mtakahela
JF-Expert Member
- Jun 11, 2016
- 801
- 1,268
Habari zenu wakuu
Nimevumilia ila nimeshindwa nahitaji msaada wenu huyu baharia mzee nimfanye nini .
Maana aliyonifanyia nahisi hata nikisema ni move on sitaweza natamani na mie nimfanyie kitu cha aibu na fedheha kama alivyofanya kwetu
Uhusiano wangu na huyu baba umedumu kwa mwaka mmoja na miezi kadhaa. Na tulivyokua pamoja tulipanga mengi kwa muda mfupi ili hata huko mbeleni kila mmoja aweze kusimamia majukumu yake kama baba au mama
Alinitamanisha tufanye biashara pamoja hivyo na yeye awe msimamizi wangu. Sikua na hela ya kutosha ikanibidi niongee na mama nikamuelezea kila kitu akanipatia pesa, nikampa baharia apige kazi.
Hapo sikua na wasiwasi maana jamaa ni mtu wa dini, kanizidi miaka mingi na pia anajiweza kwa biashara zake na nyumbani tayari anajulikana kama mtarajiwa
Mwezi wa sita mwaka huu alifiwa na mama yake tukaenda kuzika ila arobaini mie sikuweza kwenda.
Hatukukaa sawa akafiwa na babu yake mzaa mama yake.
Basi tangu hapo mawasiliano yamekua ya shida maana mwenzangu alikua hafanyi chochote cha kuingiza pesa. Kila siku ananiomba nimtumie pesa. Nikamuuliza hivi kama tungekua tunaishi pamoja na tuna watoto ingekuaje kama wewe hutaki kujishughulisha. kwamba tangu mwezi wa sita mpaka leo bado unaomboleza tu? Basi akawa kimya ukimpigia anasema alikua busy na shughuli za nyumbani na kama siamini nimpigie shangazi yake.
Sasa hivi mimi na yeye tumeachana kwa sababu ambazo hazieleweki maana hata nikimpigia simu tuongee yetu mimi na yeye hataki tuongee. Mwezi sasa hakuna meseji wala simu kupigiana.
Sasa mie nawaza nifanye kitu gani aumie zaidi yangu kwa maana kama kunila kanila sana, kuanzia kipochi manyoya mpka kipochi mapesa. Nyumbani ndio hivyo nimeshamtambulisha yeye na sasa hivi hata nikiulizwa sina la kujibu
Naombeni msaada wa mawazo nifanye kitu gani na yye ahisi maumivu ninayoyapata.
Shukrani
MICHANGO YA WADAU:
Nimevumilia ila nimeshindwa nahitaji msaada wenu huyu baharia mzee nimfanye nini .
Maana aliyonifanyia nahisi hata nikisema ni move on sitaweza natamani na mie nimfanyie kitu cha aibu na fedheha kama alivyofanya kwetu
Uhusiano wangu na huyu baba umedumu kwa mwaka mmoja na miezi kadhaa. Na tulivyokua pamoja tulipanga mengi kwa muda mfupi ili hata huko mbeleni kila mmoja aweze kusimamia majukumu yake kama baba au mama
Alinitamanisha tufanye biashara pamoja hivyo na yeye awe msimamizi wangu. Sikua na hela ya kutosha ikanibidi niongee na mama nikamuelezea kila kitu akanipatia pesa, nikampa baharia apige kazi.
Hapo sikua na wasiwasi maana jamaa ni mtu wa dini, kanizidi miaka mingi na pia anajiweza kwa biashara zake na nyumbani tayari anajulikana kama mtarajiwa
Mwezi wa sita mwaka huu alifiwa na mama yake tukaenda kuzika ila arobaini mie sikuweza kwenda.
Hatukukaa sawa akafiwa na babu yake mzaa mama yake.
Basi tangu hapo mawasiliano yamekua ya shida maana mwenzangu alikua hafanyi chochote cha kuingiza pesa. Kila siku ananiomba nimtumie pesa. Nikamuuliza hivi kama tungekua tunaishi pamoja na tuna watoto ingekuaje kama wewe hutaki kujishughulisha. kwamba tangu mwezi wa sita mpaka leo bado unaomboleza tu? Basi akawa kimya ukimpigia anasema alikua busy na shughuli za nyumbani na kama siamini nimpigie shangazi yake.
Sasa hivi mimi na yeye tumeachana kwa sababu ambazo hazieleweki maana hata nikimpigia simu tuongee yetu mimi na yeye hataki tuongee. Mwezi sasa hakuna meseji wala simu kupigiana.
Sasa mie nawaza nifanye kitu gani aumie zaidi yangu kwa maana kama kunila kanila sana, kuanzia kipochi manyoya mpka kipochi mapesa. Nyumbani ndio hivyo nimeshamtambulisha yeye na sasa hivi hata nikiulizwa sina la kujibu
Naombeni msaada wa mawazo nifanye kitu gani na yye ahisi maumivu ninayoyapata.
Shukrani
MICHANGO YA WADAU:
=====Wanawake mahala pekee tunapokosea ni kwenye maneno, huwa tuna maneno sana hasa pale tunapowasaidia wenzi wetu wanapokwama,
I'm not supporting him kwamba alikuwa sahihi kutokujishughulisha, Ila nina wasiwasi sana na kauli zako ulizotumia wakati unamkumbusha majukumu yake!
Inawezekana pia kakupa mtihani mdogo wa kupima kiwango chako cha uvumilivu and you came out with your true colours!
Mwanaume hata umsaidie kiasi gani cha pesa, kitakachompa thamani ni namna gani utajali utu wake na heshima unayompatia na hii ni tofauti kabisa na sisi wanawake!
====Kwanza nasikitika kwa mawazo yako dada yangu, labda nikupe elimu hii ndogo juu ya kufiwa na maombolezo
Sikuungi mkono adhima yako ya kutaka mkomoa mwenzio kwa sababu;
1. Hajadhamiria
2. Kafiwa mara mbili
Turudi kwenye elimu.
Ipo hivi kwa wastani ni inamchukua miaka miwili mwanadamu kukamilisha maombolezo (kiimani) nikiwa na maana kuwa roho za wawili hao kuweza kutengana na kuamua kuendelea na maisha mengine.
Kwani hujawai kuona mtu kafiwa na mke au mpenzi akakosa hamu ya kujamiiana kwa hadi miaka miwili?, sasa ndio sawa na huyu mwenzako kumbuka kafiwa na mama yake mzazi na pia bado kafiwa na babu mzaa mama ndani ya mwaka mmoja.
Nikuulize swali, je ulikuwa unamfahamu mama yake na mwenzio?, na je, unafikiri mwenzio hakuwa amemwambia mama yake malengo yake kwako kama wewe ulivyomshirikisha mama yako?
Imagine ndio wewe mama yako angefariki, unajua kuwa ungeumia sana kukumbuka kuwa mama yako hataweza kushuhudia ndoa yako na umpendaye?
Dada yangu jirudi upya na urudishe upendo kwa huyu kijana, tambua kuwa bado yupo kwenye maombolezo na wewe ndio mtu sahihi ambaye ungempunguzia muda wa maombolezo kwa kuifanya roho yake iwe bize kwako.
Ingekuwa labda amechepuka ungekuwa na haki ya hizi lawama ila hivi amepata matatizo una hizi lawama jichunguze upya jitathimini na ujiulize ni wapi umeitoa hii hali ya kutokuwa na huruma.
Mungu si Athuman dada yangu unaweza jikuta umepata pigo kubwa kuliko huyu kijana pengine hata ukawapoteza wazazi wote wawili kwa mpigo alafu upo na mhuni atakayekutosa hapo hapo utalia na kusaga meno ukimkumbuka huyu jamaa ambaye wakati huo atakuwa karibu na wewe ila ndio hivyo ameshaoa mwanamke mwingine na ana familia yake. BEWARE my sister.
=====mtakahela,
Pole mkuu sasa umeweka habari vizuri zaidi, hapa nitakuuliza maswali machache yatakayosaidia kukupa mwanga wa hatma yenu
1. Vipi huyu mwenzako anao ndugu wa karibu unaowasiliana nao au uliokuwa unawasiliana nao mf. Wadogo zake au mkubwa wake
Kama ulikua/unawasiliana na ndugu zake wao wanamuongeleaje ndugu yao je mabadiliko aliyonayo ni kwako tu au kwenye kila nyanja ya kimaisha (amepoteza dira ya maisha?) kama amepoteza dira ya maisha basi jua tatizo ni kubwa unapaswa kumsaidia kurudi kuwa kawaida
Ila pia kama amepoteza dira kwako pekee hili ni tatizo kubwa zaidi (kwa uhusiano wenu) na utalijua hili kupitia ndugu zake kama wanakwepa kukwambia wazo la ndugu yao juu ya hatma yenu basi jua labda mpo wawili au zaidi au pia huwenda ameamua kutokuoa kabsa baada ya maswahibu yaliyotokea.
Wanadamu tupo tofauti sana ila kwa ukubwa naona huyu mwenzio amepata matatizo ya kimtazamo unajua anaweza kuwa hakuja kwenye msiba kwenu kutokana na hofu ya kukumbuka aliyoshuhudia kwenye msiba wa mama yake na mbaya zaidi ukute alikuwa ndio anayemuuguza wanaume ni very week emotionally ila wengi hawajui hili.
=====Kuna saa unaeeza ukahisi uwezi kumove on bila kufanya jambo, ili naye apate maumivu haitakupunguzia maumivu uliyonayo. Amini kwenye muda, muda ukisogea ipo siku utamsahau na itabaki kuwa historia.
Fanya yafuatayo.
1.mwambie rasmi kwamba tunaachana usikae njia panda kusubiri huenda kuna siku atabadili mawazo NO usisubiri ndo unajiumiza zaidi. Ushaona hakupendi basi amua kuachana naye.
2.JIFUNGIE LIAA MPAKA UTOE KILA AINA YA HASIRA ULIYONAYO. KISHA FUTAA KILA KUMBUKUMBU YAKE KWAKO KAMA NI MESEJI KAMA NI PICHA.
3.waambie wazazi wako hasa kinachoendelea sana sana mama yako.
4.jipe muda wa kuponyesha moyo wako na pia anza kufanya kazi kwa juhudi na penda kwenda sehemu zinazokuvutia. Usijifunge kwamba sitopenda tena japo ujipe muda kiasi kabla ujampenda mtu
=====mtakahela,
Pole sana ndugu...
Tafadhali sana, usije ukajaribu kufanya hicho kitu unachowaza cha kumuumiza huyu kibosile wako!
Huwezi kujua ni kitu gani kilichomfanya akawa hivyo, yawezekana ana stress nyingi tu au kuna tatizo kubwa limemkumba.
Kikubwa kwa kuwa unajua kwao, nenda ukutane na familia yake, watafutwe watu kama wawili wa karibu wakae nae pamoja na wewe aulizwe ni kitu gani kimemsibu au pengine hao watu tayari wanaweza kuwa na majibu!
Usiporidhika na majibu basi, ikiwezekana ingia ndani kwenye imani yako labda unaepushwa na jambo zito mbele yako!
Usichukue maamuzi ya ghafla utakuja kujijutia baadaye!
Take care.
=====Sweet Lee,
That is very correct, It is further said Relationship is a combination of two imperfect people.
Imperfection no 1. is the gender a female and a male. however, the traits differ you have to moderate them evenly to affirm the relationship. No 2 is adoptation each one has been adopted on her or his own way propelling to each and every kind of character, eventually after all this and other that we can't mention today, one needs to maintain the relationship with great care on a self awareness status.
The problem is, when relationship is at start there is true love and great respect, but when time goes and each has known the weakness of the other and that the true taste of love is no longer there this is where the junction is created even the treachery starts this is at a lengthy starting 7 - 10 years no one cares about the other unfortunately the woman thinks she is still in market.
When it goes to 15 years and above that is kubali yaishe it is amongst the few old age couples who successfully have crossed the ozone.
African relationship is entirely spoiled by crops especially women who tend to copy lifestyles of others without scrutinizing or comparing the possibilities of doing so.
People regret when it comes to age, if a man had just fucked his life during tender age when he is 50 he needs an assistance this is a covenant between God and human.
Life gets spoiled at this juncture and is late to adjust it.
So ladies I would advice you to form social educational groups to teach those who are arrogant or else say they don't care whether they find marriage potential, it is this is where you build a well built family.
Sweetie Lee,
Kazi ngumu iko hapo sababu wanasema relationship is a combination of two impafect people.
Ndio sababu ndoa za watu waliozeeka pamoja chache.
Binadamu ni ibilidi sana.
Maisha yana tafsiri nyingi sana.matatizo huja wakati mwingine kwa faida ya mwenye kukutwa na matatizo husika hapo mi nachoona kuna mawili
1. Misiba imetokea ili huyo jamaa yako ajue uhalisia wako katika kujali shida zako yaani kiwango cha uvumilivu kilichopo ndani yako pindi apatapo shida. Pia muda wa matanga unatofautiana kutokana na desturi za jamii husika, inawezekana wewe uliona amekaaa sana msibani kumbe desturi zao huenda tokea msiba umetokea matanga yanachukua muda mrefu, pia kuna jamii ambazo matanga yanachukua muda mfupi sana .hivyo inawezekana alivyokupima wewe kwa hilo tu la msiba ameona hutaweza kumvumilia pindi atakapopata matatizo yanayofanana na hilo.
2. Inawezekana kabisa Mungu amekusaidia wewe kujua uhalisia wa mwenzako juu yako na maanisha inawezekana tayari ana mtu mwingine ambaye inawezekana hana hela kama ulizonazo wewe ila yeye anajali na kuheshimu hisia za huyo jamaa ikiwa ni pamoja na kushiriki matanga kwa kipindi chote tangu jamaa huyo alipofiwa. Huenda wewe uliamini kuwa msaada wa fedha unaompa unatosha kwa 100% kutokukuacha na huenda uliamini hawezi kutafuta mwanamke mwingine .wanaume wengi wanapenda uwajali na kuwaheshimu bila kujali uwezo wake kifedha mwanamke yeyote anayefanya hivyo matatizo ya ndoa yake utayasikia mara nadra sana nayo ni yale yanayovumilika na kutengenezeka.
Ushauri wangu ili uwe na uhakika na unachokifanya wasiliana na shangazi yake ujue uhalisia kabisa maana unaweza kulipiza kisasi kumbe mtu mwenyewe anahitaji msaada wako kuliko kisasi, panoja na kuwa hajibu sms zako wala simu cha msingi mtumie shangazi yake ili hata unapofanya maamuzi uwe umejiridhisha kwa namna zote.ila kuhusu kisasi hata mimi sikushauri kufanya hivyo.
Sent using Jamii Forums mobile app