Mpina atakiwa apeleke Ushahidi wa Madai yake kwamba Maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa hayatekelezwi na Watendaji wa Serikali!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,961
141,959
Akizungumza Bungeni leo Lugaha Mpina amedai ya kuwa kuna maagizo aliyatoa Waziri Mkuu na hayafanyiwi kazi na Waziri Mkuu yupo kimya hatua inayoonesha labda naye ameridhia

Hata hivyo hoja zake zilipingwa na Waziri Jennista Mhagama akidai ya kuwa hazina ukweli kwamba maagizo yanafanyiwa kazi na machache sana inawezekana bado hayajafanyiwa kazi

Mpina amesema kuwa tangu Waziri Mkuu akataze ‘Kamatakamata ya Mifugo bila kushirikisha Wananchi’, jambo hilo limekuwa likiendelea katika baadhi ya maeneo akidai na ushahidi upo

Spika wa Bunge amemtaka Mpina kuwasilisha Ushahidi wa mambo hayo kabla yeye hajatolea uamuzi jambo hilo ikiwa ni kweli Mpina amedanganya Bunge au la (Taarifa ya Waziri Mhagama)
==

MY TAKE
Hapa nadhani Mpina keshaingia Kwenye 18 akishindwa kuleta ushahidi atatupwa nje ya Bunge hadi mwakani 2024

Akirudi Ripoti ya CAG ishajadiliwa na maazimio yameshatolewa

Mungu wa mbinguni awabariki!
 
Hapa nadhani Mpina keshaingia Kwenye 18 akishindwa kuleta ushahidi atatupwa nje ya Bunge hadi mwakani 2024

Akirudi Ripoti ya CAG ishajadiliwa na maazimio yameshatolewa

Mungu wa mbinguni awabariki!
Yapo mengi mimi mpina aje pm nimtumie yamejaa tu hata la michango shuleni, usambazaji wa mbolea,kodi kwa mazao ya kilimo,kuandikisha watoto shule,kuvuta shisha,

Kiufupi ukipitia hotuba za waziri mkuu na kinachotokea ni zero tupu ni kama mpiga kelele tu.

USSR
 
Hapa nadhani Mpina keshaingia Kwenye 18 akishindwa kuleta ushahidi atatupwa nje ya Bunge hadi mwakani 2024

Akirudi Ripoti ya CAG ishajadiliwa na maazimio yameshatolewa

Mungu wa mbinguni awabariki!
CCM ni tatizo kubwa na baya sana nchini kwetu.

Hizo figisu zote ni zao wao kwa wao, ni mambo yao ya ulaji na maslahi yao tu; hawajui wala kujali Taifa au wananchi.

Leo tunashuhudia live maana ya kauli:-
"Wapinzani wanatu cheleweshea maendeleo..."
"Nipeni mafiga matatu...."
Bunge hili ni lake na ndio "legacy" ya hayati Magufuli hasa!

Yatosha sasa! Tunataka Katiba Mpya.
 
Sio maagizo ya waziri Mkuu tu hata ya Rais Samia Suluhu Hassan wala makamu wake dkt mpango ni kelele tu kwa watendaji

USSR
Ulitaka awauwe ndo mjue wanafanya kazi nchi ina sheria mzee. Malalamiko tuuu
 
Hapa nadhani Mpina keshaingia Kwenye 18 akishindwa kuleta ushahidi atatupwa nje ya Bunge hadi mwakani 2024

Akirudi Ripoti ya CAG ishajadiliwa na maazimio yameshatolewa

Mungu wa mbinguni awabariki!
Wewe endelea kumsubiri mpina na maazimio yenu.....wajanja washausoma mchezo wanafanya yao...
Kila mtu ashinde mechi zake...
 
Back
Top Bottom