Mpango wa kukamata daladala za wanachadema umeanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpango wa kukamata daladala za wanachadema umeanza

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Godwine, Mar 30, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwa kifupi kuna agizo kutoka chama cha CCM kwa jeshi la polisi ili kuwakomoa wanaharakati wa Chadema wanaomiliki mabasi ya Usafirishaji katika jiji la Dar es salaam
  na mpango huo umeanza toka jana na utakuwa endelevu . Kwahiyo kwa wanaharakati mjipange kufirisika au kujisalimisha kwao nao wafanye wanachokitaka
   
 2. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  sasa watajuaje kuwa daladala flani linamilikkiwa na mtu wa chadema??... Hata ivyo, sio swala la kuwaambia watu wa chadema wajipange kufilisika, bali waweke vizuri daladala zao na wahakikishe wanafuata sheria zote za barabarani na madereva wao kuwa makini na kuwa na vifaa vyote necessary vinavyotakiwa katika gari...eg fire extinguisher, necessary stickerz n.k
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  katika kila wajumbe wa nyumba kumi watapeleka majina ya wananchi wao na namba za daladala za wanachama ambao si za wanaCCM na kisha chama kitawasilisha kwa polisi nao wataanza kuzifanyia kazi. kwa mfano kwa jiji la dar es salaam Dala dala inakamatwa kwa kosa la abiria kutofunga mkanda. jamii yote tunafahamu ya kuwa kutofunga mkanda kwa abiria ni kosa lakini je ili agizo linatekelezeka kwa mazingira ya Kitanzania kwani kutokana na Idadi ya abiria unakuta watu wamesimama je ufungaji mkanda utaendana mpaka abiria waliosimama? na kama hili ni kosa basi lifanyike kwa Dala Dala zote na si kukamata 20 au kumi kwani wakazi wa dar pindi tunapotumia daladala tunaona karibu zote hazina mikanda na wakati mwingine watu wanajaa na kusimama
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ukawa na daladala bovu halafu likamatwe unasingizia eti wewe Chadema? Katika hilo hata Mh. Mbowe hatakutetea!
  Nyie wekeni magari yenu katika hali nzuri halafu tuone nani atamwonea mtu.
   
 5. G

  Godwine JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kukamatwa kwa dala dala hakutokani na ubovu wa dala dala pekee kuna mambo mengi ikiwemo kutotoa hesabu ya matrafiki kila siku gari hizi wanapeleka kati ya 5000 na 100000 kwa mapolisi wazilinde uwe na kosa au usiwe na kosa
   
Loading...