‘Mpeni Sioi ubunge mumfute machozi’

‘Mpeni Sioi ubunge mumfute machozi’

Hivi jamani nikisema kuwa ccm ni janga la taifa mtakataa?
Tangu lini ubunge umekuwa ni kifuta machozi?eti aonewe huruma these people are nat serious at all.Wanajali matumbo yao, angekuwepo mwalimu angesema hawa kina lusinde waogopwe kama ukoma.
 
Duh!kwahiyo siku hizi ubunge unafariji ee!i thought kuwa nia ni kuwatumikia wananchi!kumbe ni njia za watu kujipatia kipato chao na familia zao??tajiri anafutwa machozi kwa ubunge!vipi masikini wasio na chochote wanaolala njaa au kuishia kula mlo mmoja wanafutwa machozi na kitu gani??halafu bila hata aibu mbunge mzima anasimama kumuombea mtu kura kwa style hiyo? ooh!poor Tanzania!
 
Mwandishi Wetu, Arumeru
WANANCHI wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wameombwa kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Sioi Sumari ili kumfuta machozi yaliyotokana na kifo cha baba yake mzazi, Jeremiah Sumari ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

Mbali na hilo wananchi hao wameelezwa kuwa kwa kufanya hivyo, watakuwa wamejipatia baraka kwa Mungu kwani watamwezesha Sioi kupata mshahara utakaomwezesha kuendesha familia aliyoachiwa na baba yake.

Mwito huo ulitolewa juzi katika Kijiji cha Migadini, Kata ya Mororoni na Mbunge wa Mtera(CCM), Livingstone Lusinde alipokuwa akimnadi mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea jimboni humo.

Lusinde alisema wananchi hao wanastahili kuwa na moyo wa huruma kwa kumchagua kwa kura nyingi ili ajipatie mshahara wa kumwezesha kumudu familia aliyoachiwa na marehemu baba yake, ikiwa ni moja ya njia ya kumfuta machozi.

“Mkimchagua Sioi mtapata baraka za Mungu kwa vile mtakuwa mmewezesha kutokea kwa mambo matatu… kwanza kura zenu zitamfuta machozi ya kufiwa na baba yake, pili mtamwezesha kupata mshahara utakaomwezesha kulea familia yake ambayo sasa haina baba,” alisema Lusinde.

Pia aliwaambia wananchi hao kwamba kumchagua Sioi kuwa mbunge wa jimbo hilo ni kumfurahisha Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa huyo ndiye chaguo lake na ndiye aliyeongoza vikao vya Kamati Kuu iliyokutana mara mbili kupitisha jina lake kuwa mgombea wakati wa mchakato wa kura za maoni.

Alisema katika kura hizo za maoni zilizofanyika mara mbili, zote Sioi alionekana kushinda na kuibuka kidedea.

“Njia pekee ya kumfurahisha Rais ni kumchagua Sioi kwa kuwa ni chaguo lake, hakika mtamfurahisha na Sioi ataweza kutekeleza vyema ilani ya chama,” alisema Lusinde.

Kwa upande wake, Sioi alisema anayaelewa vyema matatizo yanayoikabili Kata ya Maroroni ikiwemo ukosefu wa mashamba ya uhakika, maji, barabara na zahanati hivyo akichaguliwa, atayatatua matatizo hayo mara moja.

“Nawaombeni sana mnichague kuwa mbunge wenu ili kwa pamoja tuweze kushirikiana kutatua kero hizi ambazo kimsingi zote nazifahamu vyema na nafahamu pia hatua za kuchukua ili kuhakikisha tunaondokana nazo,” alisema Sioi.

Shabiki wa Chadema
Katika tukio jingine hekima na busara za Mratibu Mkuu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba zilitumika kuepusha maafa kwa mwanachama mmoja wa Chadema, aliyevalia sare za chama hicho baada ya kufika kwenye mkutano wa CCM katika Kata ya Kikatiti.

Wakati Mwigulu akihutubia mkutano huo, mwanachama huyo wa Chadema, ghafla alivamia mkutano huo na kuanza kupiga mayowe huku akitamka maneno ya "Peoples Power" (Nguvu ya umma).

Hatua hiyo iliwakera wafuasi wa CCM ambao waliamua kumtia adabu kabla ya Mwigulu kuingilia kati kuwazuia akiwataka wamwache kwani alikuwa anapaswa kufundishwa sera za CCM.

Hivi hawajamaa wanatuchukuliaje?
 
Mpeni Vicent Nyerere urais kumfuta machozi ya hayati J.K.Nyerere, Lusinde fungua kichwa acha kuongea vapour na safari hii tembea uchi , babako alikuwa balozi nk kwa taarifa yako watu kibao wanaweza kuongoza
 
Huyu Lusinde si ndiye aliyewahi kushauri kuwa Bungeni wapelekwe madaktari kupima wabunge akili...nafikiri alikuwa sawa maana alijua akili zake si sawa!
 
CCM wameshindwa kuwafuta machozi wananchi wa kawaida kwa angalau kuwapa haki zao na mahitaji yao ya kikatiba(ajira endelevu,elimu bora,matibabu n.k) wao wanataka kufutana machozi kwa kupeana ubunge!!!
Kweli aliye nacho anaongezewa na asiye nacho hata kile kidogo chake ananyang'anywa kwa masilahi ya aliyenacho.
Kama Sioi hana vigezo hapaswi kuwa mbunge kwa sababu tu ya sentiment kutoka kwa wananchi eti kwa sababu amefiwa na mzee wake ..Period.Wangapi wamefiwa na wazee wao na bado wanapigana na maisha kwa kutafuta kwa jasho lao na sio kuonewa huruma na mtu yeyote!!???
 
Huyu naye ameenda kumpigia kampeni mgombea kwa kauli hizo?!! Magamba kwisha!
 
sijawahi kuona mijitu mipunguwani kama viongozi hawa wa CCM?? tumfute machozi? si aende akachukue shares za babake CRDB bank alee hiyo familia ..babake ana 13% ya share za CRDB Bank kwani hazitoshi hizo kulea familia?
 
Hawa jamaa wameishiwa la kuzungumza mbele ya wananchi, ina maana Mtanzania atakayefariki akiwa kwenye utumishi wa umma nafasi yake apewe mtoto ili aweze kuendelea kutunza familia hiyo? Job Lusinde alikuwa balozi lakini kijana wake anayesema maneno hayo hajapewa nafasi hiyo, matokeo yake yeye alimg'oa baba yake Mzee John Malecela kwenye nafasi ya ubunge akaichukua yeye na sijui familia ya baba yake aliyefanya kampeini kumuondoa kwenye nafasi hiyo anaionaje aulizwe Lusinde.
Kama familia ni ya katibu mkuu akifariki mtoto apewe nafasi hiyo ili atunze familia yao? acheni kupotosha umma wa Arumeru Mashariki nyie CCM ongea yenye mantiki. Angalia penye wekundu


Huyu Lusinde is a Joke.......kwa kweli...naungana nawe kumshangaaa.......yaani wamegeuza ubunge au utumishi wa umma ni rambi rambi....sasa kama ndivyo leo hii ..Makongoro angekuwa rais kwa sababu ya kuwapooza kwa kifo cha baba yao.........
Joseph Sokoine angekuwa waziri mkuuu .....Na Vita kawawa angekuwa makamu mwenyekiti wa ccm
 
sijawahi kuona mijitu mipunguwani kama viongozi hawa wa CCM?? tumfute machozi? si aende akachukue shares za babake CRDB bank alee hiyo familia ..babake ana 13% ya share za CRDB Bank kwani hazitoshi hizo kulea familia?

kweli nimekumbuka ...yeye anawaza mshahara wakati Sioi ameridhi mabilioni ya pesa za baba yake,hisa makampuni mbali mbali ...na kampuni ya ushauri wa mitaji na fedha..SOLOMON SECURITIES anafikiri ni mwenzake huyo!!!..the guy is filthy rich..yet kaoa "royal family" kwa lowasa ....another tycoon ...kwa kifupi ukishanganya utajiria wa sioi na mkewe na proceed toka kwa baba zao....kibongo bongo ....wao na wajukuu kama wakijaaliwa wanaweza kukaa na kula maisha yao yote
 
kuomba kura kwa kutegemea huruma ya wananchi eti kwa kuwa ametoka kufiwa na baba yake ni ujinga mtupu na utumishi wa umma hauwi hivyo. Kwanza wanataka tumchague ili akapate mshahara hawa jamaa kweli ni wajinga sanaaaaaaaaaaaaaa
 
Kweli Lusinde ni kibajaji tulichoahidiwa na presidaa! Nimemkumbuka sana tingatinga! Poleni wanamtera wote,huyu ndo mbunge wenu!

Hivi ulifikiri alipojiita kibajaji ilikuwa utani?
Jamaa ni kibajaj kweli, akili yake finyu kama injini ya bajaji.
Kutoka Dar hadi Chalinze kibajaj kinatumia masaa kumi plus vituo sita vya mapumziko.
 
Msimshambulie Lusinde jamani, muoneeni huruma, Akili yake haipo sawa.., ni mgonjwa yule..:scared:
 
He! Kama hizi ndo fikra za viongozi wetu basi tufwile mnyambala!!
Ndio kusema sera zimewaishia au?
 
ni uzandiki usio hitaji ata elimu ya chekechea, ata asinge sema ilishaeleweka...
 
Back
Top Bottom