Mpangaji wangu kashindwa kunilipa kodi

Kama vipi we mtafune huyo mke wa huyo jamaa ujipoze, yaani anakuandikia hadi SMS hujiongezi tu mkuu!! unafeli sana ningekuwa katika position yako nishakula kitumbua zaman!!
 
kaka umesema maneno magumu mno, ila kumbuka nimewavumila mno mwaka wa pili sasa jamani...kweli? yaani hela ya kodi miaka miwili
Kama umeweza kuvumilia miaka miwili sina shaka na moyo wako kwa kuwa najua ni mzuri,hivyo kwa uvumilivu huo huo nakuomba usichoke kutenda wema huo zaidi kwa kuwa hajagoma lakini ni hali tu ngumu kwake.
 
Kama binti anasoma shule ambayo wanaruhusu mtoto kuwa na simu ya kuchati na baba mwenye nyumba, hiyo familia ni ya kutimulia mbali.
 
ubarikiwe mkuu watu kama wewe ni wachache sana🙏🙏🙏
 
Unawadai kodi kiasi gani mhenga?
 
kama huwa haupatagi shida za kuomba Msaada watimue tu...
Ila kama na wewe unapataga shida mpaka unahitaji ndugu jamaa wakusaidie, Wavumilie tu...
Shida ni Rafiki tunaeishi nae kwenye dhiki...
 
Timua haiwezekani mtu umefulia alafu bado anakomaa kupanga nyumba ya kodi ya laki 3 kwa mwezi kuna watu wanapokea milioni kwa mwezi lakini wanaishi nyumba ya chini ya 200000

Hao bado hawajakubaliana na hali tena unaweza kukuta wanamiliki na chombo cha usafiri na kufanya outings kama.kawaida. pia utakuta kwenye vikao vya harusi wao ni wanakamati na wanatoa madau makubwa.

Mimi nimepatwa na majanga kibao yaani hao wapangaji wanakuchukulia poa sana Tena wameajiriwa mke na mme. Ata shetani ana majaribu mkuu usizani upole ndio tiketi ya kwenda peponi ama ukali ni tiketi ya kwenda motoni nazani pepo la umasikini linakuandama wafuatilie kwa akili zaidi kuliko hisia huenda ata apajamii forum wapo.....haikuwa vema kutaja taarifa zao sahii kama kidato cha mtoto ungesema ata yupo form two .....kama hawajakuloga kuwa makini kwenye kudai chako unaweza kupoteza vingi kimchezo mchezo bila kujua mwanzo wala mwisho.
Sitaki kusema huo mkasa kwani sio lazima na wewe mwisho wako uwe vile inaweza isitokee ukafanikiwa zaidi amaukabaki kama ulivo ama kisibadilike chochote uwe umepata tu story ya kusimulia mbeleni ama wewe ndio uje kuwa story ya kusimuliwa huko mbeleni
 
UNAAMUA KUWAHURUMIA NA KUA NA UTU, unawavumilia mwisho wa siku wanakuja kutoroka na kwenda kupanga kwingine na kodi wanalipa. Binadamu sisi tuna hatari sana.

MAONI YANGU: Naomba uwahurumie na kuwasaidia kwa changamoto wanayoipitia pia kama itakupendeza dai nusu ya kodi unayodai
 
Unawadai Pesa Ndefu Sana,kama Vp Jimilikishe Huyo Binti Ili Ijulikane Unakaa Na Ndugu Zako!!
 
FUSO,

Serikali inadaiwa trilioni 43 na haijauzwa, na wewe unadai visenti unabwatuka, kuwa na utu kama serikali
 
kaka Maisha ni SIASA na ndiyo maana kila nikiwadai wananijibu siasa tupu - ndo nimekuja hapa mnipe ushauri ila sitaki ushauri wa kisiasa.
Waambie walipe mwezi mmoja mmoja kila mtu ana matatizo yake
 
Nyumba yako,umejenga kwa pesa zako bado ushauri kwetu,be serious mkuu NB: zingatia utu pia
 
kaka pango ni Sh 300,000 kwa mwezi, kwa mwaka ni Tsh 3,600,000 kwa miaka miwili ni 7.2m. ni hela nyingi sana wakuu.
Mkuu wape notisi miezi mitatu tu nyumba ya laki 3 mtu mwenye shida hapamfai hapo waambie wasogee nje ya mji kuna vyumba hadi vya 25k wahamie huko.
Kama umewabeba 2yrs mkuu its enough.
 
Huenda hata nyumba huna unalala kwa shemeji yako
 
Ohoooo kumbe huwezi kusamehe mkuu?
 
Yani maisha magumu sn.Me mwenyewe hapa nadaiwa balaa pango ila mwenye nyumba kaelewa Na ameniacha tu maana pamoja na kuwa ana ukwasi ila anakumbuka alikotoka kulikuwa kugumu sana.Nawaza hapa nianze punguza deni kwa kasi mpaka liishe.Mungu atanisaidia.
 
Wameamua na wamefanikiwa kuishi bure. Nilifikiri hawana kazi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…