herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,199
- 1,378
Mambo ya hovyo sana na ajabu mada kama hizi kutukana walimu zinakua nyingi na zinaachwa tu.Mtu anayesema kwamba "mwalimu ana laana" nadhanI yeye ndiye mwenye hiyo laana.
Tuache dharau tujifunze kushukuru,hao walimu mnaowashambulia kwa maneno mabaya na kuwaona hawafai ndiyo hao hao waliwashikisha kalamu wakiwafunza kuandika,na hapa ndipo ile dhana Mtanzania anafurahia kuibiwa inapojidhihiri maana mkisikia mwanasheria wa serikali kaiba mnamuona ndiye mwenye akili lakini mwalimu kwa sababu kazi yake ni kuwafundishia watoto wenu na siyo kukutana kwenye vikao vya pesa mnamuona akili hana.
Nafikiri huu si uhuru manq uhuru unaenda na kuheshimiana, utu, wajibu na haki kwa kila mmoja.