Mpinzani wa Mbowe ajitoa

Mpinzani wa Mbowe ajitoa

Mkuu Bramo, utabiri wako umetimia. Au wewe ni miongoni mwa waratibu wa mpango huo nini? Na je kanuni zenu zinasemaje kwa mtu anayejitoa hatua za mwisho

Anaejitoa dkk za mwisho adhabu yake ni kufukuzwa uanachama,kwa hiyo magamba jiandaeni kuupokea mzoga wenu ulioathiriwa na Kansa.
 
Kansa Mbaruk! Kweli majina huumba, hiyo kansa itakuwa imeshatafuna ubongo wake.

alipandikizwa kwa malengo ya watu flaniflani kwa maslai ya kundi flani.
viongozi wanapaswa kumwajibisha haraka sana kwa maslai ya chama
 
kilichobaki sasa ni kufukuzwa ndani ya chama,akiacha atakuja kusumbua kwa hapo baadae

Huyu nin wa kufukuza, hafai. Huu muda sio wa kuleta chokochoko ndani ya chama maana ni wakati tete ukichukulia nguvu zote za dola zimeiangalia CDM
 
Tulijua toka mwanzo kuwa haya yatatokea.

Kwa nini mkamtuma kama mlijua? Mjulishe na Kinana kuwa hata msajili wa vyama vya siasa atajitoa tu mbele ya CHADEMA. Na Mbowe lazima atakuwa mwenyekiti atake asitake. Ni vigumu sana kuchakachua mpango wa Mungu!
 
Inawezekana ana uhusiano na CCM guyu maana hata mwenyekiti CCM mkoa wa Shinyanga HAMIS MGEJA alimpongeza kuamua kugombea kwake uenyekiti wa chadema taifa katika mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika ngokolo mtumbani mwanzoni mwa mwezi huu,maana kulikuwa na hila za kila aina ili mbowe asiwe mwenyekiti ili chama kiyumbe,lakini wameshindwa kwa jina la Yesu wataendelea kuwa vibaraka lakini mwisho wa siku ni aibui wamwulize ZItto ambaye yuko njia panda anaangali gia ya kuondokea chadema na kuingilia ACT,washamba hao lakini wajue kuwa si rahisi kukabiliana na mtu aliyebeba kusudi la Mungu mpaka alitimize CHADEMA NI CHAMA KILICHOLETWA NA MUNGU na kimejengwa juu ya mwamba wala upepo wa ccm hautakitikisa
 
Kweli usipotumia akili na nguvu zako vyema kuna wajanja watajipenyeza kukutumia kwa faida yao!!!
Wasaliti daima wanaendeshwa kwa rimoti na mabwana zao; mara nyingi wanastuka muda ukiwa umeyoyoma! Rejea Yuda Iskariote, et al
 
Huyu nin wa kufukuza, hafai. Huu muda sio wa kuleta chokochoko ndani ya chama maana ni wakati tete ukichukulia nguvu zote za dola zimeiangalia CDM

Uongozi wa CHADEMA unamtafuta ili alipe hela za T-shirt 1000 alizokabidhiwa wakati wa zoezi la M4C.
Onyo: unapotoa jina la mtoto angalia madhala yatokanayo na jina hilo. Wazazi kumpa mtoto jina KANSA sijui walimaanisha kinachotokea?!!
 
napendekeza afukuzwe ndani ya chadema,kwani ameonesha makucha yake ingali bado mapema sana.


hata mie naunga mkono afukuzwe, hilo jitu kwanza latokea huko kanda ya ziwa/tabora, pili hana asilia ya kichaga, tatu hakuowa mchaga na wala dadayake hakuolewa na mchaga, na tena muislamu, atagombeaje uenyekiti wa chadema, na hatimiza masharti yote yanayompasa mtu kugombea kugombea uenyekiti wa chadema.

Huyo ni mroho sana afukuzwe tuu, na tena apigwe na kila lema na lile genge lake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom