Nifanyeje mume wangu aniamini tena?

happy amos

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
229
250
Naombeni ushauri

Nifanyeje mume wangu aniamini kama mwanzo?

Iko hivi:-

Mwanzo mwenzangu alikuwa ananishirikisha mambo yake. Ikifika mwisho wa mwezi ananiambia kimepatikana kadhaa tufanye yafuatayo.

Sikujua kama alikuwa ananishirikisha kwa kunitega au la maana alikuwa anataka robo tatu ya kipato chake awekeze kwao. Sasa akawa akiniomba ushauri namwambia nusu aweke kwao nusu inayobaki tufanye yetu kwa ajili ya familia yetu.

Kumbe nilikuwa nakosea yeye alitaka nimshauri awape zote nyumbani. Alikua kila tukikaa mipango ya maendeleo anapanga ya kwao mi nikawa namshauri asisahau na sisi ndani maana alikua hafanyi chochote kwa ajili yetu.

Mashemeji zangu wanamsumbua sana kumuomba hela, akawa ananishirikisha namwambia angalia shida yenye umuhimu umsaidie mtu, ukiona mtu anakuomba sana hela kama hana kazi mpe mtaji au mtafutie kazi.

Kumbe nilikuwa nategwa tu bila kujua. Siku hizi mwenzangu hanishirikishi kabisa mambo yake Mshahara ukitoka sijui umetumikaje na
likitokea tatizo kwao wala haniambii kama mwanzo.

Moyo unaniuma nashindwa nitairudishaje ile hali ya zamani. Nifanyeje ajue sikuwa na nia mbaya?

Naumia sana ndugu zangu mke na mume ndani hatushirikishani, hatukai tukapanga kama mwanzo kila mmoja anafanya kulingana na kipato chake na maendeleo hakuna.

Nimejaribu kuongea nae na kumuelewesha lakini kama hataki kuelewa hivi. Nisaidien nifanyeje?
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,187
2,000
Ushauri wangu.....
901aa43011f9f7be47d48119038d346d.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

google helper

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
8,443
2,000
Kuna kauli au uwasilishwaji wa mawazo mengi ya wanawake yamekaa kama dharau hasa kwa ndugu wale wanaopewa misaada kutoka kwa mume. Hivyo badili namna ya kuongea nae, japo mchango na mawazo yako yako sahihi kabisa. Utakuja kunishukuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

yellow eyes

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
2,132
2,000
Lakin ukiangalia kwa jicho la kipembuzi sana n kama vile ulikuwa hataki saaana aweke maendeleo kwao.

Kumbuka kwao ndo kuna wazaz waliomsomesha na kila kitu hd akapata na hyo kaz so cha msingi we mwache tu kwanza afanye mambo anayofanya ya kuwasaidia hao ndugu zake huenda mali zote za kwao alizimaliza yeye kipindi anasoma.
Unapoona anatoa hela kusaidia ndugu zake usiwe unaumia roho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
11,708
2,000
WAKUU,
MSISHANGAZWE NA POVU LANGU,
MIMI NDIYE MMEWE MWENYEWE (Nimem'bani haraka kwani ID Aliyotumia ina jina lake halisi,
Ila yeye alikuwa hajui ID yangu).

WEWE NI MWONGO MKUBWA,

TANGU MWANZONI NDOA IKIWA CHANGA
MAWAZO YAKO YALIJIKITA SANA KWENYE UROHO, TAMAA ZA MALI NA KUWEKA KUNYONGO PINDI MISAADA INAPOENDA KWA NDUGU HASA WALE WENYE UHITAJI KWELI.

HAKUNA MWANAUME YEYOTE TIMAMU ANAWEZA KULETA MABADILIKO HASI KWA MKE ATOAYE MAWAZO CHANYA.

ULICHOKIANDIKA HAPA UMEKIEGEMEZA KUTETEA UPANDE WAKO ILI UPATE MATH SYMPATH-
HAITOSAIDIA.

WANAUME TUKIBAINI MKE ANA ROHO MBAYA TUNAMWEKA KANDO KWENYE MAMBO YENYE TIJA-
NA HUO ND'O MSIMAMO WETU KWA MUJIBU WA KIKAO CHETU CHA MWISHO CHA MWEZI JANUARI.

NAKUONYA:
ACHA UROHO HAPPINESS,
VINGINEVYO MWENDO UTAKUWA WA JESHI LA MTU MMOJA BILA KUJALI MUSTAKABALI WA NDOA!!!

"ILA MAISHA LAZIMA YAENDELEE."
Aahaaaaaaa wewe katoto unaeishi kwa shemeji seblen umeoa lini??
 

luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
11,708
2,000
Wewe Dada kana hakuna la ziada uloficha, basi hujakosea, mmeo ana mchepuko, hawezi kuendelea kukwambia kila kitu.

Ila kama umejaribu ongea nae ikashindikana basi, nyamaza la muhimu anatoa matumizi ya nyumbani. Kama matumizi hatoi, coz hujui pesa yake inaenda wapi
1: kama uatoi matumizi ya ndani usipike
2:asipojali watoto kukosa chakula mwisho ndoa utaiona chungu
3: kwakuhofia Wenda anachepuka na wewe utatatafuta wa kukufariji
4: ndoa itakua hatarini
5:hapo ni kusuburi Mungu aingilie kati. Wanaume wanatesa sana

Ushauri:
Kama wewe una mshahara wako umejaribu kila njia kimefel achana nae, Siku akili ikimkaa atajirudi mwenyewe.

Kuna ndugu wengine wapumbavu hawataki mdugu yao afanye maendeleo .mmeo mshenzy.
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,060
2,000
Ungemleta na yeye hapa akaandika kama wewe ulivyojitetea ndo uchambuzi ukaanza hapa tutakuwa hatujamtendea haki maana hakuna maelezo yake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom