Mpanda: Wananchi wakerwa kutogawiwa mashamba mapema

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464

Wakazi wa Vijiji vya Matandalani na Mtisi vilivyopo Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wamekerwa kwa kucheleweshwa kugawiwa mashamba mapema ambapo wamekuwa wakiahidiwa na Ofisi ya Ardhi kwa lengo la kutekeleza zoezi hilo lakini utekelezaji unasuasua ambapo maeneo hayo yalirejeshwa kwa Wananchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Fortunata Katula, Frank George Magamba Makishali na Juma Kalugutu ni baadhi ya Wananchi wa Vijiji hivyo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisubiri zoezi la ugawaji mashamba lakini utekelezaji unachelewa.

Damas Ngassa ni Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Nsimbo amesema mbali na kuchelewa kutekeleza zoezi hilo la ugawaji mashamba lakini ofisi ya ardhi iko tayari kutekeleza zoezi hilo.

Mkuu wa Wilaya, Jamila Yusuf amekerwa kwa kutofanyika zoezi hilo la ugawaji mapema ambapo amelazimika kuagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi ili kubaini kikwazo cha kutotekeleza zoezi hilo mapema na kwa yeyote atakayebainika kuchelewesha zoezi hilo rungu la Sheria litamuangukia.

Ikumbukwe kuwa maeneo hayo yalikuwa hifadhi ya Msitu wa Kijiji lakini Rais aliyarejesha kwa Wananchi ili wagawiwe kwa akili ya shughuli za kilimo.

#Bugoma Wa Bugoma
Katavi.
 
Back
Top Bottom