Mpina, Panya anayejaribu kumvisha paka kengele!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,640
697,940
Kuna usemi unasema, "Usimuone kima mjini ukamrushia jiwe (yaani hakufika pale peke yake)."

Pale bungeni wapayukaji ni wengi, lakini zinapotokea 'sensitive issues' kwa maslahi ya taifa katikati ya hao wapayukaji kuna watu maalum huandaliwa kuongea facts kwa data. Hao waandaaji ndio hutoa data kwa usahihi katika uhalisia wake na hutoa ulinzi na backup kwa watakaolifikisha hilo jukumu kwa jamii hasa kupitia chombo rasmi cha bunge.

System ina data halisi kwenye kila jambo, liwe kubwa ama dogo, lakini kamwe haiwezi kujitokeza kwenye jamii na kusema chochote. Inapolazimika kufikisha jambo kwenye jamii basi hutafutwa watu sahihi kwa vigezo vyao kulifanya hilo jambo.

Wewe kama ni jambazi muuaji lakini bado umeweza kukwepa mkono wa sheria maranyingi huwa unawekwa kiporo kama ukionekana 'unafaa' kwa mahitaji ya baadae. Siku kukiwa na kazi chafu ya kula kichwa utaitwa ufanye hiyo kazi huku mafaili yako yote yakiwekwa wazi mbele yako!

Wahuni, vibaka, mapusha, wauza ngada, wauza bangi, wauza watu. Wauza gongo nknk. Kuna mahali mafaili yao yote yapo. Ikitokea kazi ya kwenda kuvunja na kufanya uharibifu mahali bila kuchukua chochote ni kumchomoa mmoja tu sahihi kwenye mafaili.

Mpina si msafi kivile kwakuwa naye ni walewale tu, lakini kwa hesabu na data alizotoa tangu jana na kuhitimisha kuwataja kwa majina baadhi ya watuhimiwa. Hizo ndio zinaitwa 'kazi maalum' na kuna sababu ya kumtumia mtu kama yeye kufikisha ujumbe tarajiwa.

Kianzio kimeshawekwa wazi ni kazi ya wahusika bungeni sasa kukifanyia kazi, kati ya vile vichwa vitatu alivyotaja Mpina kimoja ndio kinawindwa zaidi, na hiki wakifanikiwa kukidondosha vingine hata vikibaki sio ishu tena!

Makusanyo ya TRA kila mwezi si chini ya Trillion moja, hapo bado kuna misaada, hapo bado kuna mikopo. Hata kama sijui hesabu lakini najua kwa mwaka ukichanganya makusanyo yote bila kusahau tozo mbalimbali serikali haiwezi kukosa trillion 20 ama pungufu kidogo ama zaidi kidogo.

Sasa ni kutoka kwenye hayo makusanyo, tozo, misaada na mikopo ndio washika dau wanajichotea kila mmoja kwa urefu wa kamba yake, lakini system ina data zote kwa kila sent inapoenda!
 
Mpina si msafi kivile kwakuwa naye ni walewale tuu, lakini kwa hesabu na data alizotoa tangu jana na kuhitimisha kuwataja kwa majina baadhi ya watuhimiwa.. Hizo ndio zinaitwa 'kazi maalum' na kuna sababu ya kumtumia mtu kama yeye kufikisha ujumbe tarajiwa
Kianzio kimeshawekwa wazi ni kazi ya wahusika bungeni sasa kukifanyia kazi..kati ya vile vichwa vitatu alivyotaja Mpina kimoja ndio kinawindwa zaidi, na hiki wakifanikiwa kukidondosha vingine hata vikibaki sio ishu tena!
Jamaa ghafla kageuka 'whistleblower'....
 
Mshana Jr,
Ni kweli Mpina sio msafi kivile ILA
Watu kama Madehu ni watu hatari kabisa na kuvaa yale matai na skafu sio uzalendo!
Hawa ndio majizi yetu kwa mikataba ya hovyo iliyotuingiza ktk hasara kuu!
Wiki hii lazima kiumane
FB_IMG_1681263492200.jpg
 
Mh Mpina the personal attack is too much kwa Mh Mwigulu haiwezekani ukamuandama Mwanaume mwenzio hivyo nina wasi wasi na jinsia yako ?Mambo ya Uganga wa kienyeji kuna uongo gani wewe ndio Mchawi mkubwa na mlishaongea bungeni mkamaliza ? Kwa nini ulimi uteleze umeamua kwa makusudi kutoa takwimu za uongo unajifanya ulimi umeteleza uchochezi huo

Husibishane na mtu bishana na taasisi

Mh Raisi wakina Mpina hawakufungua ulimi enzi za mwenda zake tumia njia hiyo ya mwenda zake kuwapa discipline kwa wote wanaoleta midomo kwenye serikali yako
 
Kwa hiyo ule utajiri wa ghafla ghafla, matozotozo na kwingine penye njuluku michongo ilifanywa na huyo bwana ili kukinga matone yanayovuja na kujipatia ukwasi mwingi kupitia mianya hiyo? Ok, sawa, sasa kama wanajua kila senti ilikovujia kwa nini waliacha ziendelee kuvuja, ina maana nao hawakukinga vikapu vyao kuambulia japo senti moja? Walaji hawajawahi kuisha nchi hii, hata wakiwekwa wengine nao watakula tu kwa mtindo wao
 
Kwa hiyo ule utajiri wa ghafla ghafla, matozotozo na kwingine penye njuluku michongo ilifanywa na huyo bwana ili kukinga matone yanayovuja na kujipatia ukwasi mwingi kupitia mianya hiyo? Ok, sawa, sasa kama wanajua kila senti ilikovujia kwa nini waliacha ziendelee kuvuja, ina maana nao hawakukinga vikapu vyao kuambulia japo senti moja? Walaji hawajawahi kuisha nchi hii, hata wakiwekwa wengine nao watakula tu kwa mtindo wao
Kazi yao sio kuziba ama kuzibua bali ni kuonesha panapovuja
 
Back
Top Bottom