Mpenzi wangu ameamua kuokoka hataki mambo ya zamani -nifanyeje

wadau, mi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwa sasa kaamua kuokoka na anadai maandiko hayamruhusu kufanya tena upuuzi wa zamani (yaani uasherati). Nimembebeleza na kumwambia kuwa niko tayari kuokoka ili nimpate lakini anasema hata nikiokoka uhusiano wangu na yeye hautaweza kuendelea. Na amenionya nisithubutu kuokoka kwa ajili yake na kama nataka kuokoka niokoke lakini si kwa ajili ya kumpata yeye. Anasisitiza kuwa inabidi amwombe Mungu ampe mme kutoka kwake hivyo mi ndo basi tena.

wadau hebu nisaidieni nifanyeje. Je nimuibukie huko huko church au nifanyeye maana bado nampenda na sitaki kumpoteza. :confused2:


mkuu kuokoka hakumzuii mtu kuwa na mpenzi na hilo la kuoteshwa mume ni kujitetea tuu hakuna kitu kama hicho
hicho ni kibuti cha kiaina na ameamua tuu kukuacha kiaina
 
Amechagua fungu bora, na ankwambia usiokoke kwa ajili yake kwa sababu mwisho wa siku ukishampata utarudia tabia zako kupretend kuna mwisho wake ipo siku utachoka. pole sana usiijali bwana atakupa wa kufanana naye.
 
Asikwambie kitu nenda Church okoka mipango mingine itajiseti huko.
 
wadau, mi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwa sasa kaamua kuokoka na anadai maandiko hayamruhusu kufanya tena upuuzi wa zamani (yaani uasherati). Nimembebeleza na kumwambia kuwa niko tayari kuokoka ili nimpate lakini anasema hata nikiokoka uhusiano wangu na yeye hautaweza kuendelea. Na amenionya nisithubutu kuokoka kwa ajili yake na kama nataka kuokoka niokoke lakini si kwa ajili ya kumpata yeye. Anasisitiza kuwa inabidi amwombe Mungu ampe mme kutoka kwake hivyo mi ndo basi tena..
yupo sahihi kabisaa, inawezekana wewe unataka kuchakachua tu, propose ndoa
 
Umemwagwa kistaartabu sana mtu wangu! But weye ulikuwa unafurahia kutungua tuuuuu kachomoa ndo unatangaza ndoa? Kha!
 
Huyo achana naye atakua amepata mtu mwingine
kama upo naye karibu jaribu kumfuatilia utaona.
 
Huyo Dada amechagua UZIMA badala ya MAUTI - Amemfanya YESU kuwa Bwana na Mwokozi wake - sasa wewe hutaki??? wewe si ulikuwa ndio Bwana kwake - kampata BWANA WA UKWELI --- YESU .................... kwanza unasikitisha sana yaani ulikuwa unamchezea Dada wa watu ... kufunga nae ndoa hutaki................ ulikuwa unampenda kweli au ulikuwa unapenda ngono?????

Mwambie Yesu akuokoe na wewe la sivyo HUKUMU inakungoja - angalia Bwana unayemtumikia ... shetani ... atakufunga na utaendelea kuchezea wa- dada wa watu -- bila ndoa -- MUNGU HAPENDI HIVYO .... GEUKA LEO UPONE...... mwache DADA wa watu aendelee na YESU WAKE ALIYEMPATA.
 
wadau, mi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwa sasa kaamua kuokoka na anadai maandiko hayamruhusu kufanya tena upuuzi wa zamani (yaani uasherati). Nimembebeleza na kumwambia kuwa niko tayari kuokoka ili nimpate lakini anasema hata nikiokoka uhusiano wangu na yeye hautaweza kuendelea. Na amenionya nisithubutu kuokoka kwa ajili yake na kama nataka kuokoka niokoke lakini si kwa ajili ya kumpata yeye. Anasisitiza kuwa inabidi amwombe Mungu ampe mme kutoka kwake hivyo mi ndo basi tena.

wadau hebu nisaidieni nifanyeje. Je nimuibukie huko huko church au nifanyeye maana bado nampenda na sitaki kumpoteza. :confused2:

Hongera kwa kuwa na mtu aliyemjua mungu katika maisha yako. Hivi una haja ya kutuuliza hebu jichech halafu uone kama utaweza kukesha nae halafu acha yote mfuate, ama endelea kutafuta waliopotea ambao watakupoteza pia. Kwa maoni yangu your luck and in right truck.
 
Ila namwona kweli siku hizi ni mtu wa church kweli kweli na amekuwa mtu wa tofauti. Kwani ina maana hata walokole wanafanya mambo ya nanihii

......Mwambie umeacha na hautamuomba tena tgo,swala si kuokoka,amechoshwa na mchezo wako wa kumla ndivyo sivyo.............BADILIKA.
 
Mwenzio kachagua njia bora na wewe okoka afu mtokee upya afu kalipe mahari uone kama atakukukataa... pia inaelekea una katabia flani mwenzio hakapendi na hutaki kubadilika ndo mana anakwambia hata ukikoka hakutaki.... ji-angalie upya mzeiya
 
Kataka tu kuachana na wewe hichoo ni kisingizio
kweli kabisa, ni kama msichana akitaka kuachana na bf wake anajifanya kapigiwa simu na mwanamke wa huyo jamaa, yuko radhi anunue line ajittumie msg mwenyewe, nilikuwa na rafiki jirani alimfanyia bf wake hivo sasa hivi anajutia uamuzi
 
Hakuna ulokole kwa vijana ni usanii mtupu ,... !

Shame on you, vijana walio okoka wako wengi na wako strong kama huyo aliyempiga kibuti mwenzio!

............... ,nimemega walokole wengi sana !

Ulio wamega ni MA.KA.HA.BA Wenzio, nasio waliokoka. geuza njia yako chafu brother, sijui umepata nini kwa kukutana kimwili na wanawake wengi, afu unakuja kujigamba hapa jamvini... eti oooh nimemega wengi.... pumbavu sana... unatia kinyaa!
 
Back
Top Bottom