‘Mpeni Sioi ubunge mumfute machozi’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Mpeni Sioi ubunge mumfute machozi’

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by mkirua vunjo, Mar 19, 2012.

 1. m

  mkirua vunjo Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwandishi Wetu, Arumeru
  WANANCHI wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wameombwa kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Sioi Sumari ili kumfuta machozi yaliyotokana na kifo cha baba yake mzazi, Jeremiah Sumari ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

  Mbali na hilo wananchi hao wameelezwa kuwa kwa kufanya hivyo, watakuwa wamejipatia baraka kwa Mungu kwani watamwezesha Sioi kupata mshahara utakaomwezesha kuendesha familia aliyoachiwa na baba yake.

  Mwito huo ulitolewa juzi katika Kijiji cha Migadini, Kata ya Mororoni na Mbunge wa Mtera(CCM), Livingstone Lusinde alipokuwa akimnadi mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea jimboni humo.

  Lusinde alisema wananchi hao wanastahili kuwa na moyo wa huruma kwa kumchagua kwa kura nyingi ili ajipatie mshahara wa kumwezesha kumudu familia aliyoachiwa na marehemu baba yake, ikiwa ni moja ya njia ya kumfuta machozi.

  "Mkimchagua Sioi mtapata baraka za Mungu kwa vile mtakuwa mmewezesha kutokea kwa mambo matatu… kwanza kura zenu zitamfuta machozi ya kufiwa na baba yake, pili mtamwezesha kupata mshahara utakaomwezesha kulea familia yake ambayo sasa haina baba," alisema Lusinde.

  Pia aliwaambia wananchi hao kwamba kumchagua Sioi kuwa mbunge wa jimbo hilo ni kumfurahisha Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa huyo ndiye chaguo lake na ndiye aliyeongoza vikao vya Kamati Kuu iliyokutana mara mbili kupitisha jina lake kuwa mgombea wakati wa mchakato wa kura za maoni.

  Alisema katika kura hizo za maoni zilizofanyika mara mbili, zote Sioi alionekana kushinda na kuibuka kidedea.

  "Njia pekee ya kumfurahisha Rais ni kumchagua Sioi kwa kuwa ni chaguo lake, hakika mtamfurahisha na Sioi ataweza kutekeleza vyema ilani ya chama," alisema Lusinde.

  Kwa upande wake, Sioi alisema anayaelewa vyema matatizo yanayoikabili Kata ya Maroroni ikiwemo ukosefu wa mashamba ya uhakika, maji, barabara na zahanati hivyo akichaguliwa, atayatatua matatizo hayo mara moja.

  "Nawaombeni sana mnichague kuwa mbunge wenu ili kwa pamoja tuweze kushirikiana kutatua kero hizi ambazo kimsingi zote nazifahamu vyema na nafahamu pia hatua za kuchukua ili kuhakikisha tunaondokana nazo," alisema Sioi.

  Shabiki wa Chadema
  Katika tukio jingine hekima na busara za Mratibu Mkuu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba zilitumika kuepusha maafa kwa mwanachama mmoja wa Chadema, aliyevalia sare za chama hicho baada ya kufika kwenye mkutano wa CCM katika Kata ya Kikatiti.

  Wakati Mwigulu akihutubia mkutano huo, mwanachama huyo wa Chadema, ghafla alivamia mkutano huo na kuanza kupiga mayowe huku akitamka maneno ya "Peoples Power" (Nguvu ya umma).

  Hatua hiyo iliwakera wafuasi wa CCM ambao waliamua kumtia adabu kabla ya Mwigulu kuingilia kati kuwazuia akiwataka wamwache kwani alikuwa anapaswa kufundishwa sera za CCM.
   
 2. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Duh! Mbunge anawaza mshahara tu? kwahiyo wanamchagua ili aweze kukimu mahitaji yake ya kimaisha!
   
 3. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hii ni comedy au???????
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hebu someni tena hicho kipande kwenye blue. Naona kama kuna hila ya kumhujumy Sioi, au Lucinde anaugua ugonjwa ambao bado haujajulikana!
   
 5. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Ubunge si fadhila wala kufutana machozi.Hawa CCM kwani wanakula nini hawa wenzetu?!
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nimeachwa hoi niliposikia kauli chafu ya aina hiyo leo.
  Hakika hii ni mbinu ya wabaya wa Sioi kumfanya aonekane ni ombaomba.
   
 7. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duuu Mh. Lusinde kweli sera zimekwisha kabisa huko CCM....... Kura za kumfuta machozi????? agrrrrrrrrr..
   
 8. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Hotuba hii ingefana sana siku ya sikukiu ya R.I.P akili ya Job Lusinde!
   
 9. w

  wikolo JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kama mtu anatakiwa kuchaguliwa ili akapate mshahara wa kujikimu yeye na familia yake basi haina maana. Hivi haya matatizo ya huko arumeru mashariki amabyo CCm wanayahubiri sasa na kuahidi kuyatatua kupitia Sioi yalikuwa hayaonekani miaka yote wao wakiwa wanaongoza hilo jimbo? Kwa kweli ukiambiwa kitu jaribu kuchanganya na za kwako!!
   
 10. m

  mbwagison Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli Lusinde ni kibajaji tulichoahidiwa na presidaa! Nimemkumbuka sana tingatinga! Poleni wanamtera wote,huyu ndo mbunge wenu!
   
 11. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa wameishiwa la kuzungumza mbele ya wananchi, ina maana Mtanzania atakayefariki akiwa kwenye utumishi wa umma nafasi yake apewe mtoto ili aweze kuendelea kutunza familia hiyo? Job Lusinde alikuwa balozi lakini kijana wake anayesema maneno hayo hajapewa nafasi hiyo, matokeo yake yeye alimg'oa baba yake Mzee John Malecela kwenye nafasi ya ubunge akaichukua yeye na sijui familia ya baba yake aliyefanya kampeini kumuondoa kwenye nafasi hiyo anaionaje aulizwe Lusinde.
  Kama familia ni ya katibu mkuu akifariki mtoto apewe nafasi hiyo ili atunze familia yao? acheni kupotosha umma wa Arumeru Mashariki nyie CCM ongea yenye mantiki. Angalia penye wekundu
   
 12. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CCM kweli wameishiwa. Nikiwa mdogo sikuwahi kuona kiongozi wa CCM mwenye uwezo mdogo wa kuzungumza kama LUSINDE. Huku ni kuwatukana hata watu waliomsaidia kumchakachua Mzee Malecela hili yeye apate nafasi. maskini chama hichi Kikongwe
   
 13. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Very goo CCM, sasa hamfichi ujinga wenu. Kwa hiyo ubunge sasa umekuwa fadhila kwa mtu kupewa ili afute machozi ya kufiwa na baba yake, loh!

  Ngoja na mimi niende UN nikadai kurithi ofisi ya marehemu baba yangu. Kumbe ndio maisha simpo namna hii kama baba aliacha ofisi
   
 14. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Hotuba hii ingefana sana siku ya sikukuu ya wajinga R.I.P akili ya Job Lusinde
   
 15. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uwezo wake wa kuzungumza sio mdogo, ni mkubwa hasa. Alichopungukiwa ni uwezo wa kufikiri, lkn hata hivyo sio shida sana ndani ya CCM. Siasa za CCM hazihitaji akili, ni mdomo na tumbo tu.
   
 16. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa na wewe umekuja kumueleza nani humu JF mambo yako?
   
 17. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa akili kama hii mtu ataache kusinzia Bungeni kweli??? Hawa ndiyo vijana wanaotegemwa na Magamba katika kuikomboa nchi hii, kazi kweli kweli.
   
 18. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lakini hizi ndio hoja zilizobakia kwa CCM. Hata mkuu wao anaongea maneno yanayofanana na haya ni kwa vile watu hawayachambui kwa kina. Baada ya kupitishwa kwa Dr. Shein kugombea uraisi wa Zanzibar mwaka 2010 alisema haya, wengine mliokosa ni wadogo, wengine mna uwezo lakini kura hazikutosha, tutawapa kazi nyingine.... Hii sentensi ni ya KEPEANA. Lakini wakati wabunge wa CHADEMA walipotoka bungeni, alisema MAMBO YAO TUTAYAPITISHA SISI, POSHO TUTAZIPITISHA SISI, kwa hiyo lazima warudi kwa sababu wanatuhitaji, hii kauli ukiichambua kiundani haina UWAJIBIKAJI ndani yake bali ULAJI
   
 19. kwelwa

  kwelwa Member

  #19
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WANANCHI WA ARUMERU WATAMCHAGUA SIOI IKIWA BABA YAKE ALIWALETEA MAENDELEO KATIKA JIMBO AMBALO LINAONEKANA KUWA NA KERO NYINGI AMBAZO ZIMESHINDWA KUPATA UFUMBUZI KAMA AMBAVYO AHADI ZA JAKAYA ZILIVYOSHINDWA KUTATULIWA.KIMSINGI WANANCHI WANA KILA SABABU YA KUTAFAKARI SANA ,NA SI KUCHAGUA ETI KUPATA MSHAHARA WA KUSUSTAIN FAMILIA.ACTUALLY THEY ARE WELLOFF.:scared::lock1:
   
 20. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  I've heard so much nonsense in my life, but they weren't as nonsensible as this.
   
Loading...