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka kudhibiti vitendo hivi kwani vinaashiria kuwepo kwa mambo ya kihuni katika uchaguzi ujao wa wabunge na madiwani.
 
Back
Top Bottom