‘Mpeni Sioi ubunge mumfute machozi’

Ebo!, yaani tumfute machozi kwa kumpa kura?. Kwanini hajatulia nyumbani arobaini iishe ya mzazi wake?. Halafu huyo Lusinde akili yake inabebeka kwenye kiganja. Awe anatafuta maneno ya kuongea...kwa mfano tumpe kura ili akapate mshahara. Hatujagui watu kwenda bungeni wapate mshahara! Kuna mtu amenidokeza kwamba Sioi katika mazishi ya babake hakutoa hata tone la chozi. Au ndio tuseme alikua analia kiume?
 
Mwandishi Wetu, Arumeru
WANANCHI wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wameombwa kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Sioi Sumari ili kumfuta machozi yaliyotokana na kifo cha baba yake mzazi, Jeremiah Sumari ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

Mbali na hilo wananchi hao wameelezwa kuwa kwa kufanya hivyo, watakuwa wamejipatia baraka kwa Mungu kwani watamwezesha Sioi kupata mshahara utakaomwezesha kuendesha familia aliyoachiwa na baba yake.

Mwito huo ulitolewa juzi katika Kijiji cha Migadini, Kata ya Mororoni na Mbunge wa Mtera(CCM), Livingstone Lusinde alipokuwa akimnadi mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea jimboni humo.

Lusinde alisema wananchi hao wanastahili kuwa na moyo wa huruma kwa kumchagua kwa kura nyingi ili ajipatie mshahara wa kumwezesha kumudu familia aliyoachiwa na marehemu baba yake, ikiwa ni moja ya njia ya kumfuta machozi.

“Mkimchagua Sioi mtapata baraka za Mungu kwa vile mtakuwa mmewezesha kutokea kwa mambo matatu… kwanza kura zenu zitamfuta machozi ya kufiwa na baba yake, pili mtamwezesha kupata mshahara utakaomwezesha kulea familia yake ambayo sasa haina baba,” alisema Lusinde.

Pia aliwaambia wananchi hao kwamba kumchagua Sioi kuwa mbunge wa jimbo hilo ni kumfurahisha Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa huyo ndiye chaguo lake na ndiye aliyeongoza vikao vya Kamati Kuu iliyokutana mara mbili kupitisha jina lake kuwa mgombea wakati wa mchakato wa kura za maoni.

Alisema katika kura hizo za maoni zilizofanyika mara mbili, zote Sioi alionekana kushinda na kuibuka kidedea.

“Njia pekee ya kumfurahisha Rais ni kumchagua Sioi kwa kuwa ni chaguo lake, hakika mtamfurahisha na Sioi ataweza kutekeleza vyema ilani ya chama,” alisema Lusinde.

Kwa upande wake, Sioi alisema anayaelewa vyema matatizo yanayoikabili Kata ya Maroroni ikiwemo ukosefu wa mashamba ya uhakika, maji, barabara na zahanati hivyo akichaguliwa, atayatatua matatizo hayo mara moja.

“Nawaombeni sana mnichague kuwa mbunge wenu ili kwa pamoja tuweze kushirikiana kutatua kero hizi ambazo kimsingi zote nazifahamu vyema na nafahamu pia hatua za kuchukua ili kuhakikisha tunaondokana nazo,” alisema Sioi.

Shabiki wa Chadema
Katika tukio jingine hekima na busara za Mratibu Mkuu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba zilitumika kuepusha maafa kwa mwanachama mmoja wa Chadema, aliyevalia sare za chama hicho baada ya kufika kwenye mkutano wa CCM katika Kata ya Kikatiti.

Wakati Mwigulu akihutubia mkutano huo, mwanachama huyo wa Chadema, ghafla alivamia mkutano huo na kuanza kupiga mayowe huku akitamka maneno ya "Peoples Power" (Nguvu ya umma).

Hatua hiyo iliwakera wafuasi wa CCM ambao waliamua kumtia adabu kabla ya Mwigulu kuingilia kati kuwazuia akiwataka wamwache kwani alikuwa anapaswa kufundishwa sera za CCM.

Tukifika mahala pa kupeana majukumu ya kitaifa kama fadhila basi taifa limeangamia. Tumehama kwenye sifa na vipaumbele vya msingi kama kigezo cha mtu kuchaguliwa, tumehamia kwenye ushikaji na fadhila.
 
CCM wameshindwa sera, sasa wanaomba huruma ya wana Arumeru Mashariki. Ni aibu sana eti Sioi apate mshahara wa kulea familia, kwa hiyo ishu si kero za wananchi bali ni Kufuta machozi, kutunza familia na Kumfurahisha Mk..were,Dah ukistaajabu ya Mkapa utayaona ya Lusinde!
 
Nataka kujua CCM wanatumia vigezo gani kupata majina ya wapiga kampeni wake.
Kwa kweli kumtaka Lusinde na wenzake wengi watafakari kabla ya kunena ni kuwaonea .Wapiga porojo ndani ya ccm wamegawanyika katika makundi makuu mawiIi:kundi la kwanza ni lile linalojumuisha ndugu zetu waliopata bahati ya kwenda shule isipokuwa baada ya kuwa ktk tabaka tawala na nyonyaji wamejikuta wamelewa chakari mvinyo wa madaraka...kundi la pili ni wale wenzetu ambao hawakupata kabisa bahati ya kukaa madarasani kujipatia maarifa na ustaarabu unaoambatana na mchakato huo.
Kwa wale waliokatika kundi la kwanza wanaweza kurejesha uwezo wao wa kufikiri iwapo tu watabadili nia zao na kuachana na siasa za ghiliba wanazoziamini na kuzifuata..wale wote wanaoangukia ktk kundi la pili(hapa ndipo alipo Lusinde) habari njema kwao ni kuwa elimu haina mwisho...wanaweza kujiunga na kisomo cha watu wazima au waanzishe mchakato wa kurekebisha sheria bungeni ili waruhusiwe kupata elimu rasmi darasani na wadogo au watoto wao kama wafanyavyo jirani zetu Kenya.
 
Lusinde is stupid. Atasemaje sumari apewe ubunge ili apate mshahara wakuhudumia familia. Anaenda kwa maswala yake binafsi na sio ya jimbo. Ameniudhi na wengine ambao wazazi wote hatuna na hata uwezo hatuna tukagombee wapi ubunge? Nimekasirika sana let him put his $$$$SSS down.
 
The only word 2 tell lusinde is not to tell talk $$$it. How can he say like dat? Hata ambaye hakusoma hawezi kumfanyia kampeni hivyo. Sio kutatua matatizo ya jimbo Bali ya kifamilia. Huyo kijana ajibu hayo matusi.
 
The guy is disgrace, I wonder how he was elected an MP! that can only happen in Tz! Mbowe was right, One Chadema MP is equal to 30 CCM MP! Lusinde has justified that!
 
Lusinde is stupid. Atasemaje sumari apewe ubunge ili apate mshahara wakuhudumia familia. Anaenda kwa maswala yake binafsi na sio ya jimbo. Ameniudhi na wengine ambao wazazi wote hatuna na hata uwezo hatuna tukagombee wapi ubunge? Nimekasirika sana let him put his $$$$SSS down.

Unashangaa nini wakati Lusinde yuko pale kwa ajili ya mshahara, maana anajua arudi kipindi cha pili
 
Nimekuwa nikiuona huu uzi nahisi kupasuka kifua, nakosa hata cha kuandika kwa kweli, kama kuna kitu kimepata kuniskitisha katika siku za usoni basi maneno ya huyu mheshimiwa yanaongoza, nashindwa kuamini kama mbunge wa chama changu hiki anaweza simama mbele ya halaiki ya watu waliokosa matumaini na kuongea UTUMBO kama huu.....hizi AK47 zitakapoingia mitaan 2tashuhudia mengi
 
duuu mh. Lusinde kweli sera zimekwisha kabisa huko ccm....... Kura za kumfuta machozi????? Agrrrrrrrrr..

ukitaka kujua busara na akili ya mtu chunguza maneno yake ayaongeayo kwa watu. Msipate shida sana kumjadili lusinde huo ndio upeo wake kifikra
 
Unashangaa nini wakati Lusinde yuko pale kwa ajili ya mshahara, maana anajua arudi kipindi cha pili

tuachane na mambo ya kurudi au kutorudi, ni dharau na matusi ya wazi kwetu kuambiwa tumchague mtu eti kisa kafiwa na baba yake. Wangapi wamefiwa? Wakitaka ubunge watatosha? Ina maana hawana lengo lolote la kuendeleza nchi hii zaidi ya kutaka mishahara wakaendeshe hizo familia zao? Wananchi wangapi hawana mshahara na wanaendesha familia zao? Lakini kwa sababtt aliyewaroga wananchi alishakufa watawapa kula!
 
Elimu ya LUSINDE

lusinde.JPG
 
Yaan mie hasira nlizokuwa nazo dhidi ya upu**avu wa huyu jamaa nahisi kifua kinataka kupasuka....eti "mkimchagua mtamfurahisha Rais maana ndilo chaguo lake" najiuliza hivi ni kweli huyu ni mbunge wa chama changu!!!
 
Kwani kazi ni ubunge tu? si akashike jembe alishe familia? alaah! Huyu jamaa ni punguani kweli...!
 
watu wa Arumelu walikuwa labda na nia ya kumchagua bw. Sioi lakini kwa kauli hizi watu watadharau.

Hii inadhiirisha hawa CCM wameishiwa (wamezidiwa kete) kiasi gani na haya ndio mawazo ambayo wameyatumia siku zote kuleta umasikini nchi hii, thank God leo tunapata kujua haya!
 
ccm kingemuwekea magumashi kumpitisha mzee nyc, ilikuwa lusinde ahamie cdm na kulinyakua jimbo la mtera kwa ticket ya cdm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom