Last edited by a moderator:
Duh.. ndio demokrasia gani! Mbowe hajiamini hata kugombea na mgombea bandia wa kupangwa? Yeye yuko confident kugombea na hewa tu! No wonder zzk kutiwa kabali na kupigwa ngwara mapema. alikua tishio dhahiri.![]()
![]()
Hamkani hali si shwari ndani ya Chadema! Kansa Mohamed Mbaruku, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Tabora, amejitoa kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa, hivyo kumfanya kwa mara nyingine Freeman Mbowe kuwa katika mashindano ya 'farasi' mmoja.
Kwa mujibu wa 'Mwananchi Breaking News', Mbaruku ameamua kujitoa kwa madai kwamba katiba ya chama hicho imekiukwa na akasema atakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uchaguzi huo na kuomba ufafanuzi wa kikomo cha uongozi.
Mbaruku amejitoa siku moja tu kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake, ambao umepangwa kufanyika kesho Jumapili Septemba 14.
Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba kujitoa kwa mgombea huyo kunaweza kusababisha mpasuko ndani ya Chadema kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya uongozi kwamba unaendesha chama kama 'taasisi
binafsi'.
Awali Mbaruku aliwasilisha pingamizi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, ambapo pamoja na mambo mengine, alidai kwamba Mbowe hana sifa kikatiba ya kugombea tena nafasi hiyo.
Pia duru za siasa ndani ya chama hicho zilieleza kwamba, majina mawili yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda katika chama hicho, Benson Kigaila, kwamba nao walijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti, Daniel Ruvanga na Garambenela Frank, yalikuwa majina hewa yaliyolenga kumsafishia njia Mbowe ya kubakia kuwa mgombea pekee baada ya kuenguliwa kwa Mbarouk.
Inaelezwa kwamba, Katiba ya Chadema hairuhusu kiongozi wa nafasi hiyo kugombea vipindi zaidi ya viwili vya miaka mitano.
Hakuwa mgombea mwenza. Chadema haina hayo ya ugombea webza. Huyu ni mamluki wa ACT-CCM aliingia kichwa kichwa kupina upepo kaona itamcost, kaweka mpira kwapani katoka ndukimgombea mwenza kwa nafasi ya uwenyekiti chadema taifa atangaza kujitoa,anasema amechezewa rafu.
Hakuwa mgombea mwenza. Chadema haina hayo ya ugombea webza. Huyu ni mamluki wa ACT-CCM aliingia kichwa kichwa kupina upepo kaona itamcost, kaweka mpira kwapani katoka nduki
Alijaribu kwenda Zanzibar kwa kuogelea kumbe hata kuogelea hawezi, wasaliti hawana nafasi ktk mambo ya maendeleo.
Hakuwa mgombea mwenza wa chadema ila ni mgombea wa act aliyetaka kuwa kiongozi wa chadema.
Watu wengine nimajanga wanatumika kupambana na waliobora zaidi yao mia mara sabini.
niheri asinge jitoa angesubiri afike mwisho,kwa tukio hili na lile la kukisema vibaya chama anapaswa kuchukuliwa taratibu za kinidhamu haraka sana ikibidi
Tulijua toka mwanzo kuwa haya yatatokea.mgombea mwenza kwa nafasi ya uwenyekiti chadema taifa atangaza kujitoa,anasema amechezewa rafu.
Hakuwa mgombea mwenza. Chadema haina hayo ya ugombea webza. Huyu ni mamluki wa ACT-CCM aliingia kichwa kichwa kupina upepo kaona itamcost, kaweka mpira kwapani katoka nduki