Mpinzani wa Mbowe ajitoa

Mpinzani wa Mbowe ajitoa






Hamkani hali si shwari ndani ya Chadema! Kansa Mohamed Mbaruku, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Tabora, amejitoa kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa, hivyo kumfanya kwa mara nyingine Freeman Mbowe kuwa katika mashindano ya 'farasi' mmoja.


Kwa mujibu wa 'Mwananchi Breaking News', Mbaruku ameamua kujitoa kwa madai kwamba katiba ya chama hicho imekiukwa na akasema atakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uchaguzi huo na kuomba ufafanuzi wa kikomo cha uongozi.


Mbaruku amejitoa siku moja tu kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake, ambao umepangwa kufanyika kesho Jumapili Septemba 14.


Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba kujitoa kwa mgombea huyo kunaweza kusababisha mpasuko ndani ya Chadema kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya uongozi kwamba unaendesha chama kama 'taasisi

binafsi'.


Awali Mbaruku aliwasilisha pingamizi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, ambapo pamoja na mambo mengine, alidai kwamba Mbowe hana sifa kikatiba ya kugombea tena nafasi hiyo.


Pia duru za siasa ndani ya chama hicho zilieleza kwamba, majina mawili yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda katika chama hicho, Benson Kigaila, kwamba nao walijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti, Daniel Ruvanga na Garambenela Frank, yalikuwa majina hewa yaliyolenga kumsafishia njia Mbowe ya kubakia kuwa mgombea pekee baada ya kuenguliwa kwa Mbarouk.


Inaelezwa kwamba, Katiba ya Chadema hairuhusu kiongozi wa nafasi hiyo kugombea vipindi zaidi ya viwili vya miaka mitano.

Ukimaliza kakojoe ulale baada ya kusoma katiba unasema imeelezwa nanann mtaje
 
Soon atatangaza kuhamia ACT,was just a plan ya kutoa political mileage kwa ACT itayoendana na propaganda hasi dhidi ya uongozi wa CHADEMA,tatzo sio katiba,bali kumchafua Mbowe na safu yake kwani CCM haitaki waendelee kuongoza,bali vibaraka wao!!
 
kwanza mtu mwenyewe anaitwa kansa wazazi wake hawakukosea kumwita kansa asiingize kansa kwenye chama chetu.
 
Msaliti huyu anatumiwa na Maintarahamwe kupitia kitengo chao cha msajili wa vyama.
 
Ha!ha!haa! Keshasngalia mwenendo wa chaguzi zilizopita kaona itakua aibu ya mwaka ndo maana kakimbia.
 
Wameona wajumbe wa mkutano mkuu hawanunuliki. Wakaogopa aibu na kujitoa kusudi isiwe katika kumbukumbu kuwa alipata zero.
 
Kule nyumbani Tabora kuna mashamba mengi ya tumbaku hivyo ni vyema angejikita zaidi katika tumbaku na hizi harakati awachie watu wanaojua, sasa mpinzani gani unajitoa kiholela? Si ndio hawa mizigo ya chama.
 
Nimempenda bila gharama Mh. Mtukufu Kansa. Loh! huo ndo uanaume. Mwanaume wa kweli, analamba hiyo mihela, anatoka nje anajitutumua, aoneshe kuwa yupo siriasi, halafu akiisha hakikisha ameficha uchagoni mihela anatokeza nje tena; anawaambia walio mtuma; Funga domo lako au nkutangaze.
Maccm hoi, tena yamepata BARIDIIIIII. Tangu mmejaribu kwa kumtumia ZZK na kampuni zake mkashindwa, mlidhani mtaleta mpasuko kwa kumtumia mtu mwenye kansa ya uongozi mtaweza???
Bahati yenu ni kuwa, huyo Kansa sidhani mlimpa zaidi ya laki moja. Ni ile fomu tu mli mnunulia. Mh. Mwingulu, Mh. Massatu naomba kuwakumbushia kuwa, Neno la mwanaume lisipotimia tunasema mwanaume huyo ni MZUSHI. Naona Chadema bado inachanja mbuga. 2015 is just here. Na kile kifo cha ghafla cha CDM ni kama ndoto. Mnatapatapa mpaka kutumia mitego mibovu yenye Kansa ya Tabora. Ni mawazo yangu tu jamani msinichukie miye muwaza hovyo
 
hapo ndipo tunapoona huo mchezo wao walioupanga wa kitoto, du kweli kansa amewaambukiza kansa wadau wake ccm/act.
 
Kasoma alama za nyakati akaona ajitoe tu maana anaweza asipate hata kura moja.
Hivi huyu Kansa yeye kaomba kugombea sasa suala la Mbowe linamsumbuaje kansa? Sasa ni bora asiende kwa msajili bali aende mahakamani kabisa. Damn kansa!
 
Dawa ya mpumbavu ni kumpuuza tu ataona aibu mwenyewe. Hajachukua round kajidhihirisha kuwa anatumika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom