Mpaka sasa sielewi hatma ya maisha yangu ni ipi

Torabola

Member
Dec 8, 2020
19
75
Siamini macho yangu kama inafika kipindi mtu unafilisika mpaka mawazo, yaani hujui nini cha kufanya ili maisha yasonge mbele lkn ukweli mtupu haya ndo ninayopitia Mtanzania mwezenu.

Historia yangu kiufupi ni hivi, Mimi ni muhitimu chuo kikuu (UDSM) kada ya ualimu wa sanaa (Art), na kama mjuavyo hii fani ina changamoto katika ajira.

Nilihitimu mwaka 2018 na baada ya nilijaribu kutuma maombi shule mbalimbali bila mafanikio, lakini Mola hamtupi mja wake nilipata kibarua kimoja hivi ambacho nashukuru Mungu kilifanikisha kunivusha sehem A kwenda B japo nilifanya kwa muda wa miaka 2.

Niliweza ku-save kiasi cha sh mil 2 hivi ndani ya huo muda na kibarua kilikoma mwezi wa kumi mwaka huu (2020).

Mpaka sasa nna mwezi wa tatu huu niko tu ndani kiufupi nimenasa katika jela ya mawazo yani kila biashara ninayoifikiria nahisi haiwezekani mpaka imepelekea naugua ulcers kwa mawazo nilonayo.

Jamani jela ya kifikra ni mbaya mno, maana nafikiria hiki kitu nilichokitafuta kwa miaka 2 kikipotea itakuaje!

Bahati mbaya sina hata wazazi wa kunipa motisha kwamba wapo nyuma yangu kwani walifariki nikiwa mdogo.

Mpaka najuta kabisa kwanini nilitumia muda mwingi kwenye kusoma halafu nakuja kufanya kazi ambazo ni out of field.

Sasa basi naombeni ushauri wenu jamani nifanye nini mana dahhh hela nilonayo ndiyo inazidi kupukuchuka, maisha ya Dar kila siku ni hela yani nahisi kukata tamaa.
 

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
5,196
2,000
Mkuu Ingia mtaani bila kujali chochote, mi nilishawahi fanya kazi ambayo hata sijawahi kuwaza hiyo yote ilikuwa tu nijikipi bize na maisha huku mzazi wangu akiwa anafanya kazi state. Sikujali kuhusu hilo.

Maisha ya kibongo sio vile kama unavyofikiri, bali ni kujisacrifice.

Ukweli ni kuwa hakuna ajira Ingia mtaani fanya chochote halali kujipatia riski

Cheti weka pembeni mzee
 

kianja kyamutwara

Senior Member
Nov 4, 2020
108
225
Ni jambo la kawaida sana, na changamoto kwa mwanadamu ni kawaida. Ila nilihitaji nikushauri. Kwanza usijaribu kuweka mtaji wako kwenye maswala yanayohitaji muda ili kupanuka mfano maswala ya mitandao, yaani Tigo Pesa mpesa n.k pia usijaribu kufungua duka lolote kiufupi usifanye biashara ambayo inahitaji muda zaidi ya miezi mitatu au sita huku ukiwa unasubir ichanganye.

Sasa utafanya nini. Tenga kiasi kidogo kama laki nne. Tafuta mabanda ya kukodi mfano ukienda maeneo ya Kibamba kuna mabanda yanakodishwa kila msimu wa ufugaji unamlipa elfu hamsini tu. Au Bunju maeneo ya Mabwe kuna mabanda mengi sana, weka mabroila ya laki kama tatu utatumia kama laki mbili tu mpaka yanakomaa ukibahatika kupata soko utapanua mtaji na utapata pa kuanzia. Ukiitaji ushauri zaidi nifate dm nitakusaidia mhanga mwenzangu.
 

Cos101

Senior Member
Sep 16, 2020
164
250
Pole sana mkuu.

Dar ndo nyumbani? Umepanga? Una utayari wa kufanya biashara? Kiasi cha pesa ulichonacho kinatosha kuanzisha biashara ndogo ndogo kadhaa na kuweza kukusukuma kimaisha? Ukiona inafaa tuwasiliane PM, naweza kujitolea kukupa skills za biashara flani ikakupush. Ukiwa na hata laki tano tu unaanza vizuri
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,271
2,000
Dogo hiyo 2 m bado ipo au umeshaigegedea? Kama bado ipo nenda dukani uchukue pikipiki uanze kupiga bodaboda. Ila pita VETA upige kozi ya kuendesha abiria kwa wiki 2 au 4 ukimaliza hapo anza kubeba abiria. Naona vijana wanatoka kidogo kidogo. Hili ndiko deal la fasta kwa vijana huku mjini. Ila uwe mwangalifu usije ukatekwa!
 

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
125,911
2,000
Mkuu Ingia mtaani bila kujali chochote, mi nilishawahi fanya kazi ambayo hata sijawahi kuwaza hiyo yote ilikuwa tu nijikipi bize na maisha huku mzazi wangu akiwa anafanya kazi state. Sikujali kuhusu hilo.
Maisha ya kibongo sio vile kama unavyofikiri, bali ni kujisacrifice.
Ukweli ni kuwa hakuna ajira Ingia mtaani fanya chochote halali kujipatia riski

Cheti weka pembeni mzee
Ushauri ni huu sema ndio hivyo wanaona aibu na aibu ndio inawafikisha hapa kwenye kutafuta hela hakuna aibu

Yaani mimi kikubwa napata hela yangu sijali nani anasema nini
 

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
125,911
2,000
Mkuu wa kuanzia ili asiwe na stress Bora aanzie huko wakat anatafuta ajira nyingine maana akikaa na hyo ml 2 muda mfup Sana itakata na biashara za uchuuz wa vtu itapotea yote Bora anunue pkpk mtaji uwe mafuta tu, atakuwa hakosi angalau 15
Na ikiibiwa je atafanya nini
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
42,164
2,000
Aisee nimeona haya
1. Una 2m inakupa mawazo cha kuifanyia hadi unapata vidonda vya tumbo
2. Unaumia kufanya kazi zilizo na nje ya field yako

Nimekumbuka msemo kuna mtu analia kakosa viatu wakati kuna asie na miguu yupo kimya.
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,713
2,000
Ni jambo la kawaida sana, na changamoto kwa mwanadam ni kawaida. Ila niliitaji nikishauri. Kwanza usijaribu kuweka mtaji wako kwenye maswala yanayoitaji mda ili kupanuka mfano maswala ya mitandao, yaan tigo pesa mpesa n.k pia usijaribu kufungua duka lolote kiufupi usifanye biashara ambayo inaitaji mda zaid ya miez mitatu au sita huku ukiwa unasubir ichanganye. Sasa utafanya nn. Tenga kias kidogo kama laki nne. Tafuta mabada ya kukodi mfano ukienda maeneo ya kibamba kuna mabanda yanakodishwa kila msimu wa ufugaji unamlipa elfu hamsini tu. Au bunju maeneo ya mabwe kuna mabanda mengi sana,weka mabroila ya laki kama tatu utatumia kama laki mbili tu mpaka yanakomaa ukibahatika kupata soko utapanua mtaji na utapata pa kuanzia. Ukiitaji ushaur zaid nifate dm nitakusaidia mhanga mwenzangu
Pole sana mkuu.

Dar ndo nyumbani? Umepanga? Una utayari wa kufanya biashara? Kiasi cha pesa ulichonacho kinatosha kuanzisha biashara ndogo ndogo kadhaa na kuweza kukusukuma kimaisha? Ukiona inafaa tuwasiliane PM, naweza kujitolea kukupa skills za biashara flani ikakupush. Ukiwa na hata laki tano tu unaanza vizuri
Nimefarijika sana kwa post hizi,vijana tusaidiane uwezo ukiwepo huwa naumia sana napoona post za graduates wakilia kufeli maisha.

Pole sana mkuu shikamana na hawa jamaa japo kwa ushauri wa kimawazo tu unaweza kusogea ila kumbuka wema unaotendewa humu na wewe uulipe kwa wengine kama ikiwa ndani ya uwezo wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,272
2,000
Nimefarijika sana kwa post hizi,vijana tusaidiane uwezo ukiwepo huwa naumia sana napoona post za graduates wakilia kufeli maisha.

Pole sana mkuu shikamana na hawa jamaa japo kwa ushauri wa kimawazo tu unaweza kusogea ila kumbuka wema unaotendewa humu na wewe uulipe kwa wengine kama ikiwa ndani ya uwezo wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa ndio vijana wapuuzi wa CCM na uvccm wakila msoto hakuna kuwaonea huruma *****.
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,271
2,000
Mkuu pikipiki zina risk sana mtoe uko unampoteza hela yenyewe anayo hiyohiyo
Siyo kweli! You are misinformed my friend Shunie! Kwa vile pikipiki itakuwa ya kwake kipato chote kwa siku kitakuwa cha kwake. Akiwa na nidhamu ya kazi huko ndiko atapata mtaji wa biashara zingine! Kwa kuanzia siyo mbaya!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom