Mpigie simu mbunge wako...

kwa wanaotaka kujua msimamo wa chadema kuhusu posho, someni hapa chini kama bado hamjasoma!


Mnyika: Tunapinga nyongeza ya posho
• Wamtaka Spika Makinda atoe kauli


na Bakari Kimwanga




WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamepinga hatua ya kupandishwa kwa posho za wabunge kulikoripotiwa na vyombo vya habari hivi karibuni.

Wabunge wa chama hicho wamesisitiza msimamo wao wa kutaka posho za vikao zifutwe kwa wabunge na katika mfumo mzima wa malipo ya wakati wa kazi miongoni mwa watumishi wa umma.

Msimamo huo ulitolewa jana na katibu wa wabunge wa CHADEMA, John Mnyika, ambaye pia ni mbunge wa Ubungo, ambapo alisema ingawa hawajapokea taarifa rasmi ya nyongeza hiyo ya posho, bado wanasisitiza msimamo wao wa kutaka posho hizo ziondolewe.

Mnyika alitoa tamko hilo kupitia taarifa aliyoituma kwa vyombo vya habari baada ya kuandikwa kwa habari kwenye moja ya magazeti ya kila siku (si Tanzania Daima), Novemba 28 na 29 mwaka huu, ikihusu kupanda kimya kimya kwa posho za wabunge kwa zaidi ya asilimia 150.

"Wabunge wa CHADEMA hatujapokea taarifa rasmi kwamba masharti ya kazi ya ubunge yamebadilika na kwamba viwango vya posho vimeongezwa. Wala kamati ya wabunge wetu haijawahi kuridhia ongezeko lolote la posho ya vikao kwa wabunge. Napenda kutumia fursa hii kusisitiza msimamo wetu wa kutaka posho za vikao ziweze kufutwa kwa wabunge na katika mfumo mzima wa malipo ya wakati wa kazi miongoni mwa watumishi wa umma," alisema Mnyika.

Katibu huyo wa wabunge wa CHADEMA, alitoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete kwa niaba ya serikali na Spika Anne Makinda kwa niaba ya Bunge, kutoa kauli kuhusu nyongeza hiyo ili kuondoa hisia zinazojengeka kwamba wabunge wote wamekaa bungeni na kukubaliana kujiongezea posho ya vikao.

"Ni vyema umma ukafahamu kwamba Sheria ya Utawala wa Bunge ya mwaka 2008 kifungu cha 19 kinataja aina ya posho ambazo zinaweza kutolewa kwa wabunge kama ambavyo Rais ataeleza kwa maandishi. Katika kipengele (d) sheria imetaja orodha (i) mpaka (iii) ya posho ambazo wabunge wanastahili kulipwa za usafiri, kujikimu na wasaidizi.

"Katika orodha hiyo hakuna posho ya kikao ambayo inalipwa hivi sasa kwa kuwekwa kwenye akaunti za wabunge moja kwa moja ambayo kamati ya wabunge wa CHADEMA tunataka ifutwe mara moja kama sehemu ya mchakato wa kubadili mfumo mzima wa malipo ya posho kwa watumishi wa umma," alisema na kuongeza katibu huyo wa wabunge.

"Kifungu 19 (d) (iv) kimempa mamlaka Rais ya kutoa posho nyingine kwa wabunge kwa kadiri atakavyoelekeza; kifungu hiki kimetoa mwanya wa kutolewa kwa waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais wa Oktoba 25, 2010 wenye kumbukumbu na CAB111/338/01/83 masharti ya kazi ya mbunge, ambao umeeleza viwango vya posho mbalimbali ikiwemo kutoa posho ya vikao.

Alisema ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge zina wajibu wa kuwaeleza Watanzania iwapo waraka huo umebadilishwa na sababu za wabunge kutojulishwa kuhusu mabadiliko hayo.

Mnyika alisema iwapo mabadiliko hayo yamefanyika ni muhimu yakasitishwa kwani yatakwamisha utekelezaji wa mpango wa kufuta posho za vikao na kupunguza matumizi ya serikali kama ilivyoelezwa katika Ilani ya CHADEMA ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, uliopitishwa bungeni mwaka 2011.

Alisisitiza ni lazima serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima hasa wakati huu ambapo uchumi wa nchi unasuasua na serikali ikiwa katika hali mbaya ya fedha.

"Binafsi natarajia serikali ije kwetu wabunge na mpango wa kukabiliana na ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi badala ya kutuletea mpango wa kutuongezea wabunge posho za vikao huku mwelekeo wa uchumi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ukiwa kwenye hali tete."

Kamati ya wabunge wa CHADEMA ilikubaliana posho hizo zifutwe kwa kuwa ilani yao ya mwaka 2010 imeeleza kwamba lengo la msingi ni kuondoa posho za vikao; hatua itakayoambatana na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kuendana na ujuzi, nafasi na wajibu, ili wafanyakazi walipwe kwa haki kwa kile wanachofanya kwa haki.

"Uamuzi huo pia ungewezesha kuelekeza fedha zaidi katika miradi ya maendeleo, hivyo Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge zizingatie kuwa serikali ya CCM imeridhia msimamo huo na kuuingiza kwenye Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano 2011/2012-2015/2016 uliosainiwa na Rais Kikwete Juni 7, mwaka huu, ambao kwenye ukarasa wa 17 unatamka bayana kwamba posho za vikao na nyinginezo zinapaswa kufutwa au kuwianishwa, hivyo kuziongeza ni kupuuza mpango huo," alisema.
 
Yaani natamani kama ningekuwa nauwezo wakuzihamisha hizoposho za wabunge wakapewa WALIMU,MANESI na MADAKTARI ningefanya hivyo kweli kinaniuma sana. :embarassed2::embarassed2:
 
Mbunge wa kwetu kule Bukene; yeye ana laini tatu, mbili ni zile tuzijuazo wakati tuko naye wote na alipokuwa hajapata nafasi!! Kwa sasa ameongeza laini ya tatu, hii inaitwa "pulaiveti laini" ya mheshimiwa!!

Wewe MKJJ untaka kuwachonganisha watu humu na wabunge wao!!!
 
[h=6]Mpigie simu mbunge wako simu mtake akugawie kidogo fedha za kukusaidia matatizo yako ya hapa na pale. Namba yake unaweza kuipata kwenye Parliament of Tanzania Hasa wale ambao wanaunga mkono kupewa posho au wako kimya! [/h]

Mbunge wangu yuko bize na ujenzi wa makazi yake mapya bunju. Jimbo lipo mkoan hana muda nalo tena. Mwenzetu kila siku ananawiri.
 
Jamani sasa hata wakitugawia tutachukua ngapi ngapi? hapa Jimbo la Ubungo itabidi Mnyika afanye
utaratibu wa kupata thumni thumni.
 
Umefanya la maana kutukumbusha, manake wabunge wanadai hizo posho zinatumika kusaidia wananchi, ngoja nimtafute mbunge wangu ABOOD aniwezeshe maanake wikend hii shem wenu anakuja af sina kitu na hapa nilikuwa napiga hesabu jinsi ya kupata ela..
 
Si kazi ya mbunge kukupa pesa kwa ajili ya matatizo yako. Kama kuna mbunge anafanya hivyo na kama kuna watu wanafikiria hiyo ni kazi ya mbunge basi kuna tatizo la msingi kwa watanzania.
 
Hii ndo Tanzania,na hawa ndo aina ya viongozi tulionao.Tujipime wenyewe tuone kama tunastahili kuendelea kuwaweka hawa viongozi madarakani,kama hatustahili tuingie barabarani mpaka kieleweke.Peoples power ndo suluhisho la mambo yote,na hakika hawatalala kama alivyokwisha kusema aliyekuwa mtoto wa mkulima
 
Mbunge wangu mgonjwa kwa sasa akipona nitamcheki!
Ila hii nyongeza imefanywa makusudi ili ionekane wabunge nao hujimegea kama ilivyo kwa Executives nkimaanisha mhimili ambao kila leo wanaukosoa
 
simu wamebadili nakunasheria ya kudhibiti mawasiliano ya kuwa kama mtu ukimaliza miezi mingi utumii simu yako na hakuna ripoti waweza kushitakiwa, hii imekaaje kwa watunga sheria kuzima simu zao mda mrefu sana
 
Ulimbukeni wa baadhi ya wabunge kwenye posho umenisikitisha sana,hata wale ambao sikutarajia !
 
Kwangu M/kijiji umenipa mtihani mkubwa sana maana mbunge wangu ni Jeremia Sumari wa Arumeru Masharaki hata kuapishwa hajaapishwa, sijamsikia, sijamuona tangu achaguliwe na jimbo letu linaendelea tu sawa naya wabunge wenu wanaochota mabilioni? Jiulizeni!
 
Kwa bahati mbaya,tena kwa fedheha ambayo haikutarajiwa Mbunge wangu ndiye alikuwa mtoa hoja na kuipa nguvu hoja yake ya kutaka nyongeza ya posho tofauti na msimamo wa chama changu kwamba ana mialiko 26 ya kuchangia.......

Sijui Mbunge wa aina hii anafikiria nini kutoa reckless statements za aina hii.Ni vigezo gani vitakavyotumika kuhakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo?ni mfumo gani huo mpya wa matumizi ya fedha za Umma kwa mtindo huo? Auditing procedures itakuwaje maanake hapa tunaongele public funds ambazo ziko kwenye mfuko wa mtu kama mshahara/allowance.

Ni bora hata angetoa suggestion ziingizwe kwenye mfuko maalumu wa jimbo,hata hivyo kazi ya mbunge ni kuwawakilisha wananchi na unaijua kazi yako ipasavyo basi buni miradi na vyanzo vya funds ili kuwasaidia wananchi katika maendeleo

To make it worse,kama ilivyonukuliwa na vyombo vya habari anasema "nilidhani ukiwa Mbunge unalipwa pesa nyingi".

WanaJF na watanzania wote kwa Ujumla,mbunge au kionganayejali maslahi ya wananchi tyumpongeze bila kujali itikadi za vyama vyetu.Tufikie mahali sasa tuwe na ushabiki(kama una manufaa) kwenye maslahi ya watanzania wote na taifa kwa ujumla
 
Nimempigia mbunge wangu Halima Mdee angalau anipatie sent ya mafuta ya shinda mkoko kangu, ameni jibu kuwa hiyo posho waliyoongezewa haiwatoshi eti wana majukumu mengi sana ya kitaifa...

Mbunge wangu amenawira sana siku hizi na chunusi nimeisha siku hizi,majukumu yake ameyasahau kabisa.
 
Back
Top Bottom