13% ya Vifo vinavyotokea Nchini vinatokana na Shinikizo la Juu la Damu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Idadi hiyo ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya ambapo kwa Dunia Vifo vimepita Milioni 20 huku Magonjwa ya Moyo yakiripotiwa kuongezeka kwa 9% kutoka 1% ya mwaka 1980. Pia, imebainika kila kwenye Watu 100, Watu 12 wana tatizo la Kisukari na 25 wana Shinikizo la Juu la Damu Nchini Tanzania.

Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) umeonesha makundi yote ya Watu kiumri yanasumbuliwa Maradhi ya Moyo huku wenye Miaka 15 na kuendelea wakisumbuliwa zaidi na Mishipa ya Moyo huku wenye miaka 20 hadi 40 wakisumbuliwa na Shinikizo la Juu la Damu.

Aidha, Kati ya Wagonjwa 83,356 waliotibiwa JKCI mwaka 2022, Wagonjwa 59,022 (66.8%) walikuwa na tatizo la Shinikizo la Juu la Damu huku tafiti za hivi karibuni zikionesha Uchafuzi wa Hewa ni chanzo kikuu cha Magonjwa hayo ikifuatiwa na Mtindo wa Maisha na Vyakula.
 
Back
Top Bottom