Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Waziri wa Afya Dr Haji Mponda amesema yeye atajiuzulu ili kuokoa roho za watanzania ambao wataathirika na mgomo mpya wa madaktari na si kwa shinikizo! Hayo aliyasema jana usiku kwenye kikao cha dharura cha baraza la mawaziri cha kujadili mgomo mpya wa Madaktari na Manesi! Hata hivyo Mponda ametoa rai kwamba watanzania wawe makini sana na jinsi watu wanavyotumia migogoro kwa maslahi yao binafsi huku wakisababisha maafa makubwa kwa raia wasio na hatia. Na kusema kuwa kama wana taaruma wakiingia kwenye ushabiki wa siasa nchi itaingia kwenye mgogoro mkubwa na kudhoofisha ustawi wa taifa letu!
Nadhani mponda amesahau kuwa kujiudhuru hakuna rangi, kwamba akijudhuru hivi inakuwa vile, akaijiudhuru vile inakuwa hivi. Sisi tunachotaka yeye ajiuzuru yaani aachie kiti cha uwaziri, kama alikuwa anataka kujiudhuru kwa sababu ya kuepusha vifo si angekuwa ameshajiudhuru???kwani hakuna wagonjwa waliokufa kutokana na mgomo wa mwanzo???