Mpaka sasa sijui sababu ya kuachwa

mtakahela

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2016
Posts
801
Reaction score
1,268
Habari zenu wakuu

Nimevumilia ila nimeshindwa nahitaji msaada wenu huyu baharia mzee nimfanye nini .
Maana aliyonifanyia nahisi hata nikisema ni move on sitaweza natamani na mie nimfanyie kitu cha aibu na fedheha kama alivyofanya kwetu

Uhusiano wangu na huyu baba umedumu kwa mwaka mmoja na miezi kadhaa. Na tulivyokua pamoja tulipanga mengi kwa muda mfupi ili hata huko mbeleni kila mmoja aweze kusimamia majukumu yake kama baba au mama

Alinitamanisha tufanye biashara pamoja hivyo na yeye awe msimamizi wangu. Sikua na hela ya kutosha ikanibidi niongee na mama nikamuelezea kila kitu akanipatia pesa, nikampa baharia apige kazi.

Hapo sikua na wasiwasi maana jamaa ni mtu wa dini, kanizidi miaka mingi na pia anajiweza kwa biashara zake na nyumbani tayari anajulikana kama mtarajiwa

Mwezi wa sita mwaka huu alifiwa na mama yake tukaenda kuzika ila arobaini mie sikuweza kwenda.
Hatukukaa sawa akafiwa na babu yake mzaa mama yake.

Basi tangu hapo mawasiliano yamekua ya shida maana mwenzangu alikua hafanyi chochote cha kuingiza pesa. Kila siku ananiomba nimtumie pesa. Nikamuuliza hivi kama tungekua tunaishi pamoja na tuna watoto ingekuaje kama wewe hutaki kujishughulisha. kwamba tangu mwezi wa sita mpaka leo bado unaomboleza tu? Basi akawa kimya ukimpigia anasema alikua busy na shughuli za nyumbani na kama siamini nimpigie shangazi yake.

Sasa hivi mimi na yeye tumeachana kwa sababu ambazo hazieleweki maana hata nikimpigia simu tuongee yetu mimi na yeye hataki tuongee. Mwezi sasa hakuna meseji wala simu kupigiana.

Sasa mie nawaza nifanye kitu gani aumie zaidi yangu kwa maana kama kunila kanila sana, kuanzia kipochi manyoya mpka kipochi mapesa. Nyumbani ndio hivyo nimeshamtambulisha yeye na sasa hivi hata nikiulizwa sina la kujibu

Naombeni msaada wa mawazo nifanye kitu gani na yye ahisi maumivu ninayoyapata.

Shukrani

MICHANGO YA WADAU:
=====
====
=====
=====
=====
=====
 
Maisha yana mambo mengi sana. Usikute unamlaumu hapa naye kule anamlaumu mtu mwingine.

Wanaume wengi wanaowaumiza wanawake walishaumizwa na wanawake fulani walichonacho kichwani ni wanawake walewale. Tatizo kubwa zaidi hatuna utamaduni wa kuongea hisia zetu hili ni hatari sana maana nihisivyo na uhisivyo ni tofauti na hatuambizani.
 
pole sana...just move on ndugu yangu kulipiza kisasi hakisaidii cha msingi we muombee huko alipo aishi kwa aman na furaha...Fanya mambo ya kimaendelea am sure kama akija kuona unamaendeleo atakuja kuona aibu na anaweza akakuomba msamaha Ila tu usije ukajiloga kurudiana naye.

Cha mwisho sali sana na jitahidi kukaa hata miezi 6 bila kujihusisha na mahusiano rasmi unaweza ukapata MTU wa kupita naye tu Ila sio kujifanya umependa moja kwa moja we mkunane then kila MTU na mambo yake....am sure huyo mzee utamsahau mazimaaaaa!!! na kama umri umeenda sana we jenga maisha yako swala la ndoa linahitaji muda na sio lazima sana, maana ukikurupuka utaishia kwenye NDOA NDOANO.... mtakahela,
 
Wanawake mahala pekee tunapokosea ni kwenye maneno, huwa tuna maneno sana hasa pale tunapowasaidia wenzi wetu wanapokwama,

I'm not supporting him kwamba alikuwa sahihi kutokujishughulisha, Ila nina wasiwasi sana na kauli zako ulizotumia wakati unamkumbusha majukumu yake!

Inawezekana pia kakupa mtihani mdogo wa kupima kiwango chako cha uvumilivu and you came out with your true colours!

Mwanaume hata umsaidie kiasi gani cha pesa, kitakachompa thamani ni namna gani utajali utu wake na heshima unayompatia na hii ni tofauti kabisa na sisi wanawake!
 
Daby,

Sure , hili nalo ni tatizo maana kila mtu analalamika kivyake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…