Mpenzi wangu ameamua kuokoka hataki mambo ya zamani -nifanyeje

Yeye anadai kuwa maandiko hayaruhusu uzinzi na uasherati na anasema akitaka kuolewa atamwomba Mungu ampe mme mwema. Sasa nafikiria sijui niokoke huenda Mungu akamwongoza kwangu tena. Jamani nisaidieni
Hivi mpaka hapo hujaona kuwa humfai tena? Yaani uokoke ili kumpata yeye ina maana unamfanyia mungu nitoke vipi. Ndoo maana mlokole kakustukia.
 
wadau, mi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwa sasa kaamua kuokoka na anadai maandiko hayamruhusu kufanya tena upuuzi wa zamani (yaani uasherati). Nimembebeleza na kumwambia kuwa niko tayari kuokoka ili nimpate lakini anasema hata nikiokoka uhusiano wangu na yeye hautaweza kuendelea. Na amenionya nisithubutu kuokoka kwa ajili yake na kama nataka kuokoka niokoke lakini si kwa ajili ya kumpata yeye. Anasisitiza kuwa inabidi amwombe Mungu ampe mme kutoka kwake hivyo mi ndo basi tena.

wadau hebu nisaidieni nifanyeje. Je nimuibukie huko huko church au nifanyeye maana bado nampenda na sitaki kumpoteza. :confused2:
Funga na omba utapata majibu!
 
Duh mpaka mmefika hapo kwakweli... huyo alikuwa akupendi. Maana kuokoka ni suala la iman... ni ishu ya kukaa chini na kujadiliana tu. Lakin yeye amechukulia serious..
Alikuwa anatafuta mlango wa kutokea
 
Nuru na Giza wapi na wapi, subiri umpate unayefanana nae ila huyo binti humpati ng'o kwasababu Yeye sio mzinzi tena.ameshatakaswa amesamehewa.wewe ukiamua kujiokokesha sawa yamkini ukakutana na Neema ya wokovu wa kweli ila kwa huyo binti huwezi kumpata tena
 
Back
Top Bottom