Mpenzi wangu ameamua kuokoka hataki mambo ya zamani -nifanyeje

Hiyo nyekundu siyo lazima iwe hivyo, Inawezekana aliona mapungufu katika maisha yake na hivyo ameamua kutengeneza na Bwana, miye nimeokoka kama miaka 7 sasa, siku niliyoamua kuokoka wadau wote walikuwa against me,including nyumba ndogo. Lakini that was my decision, kila mtu alisema lake lakini kwa kuwa niliamua mimi mwenyewe bila kuhubiriwa na mtu na ikawa hivyo, NA NDIVYO ILIVYO.

Wewe kwa uzoefu wako wa kuokoka miaka 7 je ni kweli kuwa hata nikiokoka kwa dhati siwezi kumpata huyu binti? na je nikweli kuwa lazima mtu akitaka koa/kuolewa kama ameokoka aombe mke/mme kwa Mungu.
 
wadau, mi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwa sasa kaamua kuokoka na anadai maandiko hayamruhusu kufanya tena upuuzi wa zamani (yaani uasherati). Nimembebeleza na kumwambia kuwa niko tayari kuokoka ili nimpate lakini anasema hata nikiokoka uhusiano wangu na yeye hautaweza kuendelea. Na amenionya nisithubutu kuokoka kwa ajili yake na kama nataka kuokoka niokoke lakini si kwa ajili ya kumpata yeye. Anasisitiza kuwa inabidi amwombe Mungu ampe mme kutoka kwake hivyo mi ndo basi tena.
wadau hebu nisaidieni nifanyeje. Je nimuibukie huko huko church au nifanyeye maana bado nampenda na sitaki kumpoteza. :confused2:
Hivi wewe unaamini kuwa maandiko yanaruhusu uasherati? Au umeamua kuyapuuza! Watu wanokoka ili kwenda mbinguni na kuanza maisha mapya ya kumpendeza Mungu, wewe unataka kuokoka ili umpate huyo dada? Huo si wokovu wa kimaandiko. Tafakari.
 
Kwa taharifa yako amempata mwanaume handsome na mwenye pesa kuliko wewe.
isitoshe amemuahidi atamwoa soon.
waangalie hawa hapa. hiyo biblia aliyoishika ni zuga tu.
hana ulokole wowote.
 
Attachments

  • bwana na bibi harusi..jpg
    bwana na bibi harusi..jpg
    23.3 KB · Views: 76
Yeye anadai kuwa maandiko hayaruhusu uzinzi na uasherati na anasema akitaka kuolewa atamwomba Mungu ampe mme mwema. Sasa nafikiria sijui niokoke huenda Mungu akamwongoza kwangu tena. Jamani nisaidieni

Narudia kusema hakukupenda; tupo wengi tulioanza kumegana na tulipofunguliwa tulirudi kwa Mungu tukatubu na tukaoana; Hivyo hata yeye ilikuwa ni rahisi kuwa pamoja na wokovu wake anaye mtu anayemthamini na angesahihisha mambo yenu kwa niaba yako;

Kinyume chake naona anakudiscourage tu nawe kwa kuwa humsomi katikati ya mistari unawka tumaini lisilokuwapo! Kubali matokeo kaka ; You will never know with women! (James Hardley Chase)nilitegemea yeye awe wa kwanza kukushawishi nawe uokoke ili mle kihalali mkiwa na ndoa yenu!

Achana nae ; jipange upya
 
Wewe kwa uzoefu wako wa kuokoka miaka 7 je ni kweli kuwa hata nikiokoka kwa dhati siwezi kumpata huyu binti? na je nikweli kuwa lazima mtu akitaka koa/kuolewa kama ameokoka aombe mke/mme kwa Mungu.

uvivu tuu! na visingizio.
Mbona mi najua kajamaa flani kalikuwa kanajifanya kameokoka..mpaka sasa kanasema kameokoka, kakakamata demu amabaye hajaokoka
Kakamlazimisha demu aokoke, demu kwa kuwa yupo desparate na alishaumizwa, akaokoka. wameoana sasa hivi. walianza kuishi pamoja (moved in) lakini wanasema hawakuwa wanakulana dudu wala nini, niambieni kama huu unaweza kuwa ukweli!!!!

Huwa nawachekaga tuu jinsi wanavyomsingizia Mungu kufanya wanayoyafanya.!
 
Wokovu wa kweli hauji kwa sababu ya kutegemea kupata kitu fulani ukipendacho sana bali ni kwa kuujua ukweli wa uwepo wa MUNGU pamoja na kutubu na kuacha dhambi. Wewe inaonekana umenogewa na penzi la huyo binti na unataka uendelee kulipata kwa gharama yeyote ikiwemo kupitia mgongo wa ulokole wa kinafiki. Ushindwe katika jina la YESU kristo aliye hai.
 
wadau, mi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwa sasa kaamua kuokoka na anadai maandiko hayamruhusu kufanya tena upuuzi wa zamani (yaani uasherati). Nimembebeleza na kumwambia kuwa niko tayari kuokoka ili nimpate lakini anasema hata nikiokoka uhusiano wangu na yeye hautaweza kuendelea. Na amenionya nisithubutu kuokoka kwa ajili yake na kama nataka kuokoka niokoke lakini si kwa ajili ya kumpata yeye. Anasisitiza kuwa inabidi amwombe Mungu ampe mme kutoka kwake hivyo mi ndo basi tena.

wadau hebu nisaidieni nifanyeje. Je nimuibukie huko huko church au nifanyeye maana bado nampenda na sitaki kumpoteza. :confused2:

mtokee mchungaji wake mtoe kidogodogo ili amwambie ameoteshwa na mungu kwamba wewe ndio chaguo lake.hapo utaua tembo kwa ubua
 
Tatizo la huyu anataka ku download na kuoa hataki.Sasa anapoambiwa mambo fulani hakuna tena ndio anapagawa.Mie nampongeza sana huyo dada.
zinaitwa trial versions alafu ataki kununua the original s/ware!
kaka binti kaokoa kweli na ameona wewe mtazamo wako wa mahusiano ni uleule wa trial version kabla ya kuinstall! Akaona utakuwa kikwazo kwake..
Sasa, kama unampenda kweli utarespect maamuzi yake na kama Mungu amekugusa na umeshawishika, okoka na wewe; ila isiwe kwa sababu yake!
Hayo mengine yote utazidishiwa!!!
 
Kwanza anastahili pongezi kwa wokovu alioupokea
Heri ya yeye alijua siri ya wokovu
nakupa pole na hongera kwa kumkosa bitnti huyo
We okoka tu kwa usalama wa roho yako na si kumpata aliyefunikwa na damu ya Yesu kwa sasa.
Hongera sana kwa kumkosa mtu ulimpotezea muda na kumchelewesha kuifaidi neema ya Kristo
 
Kwa mbali nausikia ule wimbo (Msondo au Sikinde?)

"..kukataliwa ni kuchungu, kunamfanya mtu awe na donge moyoni, utafanyaje naye kishakukataa?"

Hapo dawa kuangalia mahesabu mengine tu, hii si rizki kaka, sanasana utanunua kesi tu hapo.

Mbona watoto wazuri kibao tu? Najua mmejenga mahusiano kwa muda na mara nyingine unaona kama alivyosema Marijani Rajab

"Zuwenaaaa, nitampata wapi eeee
Zuwenaaaa, mwingine sawa na wewe
Mtoto aliyeumbika, na tabia ya kupendeza
Zuwenaaa, Zuwenaaaa kweli nampendaaaa"

Lakini ndiyo hivyo, hakuna marefu yasiyo na mwisho. Huu ni ukweli usiopingika.

Tafuta mwingine.
 
Wewe kwa uzoefu wako wa kuokoka miaka 7 je ni kweli kuwa hata nikiokoka kwa dhati siwezi kumpata huyu binti? na je nikweli kuwa lazima mtu akitaka koa/kuolewa kama ameokoka aombe mke/mme kwa Mungu.
We kaburunye, mimi naona usihangaike tena na huyo dada kama wachangiaji wengine walivyosema. Hapo mlishaanza mchezo kabla ya kuruhusiwa ambapo ni dhambi, na yeye ametambua hilo na ndio maana kaamua kumrudia Mungu. Na pengine wakati wa mahusiano yenu kuna vitu au mapungufu aliyagundua toka kwako na ndio maana anabaki na msimamo huo. Hata ukiamua kuokoka sasa hivi inaonekana ni wazi kabisa unataka kuokoka kwa lengo la kumpata yeye. Pole sana kaka. Nakushauri uokoke lakini si kwa ajili ya huyo dada, ila omba Mungu utampata mwingine pengine mzuri zaidi kuliko huyo.
 
Duh, huyo aligundua njia aliyoshika siyo(uasherati kama ulivyosema) haijalishi ameenda umbali gani akageuka, na wewe geuka upate upako wa kweli, kisha uombe sana upate mke mwema toka kwa bwana kama afanyavyo yeye, kama mmepangiwa kupanda merikebu moja mtaanza safari yenu ya ndoa salama, vinginevyo ukubaliane na matokeo.
 
Hiyo nyekundu siyo lazima iwe hivyo, Inawezekana aliona mapungufu katika maisha yake na hivyo ameamua kutengeneza na Bwana, miye nimeokoka kama miaka 7 sasa, siku niliyoamua kuokoka wadau wote walikuwa against me,including nyumba ndogo. Lakini that was my decision, kila mtu alisema lake lakini kwa kuwa niliamua mimi mwenyewe bila kuhubiriwa na mtu na ikawa hivyo, NA NDIVYO ILIVYO.

Ila mi najua kuna wanaume wanaoamuaga kuokoka baada ya kupungukiwa au kuishiwa na nguvu za kiume. Unakuta ana 'nyumba ndogo' kama tatu au nne hivi, anazipitia mojamoja kuzijulisha kuwa ati kaokoka hataki tena nanihii kumbe.......!

Na wanawake wanaookoka baada ya kufikia ile wanaita 'menopause', wapo kibao, wengine wameanzisha hadi makanisa maarufu kumbe ukisikia enzi zao utakoma!

Mimi namsifu na kumkubali anayeingia msimamo huo akiwa bado na nguvu zake kamili, lakini kwa hao wengine bado nina maswali ya mshangao.
 
Bwana YESU asifiwe,

Mada hii kwanza nimeipenda maana mimi ni mpendwa yaani nimeokoka,na mimi nimeoa,

Kwanza ninapenda kumpongeza huyo dada,kwa kufanya uamuzi ulio sahihi sana wa kutoa maisha yake kwa YESU,kwa nyakati hizi kwa Yesu kuna usalama zaidi,Pia kwa kumpa mwezie huyo wa zamani kuwa asiokoke kwa ajili yake,bali amtafute YESU wa dhati,hiyo imekaa safi.

Maana neno la Mungu limekataza vijana kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa,na inaonyesha huyu kijana mwanaume ni tabia yake kufanya tendo hilo kabla ya ndoa,ndio maana huyo dada akamkimbia,kijana wa kiume hajatulia,ukimfuata kanisani utakutana na nguvu kubwa zaidi,na labda kwa kupitia huyo msichana unaweza kumpata YESU,kuwa mwangalifu kama unataka kufanya usanii church be very careful,CHURCH is a holy place.

UBARIKIWE,Soma Yohana 3:16
 
Wewe kwa uzoefu wako wa kuokoka miaka 7 je ni kweli kuwa hata nikiokoka kwa dhati siwezi kumpata huyu binti? na je nikweli kuwa lazima mtu akitaka koa/kuolewa kama ameokoka aombe mke/mme kwa Mungu.

kubaliana naye tu, ni kweli unampenda na yeye alikupenda lakini anampenda Yesu zaidi! Muelewe tuu, utampata msichana mwingine mwenye tabia kama zako! Huyo dada kaamua kubadilika.............its a matter of dacision. Tena ukiokoka kwa sababu yake........yatakushinda! hatakubali kufanya mapenzi na wewe................ lakini ukiokoka serious bila ya kulazimishwa na m2...Mungu aweza kuwaunganisha tena.
 
wadau, mi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwa sasa kaamua kuokoka na anadai maandiko hayamruhusu kufanya tena upuuzi wa zamani (yaani uasherati). Nimembebeleza na kumwambia kuwa niko tayari kuokoka ili nimpate lakini anasema hata nikiokoka uhusiano wangu na yeye hautaweza kuendelea. Na amenionya nisithubutu kuokoka kwa ajili yake na kama nataka kuokoka niokoke lakini si kwa ajili ya kumpata yeye. Anasisitiza kuwa inabidi amwombe Mungu ampe mme kutoka kwake hivyo mi ndo basi tena.<br />
<br />
wadau hebu nisaidieni nifanyeje. Je nimuibukie huko huko church au nifanyeye maana bado nampenda na sitaki kumpoteza. <img src="/images/styles/JamiiForums/smilies/confused.gif" border="0" alt="" title="Confused" smilieid="159" class="inlineimg" />
<br />
<br />
 
Back
Top Bottom